Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Mizengo Pinda: Mnaitaka Tanganyika ipi?.

Kwani Tanganyika umeungana na nani mbona cc Zanzibar tuko nje ya muungano tuna jeshi letu {j.k.u na kmkm na kvz na magereza} tuna wimbo wa taifa , rais , katiba , ardh mali ya serikal ya z'bar , rais wa zanzibar amepewa mamlaka na katiba ya z'bar kuigawa z'bar ki mikoa na wilaya tuna bunge , mahakama kimebaki nn kitakachowafanya muamin km cc tuko nje ya muungano ila tunafanya danganya toto
 
Mimi naona jambo la muhimu kwa sasa ni kuangalia upya mfumo huu wa serikali mbili na kuufanyia marekebisho lakini mfumo wa sijui serikali Tatu,Nne ,Tano Mara shirikisho ni kujiongezea matatizo yasio ya msingi

Waongo wakubwa kwa nini hawataki kusema serikali moja ? wote wanafyata mkia kwa waunguja , wanaogopa nini serikali moja kama kweli wanapenda muungano kwa dhati
Serikali mbili ni ulaji unawasumbua

 
Hatutaki Tanganyika ya ukoloni wala ile iliyoishi miaka mitatu tu baada ya uhuru. Tunataka Tanganyika mpya itakayoongozwa kwa misingi ya utawala bora na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kasi kama ile ya nchi za asia.
 
hivi nasi tunajivunia kuwa tuna waziri mkuu mwenye kuwatetea wazanzibar tu?
kwani yeye anatka tuwe na tanganyika ipi?

nasisi watanganyika tunataka tuwe na serikali yetu yenye katiba yetu kama wazzanzibar walivyo
hivi kwanini wanatinyima haki yetu ya kuwa na serikali yetu? hawa viongozi wa sisiem wana nini?
wanaota ndoto za usiku wakati ni mchana sasa? haaaa wanatushangaza sana hasa hii serikali ya ksisiem
inavyotaka kuwa na serikali mbili huku ikiona inatukalia makooni siye tuko kimya kama wanyama vile
na sisi ni watu jamani nyie ni watanganyika kweli kama siye au wenzetu mmeloea hapa haaa!!!
 
mkuu umesema kweli kabisa ungekuwa karibu ningekupandisha daraja
maana naona hawa viongozi wa kisieseem wamekaliwa na waznz hawaoni wala kusikia
Hatutaki Tanganyika ya ukoloni wala ile iliyoishi miaka mitatu tu baada ya uhuru. Tunataka Tanganyika mpya itakayoongozwa kwa misingi ya utawala bora na kuwaletea maendeleo wananchi wake kwa kasi kama ile ya nchi za asia.
 
Nyerere aliasisi Muungano akitarajia Kuwa Muungano huu Analojia utakuwa ukijiboresha kulingana na wakati yaani Muungano Digtal Sidhani Kama Nyerere alitaka Muungano ubaki Kama ulivyo pasipo Kuwa Muungano tulivu Kama muungano wa kule U.S.A au kule UK kwa Malikia . Tiba Pekee na nzuri ni Kuwa na Serikari Moja tu Yaana ZNZ atawale Gavana kisha Bara atawale Gavana na Rais awe Mmoja tu na makamu wake wahamie Dodoma hakika huu Mvutano Kati ya Visiwa vyenye watu 1.5 million tu na Nchi kubwa ya watu million 43 utakwisha na Nchi kubwa itaepuka kupelekeshwa na watu wachache wajanja kuliko wengi wapole.
Nakuunga mkono kabisa serikali moja suluhisho hizo 2 au 3 ni kwa maslahi ya vikundi na kwa faida ya watu wachache
 
Methali: KILA PENYE ZANZIBAR PANA TANGANYIKA - Aidha kiwaziwazi au kiwiziwizi.
 
hadi leo hii kuna watu bado eti wanaota ndoto ya Serikali moja ??
kumbuka kwamb Muungano huu ni wa nchi mbili huru, na katu kwetu sisi Wazanzibar hatupo tayari kupoteza identity yetu ya asili kwa kusarenda kumezwa na Tanganyika, iliyojivisha Utanzania!!
Ikiwa CCM mumeshindw kutafuta ufumbuzi wa kero za Muungano, Wazanzibar tayari tumeshatatua tatizo hilo kupitia Muungano wa Mkataba (60%) ili kila mshirika awe na Uhuru wa kujiamulia mambo yake!!
Binadamu kuota ndoto siyo vibaya na huwezi kuizuia ndoto kwa sababu ndiyo matamanio ya kibinadamu.

