Pooor Pinda. kweli hii nchi ina viongozi mizigo. uwezo wake na akili yake na uzoefu wake ameweza kuchambua off-points kama hizi. kweli tuna kazi. Kwanza hafahamu kwamba muda ni kitu muhimu katika kila jambo. Ni vigumu kuwashawishi watu waamini jambo ambalo limeshindwa kurekebishika kwa miongo mitano au nusu ya karne, halafu utuambie bado linazungumzika. Ukweli ni kuwa sisi kizazi kipya tunaona muungano hauna maslahi tena na kwa hakika umepitwa na wakati. istoshe muungano unatokana na pilika pilika za vita baridi vya wakati ule ambapo wababe wa vita ile walishasahau na athari zake zote zilishafanyiwa marekebisho makubwa. rejea ukuta wa Berlin na kuvunjika kwa USSR au Soviet Russia na reforms au mageuzi yaliyofanika China. Watu wengi wa aina ya Mtoto wa Mkulima wanaogopa mabadiliko kwa vile; mosi, wanafaidika na mfumo wa hovyo uliopo na hawana uhakika iwapo wata-sustain ulaji iwapo mabadiliko yatatokea. pili, watu wengi hawana taaluma ya kuona mambo ya mbele au jamii yetu haina taasisi za kufanya strategic studies ambazo huweza kufanya prdictions kuhusu expected outcomes for any reforms in 50 to 100 years ahead. Kwa hiyo katika hali ya kila kitu kwenda gizani ndio maana kina Pm na nyinyiem yake wanaogopa mabadiliko.
nitawapa mfano, nchi ya China ambayo leo ni tishio kwa uchumi wa dunia, baada ya kuwa na uchumi wa kijamaa kwa miaka 30 tokea 1948 baada ya mapinduzi ya kizalendo, walifanya utafiti na kuona iwapo mfumo ule ulikuwa sahihi na iwapo ungewapeleka kuwa China ya karne ya 21. Ile study iligunduwa kuwa China ilikuwa na nafasi kubwa ikiwa mabadiliko makubwa yangefanyika na ndani ya mika 50, mabadiliko yale yangeifanya kuwa uchumi mkubwa wa dunia. mwaka 1978, bila kusita, China ilifanya mageuzi makubwa ya kiuchumi, kutoka uchumi wa kijamaa kwenda uchumi wa soko. Miaka thelathini baadaye, nyote ni mashahidi. kila kitu, whether uko Los Angeles, Cape Town, Glasgow, au Hokkaido, MADE IN CHINA ndio habari ya mjini. si nguo, tab pc, super computer wala smart phone unayoitumia kusoma uzi huuu.
Mimi namhamsisha Mkuu Pinda na wenzake magamba, wasiogope mabadiliko, hawawezi kuyazuia. Istoshe, dunia inabadilika kila sekunde nao hawezi kuuzuia muda kwa mikono, ila ni wao kubadilika ili waendelee kuwa "relevant".
Sorry kwa post ndefu anyway.
Capital