Huwa napata tabu sana mtu akisema analogically muungano kuvunjika?
Mkuu ingekuwa vizuri ukaeleza njia na mantiki inayokufanya upate shida kuhusu mawazo na maoni ya baadhi ya watu wanakuja na hoja zinazobainisha kuvunjika kwa Munngano.
Kama wananchi hawataki muungano/kuendeelea kuungana kwa nini "walazimishwe" kwa kuweka protactive structure?
Ni kweli huwezi kulazimisha wananchi katika mazingira ya demokrasia kufanya jambo ambalo wengi hawataki lakini vile vile hakuna research au kura ya maoni iliyopigwa kubainisha maoni ya wananchi kuhusu muungano.
Hatuwezi kusema wananchi wanalazimishwa au hawalazimishwi kutokana na historia na pia structure ya muungano.
Viongozi wetu waanzilishi wa mataifa yetu waliamua nchi ziungane na wakaziunganisha bila kutaka kusikia neno la wananchi wote kwa njia ya kura ya maoni, na kwa maana hiyo, mpaka sasa hatujafahamu mitazamo ya wananchi wengi kuhusu muungano.
Serikali moja ama tatu ingalikuwa ni kipimo sahihi cha kuweza kujua kama muungano huu ni wa hiari ama wa kulazimishana.
Hoja mbadala nadhani ni kura ya maoni ambayo itatoa constitution legitimacy kutoka kwa wananchi kuhusu aina ya muungano wanaoutaka lakini siyo kufanya test ambayo matokeo yake hasara kubwa kitaifa.
Kwa mazingira ya kisiasa tuliyonayo kwa sasa na pia historia ya nchi zetu, nadhani serikali moja ndiyo ingetoa jibu kama kweli tunataka kuungana na siyo kuwa shirikisho kama inavyoonekana kupigiwa chapuo kwa sasa.
Muungano hauwezi kuimarika kama tutaendelea kuishi kwenye pretext ya muungano wakati tunafanya mambo katika misingi ya shirikisho.
Tusiogope muungano kuvunjika kama hivyo ndivyo wananchi walio wengi wanataka iwe.Lakini suala la serikali moja kwa sasa sio mojawapo ya options kwa sababu serikali ya Zanzibar ni lazima iwepo(kwa mujibu wa ToR).
Ninadhani watu hawaogopi muungano kuvunjika bali wanahofu na gharama za muungano kuvunjika katika mazingira fulani.
Kama watu wa nchi mbili watakaa na kuamua kuvunja muungano kwa amani, basi nadhani hili wala halina uwoga lakini hofu inakuja kama kuna kundi au nchi moja itataka muungano kuvunjika kwa kutumia nguvu nje ya amani ambapo nguvu hiyo inapelekea kuwepo kwa gharama kubwa kisiasa, kiuchumi na kijamii.