Disappointment ni sehemu ya maisha kwa binadamu ili kuyakamilisha mapungufu yake.

Kujivika usemaji wa wananchi wa Zanzibar ili kuharalisha hoja yako ni moja ya sign katika mapungufu ya hoja yako. Hata kama wananchi wa Zanzibar wameishafikia uamuzi kuhusu Muungano tofauti na mawazo yangu basi sioni kama hilo ni tatizo lakini kumbuka kuwa aliyekiunganisha kwa kiasi kikubwa sana ndiye anayeweza kukiachanisha. Ninasema hivi nikiwa na maana kuwa, huu muungano uliletwa na viongozi na siyo wananchi, na kutokana na mantiki hiyo, ni viongozi hao hao kwa matakwa hayo hayo ndiyo watakao ubadilisha!.

Sisi tuendelee tu na matamanio ya kibinadamu.
 
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

Mbali na hilo, amesisitiza yeye na chama chake cha Mapinduzi wanataka mfumo wa serikali mbili na si tatu kama Rasimu ya Katiba ilivyopendekeza.

Amekiri kuwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bunge unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo, utakuwa na misukosuko mingi, lakini utavuka salama.

Pinda aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya viongozi na watendaji wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwenye Makao Makuu ya chama hicho, White House mjini hapa.

Pinda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, alisema zipo hoja nyingi za msingi katika mchakato huo wa kutunga Katiba, lakini kubwa na litakalochukua muda mwingi ni muundo wa Serikali. Hata hivyo, alisema wazi msimamo wake na ule wa CCM kuhusu pendekezo lao la kuwa na Serikali mbili, kinyume cha Rasimu ya Katiba inayopendekeza Serikali tatu.

"Hata ukiniamsha usingizini usiku wa manane, kwangu mimi bado Serikali mbili ni muundo mahsusi.

"Mwalimu Nyerere hata wakati ule alikaa na Tanganyika kwa kipindi kifupi, mwaka 1961 Tanganyika ikawa huru, 1962 tukawa Jamhuri, 1963 Zanzibar ikapata uhuru (baadaye alisema Uhuru wa bandia), mwaka 1964 ikazaliwa Tanzania.

"Tanganyika ya kikoloni ndiyo iliyokaa muda mrefu, hii nyingine ni kutoka mwaka 1961, 1962 na 1963. Ikazaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii miaka 50 tuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunadai Tanganyika," alihoji Pinda na kuongeza:

"Tanganyika ipi? Nikadai ile ya mkoloni? Kipi kimo katika Tanganyika ya miaka mitatu? Tanganyika wakati inazaliwa nilikuwa na miaka 13, Tanzania nilikuwa na miaka 16, naujua vizuri Muungano. Kuanzia pale sijui chochote kingine, kama ilivyo wengi wetu humu.

"Au wale waliozaliwa miaka 50 iliyopita, wanaijua vizuri zaidi Tanzania. Tanganyika ipi mnazungumzia? Maana haikuwapo zaidi ya ile ya kikoloni iliyokaa muda mrefu."

Alisema njia bora ni kukaa chini na kuzungumzia matatizo ya muundo wa Serikali mbili na kuyaboresha kwa nia ya kusonga mbele kuliko kudai Serikali ya Tanganyika. Waziri Mkuu alisema si vyema kuanza sasa kujaribu muundo wa Shirikisho baada ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, huku akitolea mfano wa Shirikisho la Afrika Mashariki (EAC).

"Pale kuna Shirikisho la Afrika Mashariki, lakini angalia mambo yanavyokwenda sasa wakubwa wakikutana. Utasikia wanazungumzia ardhi, mara pasipoti.

