Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Watanganyika wenzangu kwa maneno ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, suala la Tanganyika litabakia kuwa historia.

Cc; Nguruvi3 Mag3 Mzee Mwanakijiji JokaKuu WildCard Mkandara Ngongo

Tutabaki kupambana kwenye forums tu, wako wapi Watanganyika watakaoweza kuirudisha Tanganyika yao.
Ritz,

..tatizo ni wa-Zanzibari.

..wanataka mamlaka kamili.

..sisi tunaweza tusidai Tanganyika, lakini hayo madai ya wa-Zanzibar tutaendelea kupiga chenga mpaka lini?


cc Bobwe, takashi, Barubaru, Mohamed Said, gombesugu
 
Ritz,

..tatizo ni wa-Zanzibari.

..wanataka mamlaka kamili.

..sisi tunaweza tusidai Tanganyika, lakini hayo madai ya wa-Zanzibar tutaendelea kupiga chenga mpaka lini?


cc Bobwe, takashi, Barubaru, Mohamed Said, gombesugu

Wanzanzibari wanataka Zanzibar huru. Mamlaka kamili ni njia tu , ya kuelekea kwenye uhuru kamili. Watanganyika waoga na wanaendelea kutishwa na kivuli cha Baba wao wa Taifa. Poleni sana.
 
Mimi naona jambo la muhimu kwa sasa ni kuangalia upya mfumo huu wa serikali mbili na kuufanyia marekebisho lakini mfumo wa sijui serikali Tatu,Nne ,Tano Mara shirikisho ni kujiongezea matatizo yasio ya msingi
kwa nini usipendekeze serikali moja?kama kweli sisi ni ndugu moja au unaogopa Zanzibar itamezwa na kwa nini kwenye serikali moja isiwe tanganyika ndio imemezwa, wacha ujinga wa mawazo kama wabunge wa ccm kutoka bara
 
Ukizungumzia Tanganyika, indirectly unazungumzia Zanzibar! Wewe fuatilia hata humu, mjadala umeanzia suala la Tanganyika lakini hoja nyingi ni kuhusu Zanzibar! Kwa hiyo kwa kifupi Pinda amezungumzia kuhusu Zanzibar!

Acha kumwekea maneno mdomoni...ambayo hajawahi kuyatamka huyo Kiongozi wa Nchi-Waziri Mkuu!

Wee unafikiri huyo Pinda anashindwa kutamka neno Zanzibar,ndo mpaka atumie neno Tanganyika!?...na tena kuleta ujumbe wa kimethali/kimafumbo kwa Wananchi wake!?

Fikra na tafsiri zako,jitahidi ubaki nazo mwenyewe na sio kuwazushia Viongozi wa Nchi humu mitandaoni!

Ahsanta sana.
 
Tafadhali bana. Kwani alichoongea pinda si ndo uhalisia?

Uhalisia uko wapi? Huyu si ndiye aliyesema Zanzibar si nchi? Angalia katiba ya Zanzibar inasemaje sasa?
Watu wa visiwani wanasema katika katiba yao, Zanzibar ni nchi halafu wewe unauliza Tanganyika ipi.Shame on you?
Sisi tunataka Tanganyika,iwe ya mkoloni au ya miaka mitatu baada ya uhuru mradi ni Tanganyika sisi tunaitaka.
 
Ritz,

..tatizo ni wa-Zanzibari.

..wanataka mamlaka kamili.

..sisi tunaweza tusidai Tanganyika, lakini hayo madai ya wa-Zanzibar tutaendelea kupiga chenga mpaka lini?


cc Bobwe, takashi, Barubaru, Mohamed Said, gombesugu

JokaKuu,

Shukran ndugu yangu,na niwia radhi naliadimika kiduchu.

Hapo nilipo-BOLD kwenye hiyo bayana yako,ndo mambo yoote!

Pana wakti humu humu-JF...nalifanza malumbano/mjadala kiduchu na Nguruvi3,kuhusu masuala haya haya ya Muungano!

