Magufuli amedai kuna mtu mmoja anapiga sana kelele wamenasa mawasiliano yake alikuwa anatuma meseji kwa Mwanyika, Je wamedukua mawasiliano yake? hii imekaaje kisheria wakuu? mtu anaweza kupitia text zako na kuzitamka hadharani bila kosa lolote?
Mbona hili linajulikana sana! Ndio sababu ukitaka kumaliza mambo yako sometimes inatakiwa ufanye physical contacts na mhusika muongee uso kwa uso. Haya ya kutumia simu kwa ishu nyeti kwa watu maarufu sio kabisaAnasema siri bila yy kujijua.sasa kashajulisha watu kua kuna watu hua wanawadukua.
Magufuli amedai kuna mtu mmoja anapiga sana kelele wamenasa mawasiliano yake alikuwa anatuma meseji kwa Mwanyika, Je wamedukua mawasiliano yake? hii imekaaje kisheria wakuu? mtu anaweza kupitia text zako na kuzitamka hadharani bila kosa lolote?
kwani mlikuwa hamjui.....kalaghabaooooooAnasema siri bila yy kujijua.sasa kashajulisha watu kua kuna watu hua wanawadukua.
Umeongea kitu cha msingi sanaSioni tatizo kwenye hili la ufuatiliaji wa mawasiliano ya baadhi ya watu kwenye vita hii iliyopewa jina la "vita ya kiuchumi".Mh.Rais anapaswa kuungwa mkono,lakini asijaribu kuuhadaa umma kwa kuwahusisha watu wasiohusika kwa namna yoyote ile na haya tunayoyapitia kama Taifa.
Nilimsikia akihoji kwa Uchungu kuwa " nani aliyeturoga?"Bila kupepesa macho,mchawi wetu siyo Tundu Lissu,Mruma wala Kafumu,Mchawi wetu ni ccm na serikali yake.Hawa ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.Mikataba hii mikubwa inayolitafuna Taifa,ilisainiwa kipindi cha Mkapa na Kikwete.Hawa ndiyo waliobeba "tunguli za kuliloga Taifa letu kiuchumi"
Chini ya uongozi wa mkapa na kikwete,nchi yetu iliuzwa kwa kila aliyekuja kwa jina la uwekezaji.Wakati wanaoitwa wapinzani walipokuwa wanapigia kelele hiki kinachomliza Rais wetu leo,waliishia kubezwa na wengine walifukuzwa bungeni kwa mbwembwe na vifijo vya wabunge wa ccm wakiongozwa na spika wao.
Kama serikali ingeungana na mh.Zitto na Chadema kipindi kile walipokuwa wanaupinga mkataba wa Buzwagi/ACACIA uliosainiwa na Karamagi Hotelini London,yawezekana kilio hiki cha kuibiwa utajili wetu kisingekuwa hivi hivi leo,lakini wa upeo mdogo wa wabunge wa ccm akiwemo na mh.anayelia na kuomboleza leo,walimtimua Zitto na kubariki mkataba wa kinyonyaji uliosainiwa Hotelini.
Majuto ni mjukuu,suluhisho la haya yote ni kutengua kinga zinazowalinda watangulizi wake na awaburuze mahakamani wakashtakiwe kwa uhujumu uchumi,hao ndiyo waliotufikisha hapa,kusikitika na kulia huku ukikwepa kiini cha matatizo haya ni unafiki wa kiwango cha lami.
Makengeza alishawahi kuwa mwanaharakati wa mazingira na alishawahi kuyapinga makampuni ya madini huko nyuma?Wengi mnadhani huyo mtu ni Lissu ila mimi naweza kuwa na hisia kuwa huyo si Lissu bali ni joka la makengeza na wengi hapa hamtanielewa ila ndio hivyo..huyo ndio aliyekua na uwezo wa kwenda kuchange baadhi ya vitu maana anajua wapi walipokanyaga na huyo bwana aliongea sana kama mlikua mnamfuatilia
Tafuta mtandao wako uwe salama na faragha zakoLeo wakati rais Magufuli anapokea ripoti ya makanikia amesema kwamba walifuatilia mawasiliano ya mtu ambaye alikuwa anawasiliana na mtu anayeitwa Mwanyika na kumuomba data, hii maanake ni kwamba serikali kwa kushirikiana na kampuni za simu zinaingilia mawasiliano ya watu.
Kwa lugha nyingine ni kwamba mitandao ya simu inatoa siri za wateja wake kwa serikali aidha kwa hiari yao au kwa kulazimishwa, je uhuru wa faragha ya mteja upo wapi? Na kwanini mitandao hii inakubali kutoa siri za wateja wao kwa watu wasio husika, kuna haja ya kuendelea kuwa wateja wa mitandao hii inayotoa siri za wateja wao?.
Niko pamoja naweWengi mnadhani huyo mtu ni Lissu ila mimi naweza kuwa na hisia kuwa huyo si Lissu bali ni joka la makengeza na wengi hapa hamtanielewa ila ndio hivyo..huyo ndio aliyekua na uwezo wa kwenda kuchange baadhi ya vitu maana anajua wapi walipokanyaga na huyo bwana aliongea sana kama mlikua mnamfuatilia
Muda tu ikifika utaelewa raisi ameongea mengi na amechanganya, na kuna sehemu ipo alipomsema lissu ila wala hakuna aja ya kukomalia kitu kisicho na tija wait muda ufike utajua vizuriMakengeza alishawahi kuwa mwanaharakati wa mazingira na alishawahi kuyapinga makampuni ya madini huko nyuma?
Uaijidanganye hata mim ukiniletea za kuleta nakudukua vizuri ndio faida ya kusoma it zaidi sio lazma niende kwenye campuni za simumkuu, kwenye mfumo wa kiimla lolote lawezekana.
dawa yake ni UKUTA tu!