"Haiwezekani miaka 50 baada ya Muungano tuanze majaribio ya Shirikisho. Aah, wapi tunataka kwenda. Tanzania Bara na Zanzibar wana historia ya udugu na ushirikiano. Ukaribu, lugha moja na kuoleana," alisema Pinda.

Huku akirejea kauli mbalimbali za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema hata hilo Shirikisho linalopendekezwa litakwama, kwa sababu Rais wake hatakuwa na ardhi, na kama nchi wanachama zitakataa kutoa ardhi, atafanyaje kazi zake.

Alisema tatizo lililopo ni utambulisho wa Zanzibar na suala la umiliki wa ardhi kwa Tanzania Bara wakiwa visiwani, ambayo alisema ni mambo yanayozungumzika.

"Suala hapa ni utambulisho wa Zanzibar ambalo hata hivyo si suala kubwa na tunaweza kulisahihisha. Pia liko suala la ardhi Zanzibar. Lakini wanaotaka ardhi huko, lazima wajiulize je, kweli iko ardhi ya kutosha," alieleza.

Akizungumzia Bunge Maalumu la Katiba alisema, "Tumeanza mchakato wa kutunga Katiba, lakini tayari kuna changamoto zetu, lakini tumeanza kwa kuchagua Mwenyekiti wa Muda na kutengeneza Kanuni wiki ijayo zitakuwa tayari ili tulifikishe mwisho hili," alisema na kuongeza:

Bunge Maalumu la Katiba limeanza vikao vyake wiki iliyopita, lakini wiki ijayo linatarajiwa kuanza mijadala baada ya kupitishwa kwa Kanuni na kuchaguliwa kwa Mwenyekiti na hatimaye kuzinduliwa rasmi.

Hata hivyo, tayari kuanza hali ya sintofahamu kwa wabunge kuanzia kudai suala la nyongeza ya posho, hadi katika vikao vyao ya kazi ambako zimeshuhudiwa kauli zinazoashiria kazi nzito mbele na inayopaswa kuwa na udhibiti ili mijadala isitawaliwe na jazba na kutekwa na makundi yaliyowapeleka bungeni humo.

Aliwaomba wajumbe wa semina hiyo ya Jumuiya ya Wazazi kuwaombea wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, watimize majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.

Kwa hisani ya Habari leo.

Huwa nasikitika pale watu wazima na viongozi wakubwa wanapoongea bila kufikiria sawasawa. Tatizo halijawahi kuwa Serikali ya Tanganyika. Watu hawana shida na serikali ya tatu hapa. Ila watu wanachosema ni kuwa kama Zanzibar ina haki ya kuwa na serikali na Kama Zanzibar ni sehemu ya Muungano huo basi na Tanganyika iwe na serikali yake. Kama Zanzibar ina haki ya kuwa Nchi huru same applies kwa the other party.

Kwa kifupi watu wanataka kusema kuwa na serikali mbili ni uhuni. Hasa pale nchi moja inapokuwa na serikali yake na nchi ya pili haina.

Nadhani wanatakiwa kufikiria upya na kuacha ubabaishaji kwenye hili jambo.

As for me na nionavyo ni ama Tuwe na serikali moja au kama wenzetu watakomalia kubaki na yao basi tuwe na serikali Tatu. Ila Tukiwa na serikali tatu kwa sababu tu kuna watu hawakuona kuwa hawana haki na haja ya kuwa na serikali yao ndani ya muungano, hii nitaitafsiri kuwa ni moyo wa ajabu kabisa wa kupelekea kuongeza matumizi ya fedha chache ambazo tayari hatuna mpaka tunadaiwa. Kwa hiyo tukiwaza kama wenye akili sawasawa ni kwamba Tunahitaji serikali moja ili muungano uwe sawa. Vinginevyo Tuvunje Muungano ili kila nchi iwe huru na iwe na serikali yake!

Udugu? Kuoleana? Huu ni upuuzi. Hata sasa kuna waliooa Zaire na Umarekani. Mwambieni Mheshimiwa Waziri akitaka kwenda kuoa ama kuoza Zanzibari atakuwa huru kwenda hata kama Muungano umevunjika. Just like tunavyooa Rwanda na Nigeria leo. Kwani kuna Muungano?
 