Matokeo yake,nikamwambia yakua vile vifijo vyake na nderemo ya kushangilia yakua Tanganyika iko njiani na kuwabeza Wazanzibary kwa tashtit na kashfa! Yaani ilikua ni kama vile mbio za darini kuishia sakafuni!...basi iko siku nitakuja kumcheka! Sidhani kama alinifahamu maskini!

Maana ule wakti nilomuahidi ndo wakurubia mno...je Nguruvi3,hiyo Tanganyika ulokua ukiishangilia iwapi leo!?...si ulitaka Wazanzibary wafunge virago kwa haraka,na ati warejee kwao!? Isije tukakufungaishia weye hivyo virago...jihadahari!

Tena aliwahi ati kunicheka na pia kunifananiza kwa kebehi ati na Ahmed Rajab...pale mie nilipomwambia yakua ni bora nikajadiliane na wachache niwajuao na watakaonisikiza huko kwenye hizo corridors of power...kuliko kubaki humu-JF tukapigizana makelele yasokwisha! Daah!

Kwa kifupi,Jokakuu ndugu yangu...huku upande wa Tanganyika kama labda wangelipatikana japo watu milioni moja tu,wenye mitazamo na maono ya mbali kama weye...basi haya matafrani yoote haya na kupotezeana muda mitandaoni kwa kebehi na majadiliano yaso maana wala kusingekuwepo,asilan!

Na leo hii Watanganyika na Wazanzibary soote kwa pamoja tungalikua tunatazama mangineyo muhimu zaidi kwa maendeleo ya mataifa yetu haya machnaga!

Tuko pamoja,Mkuu!

Ahsanta.
 
Hi hoja ya mtoto wa mkulima ni dhaifu sana, tena sana! Kusema eti Tanganyika mnayoitaka ni ya mkoloni au ya miaka 3? Na eti kwa vile wengi wetu humu ndani hata hiyo Tanganyika ya miaka 3 hatukuwepo nalo sio hoja kabisa! Hivi tunapotaka KUOA/KUOLEWA ni kwamba tuliisha wahi kufanya hivyo kabla so tunayo experience au mambo tutakutana nayo huko huko!? Kipya hapo kitakua nini, jina au sehemu ninayoishi!? Leo hi hata tukibadiri jina la nchi, sema iwe Tanzania Bara au Tanganyika au vyovyote vile, hailete maana yoyote kwa mwananchi wa kawaida but tukiwa na usawa kwenye huu muungano nalazimika kuamini kwamba Tanzania bara itakua na mihela mingi cause kwasasa kila Tsh 100/= ninayo lipa kama kodi, Tsh 4/= zinaenda Zanzibar, hicho mimi kinanikela kwasababu nachangia kitu kisicho na faida yoyote kwangu, kama jina ndio tatizo basi tuwe na serikali 1 tu na iitwe Tanzania kama ilivyo leo na Zanzibar na Pemba iwe mikoa kama ilivyo Dar au Iringa na Mwanza, faida ya hiyo, kwanza hakutakua na manung'uniko na pia hata ukubwa wa serikali utapungua. Tumeshindwa kutatua migogoro hi ya muungano kwa miaka 50 halafu unadai eti hi migogoro yote inazungumzika, hivi kama sio wenda wazimu huo ni nini? Si ndio yale yale ya mchungaji Msigwa anayoyasema kila siku kwamba "A Problem cannot be solve in the same way always" Kila siku tumekua na vikao vya kutatua matatizo ya muungano (mengine hadi yaliwagharimu nafasi zao za kisiasa, rejea issue ya Abdul Jumbe, Seif Sharrif Hamad na hata ugombea mwenza wa Dr. Bilali sasa) lakini bado matatizo hayo na manung'uniko haiashi. Wengi wanaokubaliana na Pinda ndio hao hao wanaopenda ccm iendelee kua madarakani halafu hao hao wana lalamika kua nchi hi imeshindikana, hatuwezi kuendelea kuwaamini watu wenye njia zile zile za ku-solve matatizo yetu na wameendelea kushindwa kila wanapo omba ridha ya kutawala.
 
JokaKuu,

Shukran ndugu yangu,na niwia radhi naliadimika kiduchu.

Hapo nilipo-BOLD kwenye hiyo bayana yako,ndo mambo yoote!

Pana wakti humu humu-JF...nalifanza malumbano/mjadala kiduchu na Nguruvi3,kuhusu masuala haya haya ya Muungano!

Matokeo yake,nikamwambia yakua vile vifijo vyake na nderemo ya kushangilia yakua Tanganyika iko njiani na kuwabeza Wazanzibary kwa tashtit na kashfa! Yaani ilikua ni kama vile mbio za darini kuishia sakafuni!...basi iko siku nitakuja kumcheka! Sidhani kama alinifahamu maskini!

Maana ule wakti nilomuahidi ndo wakurubia mno...je Nguruvi3,hiyo Tanganyika ulokua ukiishangilia iwapi leo!?...si ulitaka Wazanzibary wafunge virago kwa haraka,na ati warejee kwao!? Isije tukakufungaishia weye hivyo virago...jihadahari!

Tena aliwahi ati kunicheka na pia kunifananiza kwa kebehi ati na Ahmed Rajab...pale mie nilipomwambia yakua ni bora nikajadiliane na wachache niwajuao na watakaonisikiza huko kwenye hizo corridors of power...kuliko kubaki humu-JF tukapigizana makelele yasokwisha! Daah!

Kwa kifupi,Jokakuu ndugu yangu...huku upande wa Tanganyika kama labda wangelipatikana japo watu milioni moja tu,wenye mitazamo na maono ya mbali kama weye...basi haya matafrani yoote haya na kupotezeana muda mitandaoni kwa kebehi na majadiliano yaso maana wala kusingekuwepo,asilan!

Na leo hii Watanganyika na Wazanzibary soote kwa pamoja tungalikua tunatazama mangineyo muhimu zaidi kwa maendeleo ya mataifa yetu haya machnaga!

Tuko pamoja,Mkuu!

Ahsanta.

..mimi kinachonishangaza ni kwamba viongozi wetu wanaona haya hata kutamka jina Tanganyika.

..Pinda anasema eti wengi wetu hatuijui Tanganyika, je aprili 64 kuna aliyekuwa anaijua Tanzania?

..sijui kama viongozi wako out of touch na kinachoendelea Zanzibar, au kiburi ndicho kinachopelekea wao kulazimisha muungano.
 
''Ee Mungu mrejeshe marehemu wetu Tanganyika, alituacha tukiwa bado tunamhitaji tena kwa sana''.
Ni maneno ya mlevi aliyekuwa chakali huku akiwa ameshikilia chupa iliyo onekana kuwa ina pombe ambayo ilikisiwa ni ya kienyeji. Wengi tulibaki tunatafakari ujumbe huo. Lakini akahoji tena kuwa
"wajumbe wa Bunge la katiba wameenda kujadili rasimu ya katiba au kudai posho"?
Wewe Mwananchi tafakari na pindi ikifika kwenye upigaji kura ufanyie kazi tafakari yako, kuunga mkono mlevi au kumpinga.
Mimi sijui maana siasa za nchi yangu zilinishinda nikaomba uraia wa nchi nyingine na sasa niko hapa kusalimia jamaa zangu huku alikozaliwa Bibi yangu
 
Nyie bishaneni tu kuhusu muungano kwani muonekano wa wengi unalenga upande mmoja "KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA FIKRA ZA MWENYEKITI WAKE" alihali baba wa taifa na waasisi wengine walisha toa fulsa ya vyama vingi, kilichoshamili katika muungano juu ya wazanzibari kutaka nchi yao ni pale ambapo wakitafakari faida ya kuungana kwa miaka hamsini na hasara yake na kujikuta hakuna liwalo hebu fikirieno kwa mfano wewe unafamilia ya watu kumi na jirani yako anafamilia ya watu ishilini kisha wewe mwenye watu kumi upewe kiasi kilicho chini ya mahitaji yako je utakubaliana? ilihali unauwezo wa kuzalisha kiasi kitakachotosheleza watu wako! ni haki kuaandamana lakini sasa miaka hamsini sasa vipi hapo kunanini Makame kamuoa Yasinta na John kazaa na Zahra je wanaodai Zanzibar na Tangayika watoto hawa waende wapi? SISI SOTE NI NDUGU. serikali moja ndo yenye manufaa kwa uma ila serikari tatu itazidisha mabilioni ya fedha kulipa wabunge huku msakatonge anakufa na njaa.
 