Tanganyika ipi unayoijua wewe?

(v) The existing laws of Tanganyika and of Zanzibar shall remain in force in their respective territories ....

Unaelewa kuwa mahakama si katika mambo ya Muungano?

Mahakama ya rufaa imefanywa kuwa mahakama ya Muungano lini?

Hiki kifungu kinailinda Tanganyika dhidi ya "ukiini macho" wa Muungano.

Sheria ambazo si za mambo ya Muungano, utaziita ni sheria za wapi? Zanzibar? Mafia? Au Tanganyika?
 
vitu viwili zikiungana kina kuwa kimoja wao walipata wapi muungano wa vitu viwili kungana na kuwa wawili hapo akuna muungano ni urafiki wa watu hao kula na kunywa pamoja
 
Huwa nasikitika pale watu wazima na viongozi wakubwa wanapoongea bila kufikiria sawasawa. Tatizo halijawahi kuwa Serikali ya Tanganyika. Watu hawana shida na serikali ya tatu hapa. Ila watu wanachosema ni kuwa kama Zanzibar ina haki ya kuwa na serikali na Kama Zanzibar ni sehemu ya Muungano huo basi na Tanganyika iwe na serikali yake. Kama Zanzibar ina haki ya kuwa Nchi huru same applies kwa the other party.

Kwa kifupi watu wanataka kusema kuwa na serikali mbili ni uhuni. Hasa pale nchi moja inapokuwa na serikali yake na nchi ya pili haina.

Nadhani wanatakiwa kufikiria upya na kuacha ubabaishaji kwenye hili jambo.

As for me na nionavyo ni ama Tuwe na serikali moja au kama wenzetu watakomalia kubaki na yao basi tuwe na serikali Tatu. Ila Tukiwa na serikali tatu kwa sababu tu kuna watu hawakuona kuwa hawana haki na haja ya kuwa na serikali yao ndani ya muungano, hii nitaitafsiri kuwa ni moyo wa ajabu kabisa wa kupelekea kuongeza matumizi ya fedha chache ambazo tayari hatuna mpaka tunadaiwa. Kwa hiyo tukiwaza kama wenye akili sawasawa ni kwamba Tunamhitaji serikali moja ili muungano uwe sawa. Vinginevyo Tuvunje Muungano ili kila nchi iwe huru na iwe na serikali yake!

Udugu? Kuoleana? Huu ni upuuzi. Hata sasa kuna waliooa Zaire na Umarekani. Mwambieni Mheshimiwa Waziri akitaka kwenda kuoa ama kuoza Zanzibari atakuwa huru kwenda hata kama Muungano umevunjika. Just like tunavyooa Rwanda na Nigeria leo. Kwani kuna Muungano?

Huyu "wapigwe tu" tokea aliposema Zanzibar sio nchi na Wazenj wakamvimbia na kumnunia, anawaogopa kama mtu aliyegongwa na nyoka - hata unyasi ukimgusa anatimka mbio. Haya anayoyasema hayatoki moyoni mwake. Anajua vizuri sana Tanganyika tunayoidai lakini basi afanyeje - ni lazima abwabwaje kama alivyoelekezwa.
 
Tanganyika ipi ambayo tulitumia mabidilioni kusherekea miaka 50 yake
 
Huyu "wapigwe tu" tokea aliposema Zanzibar sio nchi na Wazenj wakamvimbia na kumnunia, anawaogopa kama mtu aliyegongwa na nyoka - hata unyasi ukimgusa anatimka mbio. Haya anayoyasema hayatoki moyoni mwake. Anajua vizuri sana Tanganyika tunayoidai lakini basi afanyeje - ni lazima abwabwaje kama alivyoelekezwa.

Nafikiri huu ni ukweli. I second the motion
 
Kama ccm sio wanafiki wadai serikali moja,hii mbili walishaishindwa,kitu gani kinawaaminisha wataweza tena?ulevi wa madaraka tu,kama hawawezi moja basi watupatie tu Tanganyika pia kama ilivyo serikali ya Zanzibar
 
Back
Top Bottom