..mimi kinachonishangaza ni kwamba viongozi wetu wanaona haya hata kutamka jina Tanganyika.

..Pinda anasema eti wengi wetu hatuijui Tanganyika, je aprili 64 kuna aliyekuwa anaijua Tanzania?

..sijui kama viongozi wako out of touch na kinachoendelea Zanzibar, au kiburi ndicho kinachopelekea wao kulazimisha muungano.


JokaKuu,

Nimekusoma!

Nakubaliana na takriban yoote ulosema,na hayo pia mie binafsi hunitatiza mno!

Nalishawahi kuandika mara kadhaa humu...yakua hawa Viongozi/Wanasiasa hapo nchini ndo wa kulaumiwa,kwa kula namna na pia kwa mparaganyiko na hizi farka/rabsha zoote zitokeazo!

Kwa kifupi,si mojawapo ya dasturi zao kwa Wanasiasa takriban woote humu duniani kuwa wakweli...na hili ndo tatizo kuu!

Yaani Watanganyika na Wazanzibary soote kwa jumla we are taken for granted!...mawazo na fikra zetu sisi Wananchi waduchu,tusiojiweza na tusio na Ilm,khasa wengi wetu tulio vijijini....sidhani kama kuna hata Mwanasiasa mmoja mwenye kuyathamini au kuyafanzia kazi kwa utuvu!? Daah!

Ndo maana utakuta kula kukacha hakwishi kauli au matamko yasomaana/yasoeleweka au kufahamika,tena toka kwa baadhi ya Viongozi/Wanasiasa wa ngazi za juu kabisa hapo nchini!? Daah!

Ahsanta.
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

Mbali na hilo, amesisitiza yeye na chama chake cha Mapinduzi wanataka mfumo wa serikali mbili na si tatu kama Rasimu ya Katiba ilivyopendekeza.

Amekiri kuwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo, utakuwa na misukosuko mingi, lakini utavuka salama.

Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Makao Makuu ya chama hicho, White House mjini hapa.

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema zipo hoja nyingi za msingi katika mchakato huo wa kutunga Katiba, lakini kubwa na litakalochukua muda mwingi ni muundo wa Serikali. Hata hivyo, alisema wazi msimamo wake na ule wa CCM kuhusu pendekezo lao la kuwa na Serikali mbili, kinyume cha Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu.

“Hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane, kwangu mimi bado Serikali mbili ni muundo mahsusi.

“Mwalimu Nyerere hata wakati ule alikaa na Tanganyika kwa kipindi kifupi, mwaka 1961 Tanganyika ikawa huru, 1962 tukawa Jamhuri, 1963 Zanzibar ikapata uhuru (baadaye alisema Uhuru wa bandia), mwaka 1964 ikazaliwa Tanzania.

“Tanganyika ya kikoloni ndiyo iliyokaa muda mrefu, hii nyingine ni kutoka mwaka 1961, 1962 na 1963. Ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii miaka 50 tuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunadai Tanganyika,” alihoji Pinda na kuongeza:

“Tanganyika ipi? Nikadai ile ya mkoloni? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu? Tanganyika wakati inazaliwa nilikuwa na miaka 13, Tanzania nilikuwa na miaka 16, naujua vizuri Muungano. Kuanzia pale sijui chochote kingine, kama ilivyo wengi wetu humu.

“Au wale waliozaliwa miaka 50 iliyopita, wanaijua vizuri zaidi Tanzania. Tanganyika ipi mnazungumzia? Maana haikuwapo zaidi ya ile ya kikoloni iliyokaa muda mrefu.”

Alisema njia bora ni kukaa chini na kuzungumzia matatizo ya muundo wa Serikali mbili na kuyaboresha kwa nia ya kusonga mbele kuliko kudai Serikali ya Tanganyika. Waziri Mkuu alisema si vyema kuanza sasa kujaribu muundo wa Shirikisho baada ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku akitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

“Pale kuna Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini angalia mambo yanavyokwenda sasa wakubwa wakikutana. Utasikia wanazungumzia ardhi, mara pasipoti.

“Haiwezekani miaka 50 baada ya Muungano tuanze majaribio ya Shirikisho. Aah, wapi tunataka kwenda. Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana,” alisema Pinda.

Huku akirejea kauli mbalimbali za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema hata hilo Shirikisho linalopendekezwa litakwama, kwa sababu Rais wake hatakuwa na ardhi, na kama nchi wanachama zitakataa kutoa ardhi, atafanyaje kazi zake.

Alisema tatizo lililopo ni utambulisho wa Zanzibar na suala la umiliki wa ardhi kwa Tanzania Bara wakiwa visiwani, ambayo alisema ni mambo yanayozungumzika.

“Suala hapa ni utambulisho wa Zanzibar ambalo hata hivyo si suala kubwa na tunaweza kulisahihisha. Pia liko suala la ardhi Zanzibar. Lakini wanaotaka ardhi huko, lazima wajiulize je, kweli iko ardhi ya kutosha,” alieleza.

Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba alisema, “Tumeanza mchakato wa kutunga Katiba, lakini tayari kuna changamoto zetu, lakini tumeanza kwa kuchagua Mwenyekiti wa Muda na kutengeneza Kanuni wiki ijayo zitakuwa tayari ili tulifikishe mwisho hili,” alisema na kuongeza:

Bunge Maalumu la Katiba limeanza vikao vyake wiki iliyopita, lakini wiki ijayo linatarajiwa kuanza mijadala baada ya kupitishwa kwa Kanuni na kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na hatimaye kuzinduliwa rasmi.

Hata hivyo, tayari kuanza hali ya sintofahamu kwa wabunge kuanzia kudai suala la nyongeza ya posho, hadi katika vikao vyao ya kazi ambako zimeshuhudiwa kauli zinazoashiria kazi nzito mbele na inayopaswa kuwa na udhibiti ili mijadala isitawaliwe na jazba na kutekwa na makundi yaliyowapeleka bungeni humo.

Aliwaomba wajumbe wa semina hiyo ya Jumuiya ya Wazazi kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, watimize majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.

Kwa hisani ya Habari leo.

Huyu Pinda hilo swali awaulize Watanganyika wenzake, Kule zanzibar wao wanataka Zanzibar yao kama anajitoa fahamu haijuwi Tanganyika ipi sisi tunataka Zanzibar yetu tu, mwache akae na kigugumizi chake
 
Ni kitu kigumu kwa mtu au kiongozi kujitangazia kwenye eneo lake kuwa ana nchi na eneo la mipaka kisha kuwa na vikosi vyake vya ulinzi,katiba,bunge,bendera,mahakama,wimbo wa taifa n.k,hebu nambie mkoa gani huko tanganyika unaoweza kufanya hivyo?kwa akili za kawaida tu unapata picha kuwa hao jamaa wanaojitangazia kuwa ni nchi kuwa hawataki muungano,zanzibar kwanza.
Chombo gani cha kimataifa kinaitambua znz?
Mbona Simba na Yanga wana bendera, nao ni mataifa? Bendera ni kitambaa umesahau.
Hivi znz ina vikosi vya ulinzi na usalama? Nani anamteua commissioner wa Police znz, nani mkuu wa majeshi ya znz?
Wimbo wa taifa unatosha kulifanya taifa kiwe taifa? Mbona kuna wimbo wa EAC, Je kuna taifa la EAC?
 
Hapana. Alikuwa anaongea na hawa hapa,

unnamed+(3).jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia wakati wa ufunguzi semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi Ngazi ya Taifa, mikoa na Wilaya nchini iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma Februari 22, 2014wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua semiana hiyo.

Kama walishindwa kuhoji alichowaambia basi ni watu wenye mili ya watu wazima lakini wenye akili za watoto tena wenye utapia mlo hawawezi kuhoji chochote ni mateka wa woga.
 
Back
Top Bottom