Mitandao ya simu kutoa siri za wateja, uhuru wa faragha upo wapi?

kwa kukufahamisha tu coz inawezekana hufahamu...MAWASILIANO YOTE YANAYOFANYIKA NCHINI YANAPITIA TCRA. Kwahyo tukitaka mawasiliano yako siyo lazima watu waende tigo au vodacom au sijui madudu gani..TCRA inatosha.
 
Kama walikuwa wakifanya wakijua ni siri kwa hili suala la kitaifa bac wamejamba na kama na ww unashirikiana nao kuiangamiza nchi kwa maslahi yenu binafsi, basi kwa hili mtajambaaa nawe jiandae
 
serikali ni big brother.
1c35bf52e013040a0b7567618be9ebb4.jpg
 
Leo wakati rais Magufuli anapokea ripoti ya makanikia amesema kwamba walifuatilia mawasiliano ya mtu ambaye alikuwa anawasiliana na mtu anayeitwa Mwanyika na kumuomba data, hii maanake ni kwamba serikali kwa kushirikiana na kampuni za simu zinaingilia mawasiliano ya watu.

Kwa lugha nyingine ni kwamba mitandao ya simu inatoa siri za wateja wake kwa serikali aidha kwa hiari yao au kwa kulazimishwa, je uhuru wa faragha ya mteja upo wapi? Na kwanini mitandao hii inakubali kutoa siri za wateja wao kwa watu wasio husika, kuna haja ya kuendelea kuwa wateja wa mitandao hii inayotoa siri za wateja wao?.
Hakuna haja Mzee baba
 
Hajataja jina la mtu
Hajamtaja Lissu
Na inaonesha ni uongo maana kama ni kweli wangeweka hadharani mbona kina Kafumu wametajwa kabisa
By the way, kutafuta data ni makosa?
Mi ningeshtuka kama angekuwa anasaidiana na hao akina Mwanyika "kupika data" za kuwaibia watanzania. Lakini kama ni kuomba data zilizopo, sioni kama ni issue. Mbona hata hizo kamati alizounda zilikuwa zinatafuta data huko huko kwa akina Mwanyika?
 
Haya matatizo yakudukuliwa niyakujitakia siku hizi .

Hivi mshawahi sikia tigo au voda wakisema mawasiliano yenu yapo secured ( encrypted)?

Inshort kutumia mitandao yakawaida kudukuliwa inaezekana.

Only and only way yakuwa angalau secured ni through instant messaging Apps kama Telegram, Signal na kidogo WhatsApp bali njia nyingine wanadukua tu.


Telegram alitoa challenge kabisa atakae dukua anapata pesa ndefu tu ila hakuna alieweza 100%

So unacho ona siri tumia means ambazo zinakulinda na Siri yako.

Sidhani if Government wanaweza dukua (decrypt) kitu ka telegram

Nawasilisha just maoni tu.
 
Serikali ya Tanzania ina tap simu sana.

Mkapa alimtap rafikibyake mmoja kwa mwaka mzima. Jamaa akajua serikali inam tap.

Baada ya mwaka akaitwa Ikulu. Jamaa akajua anaenda kuchinjiwa baharini. Mkapa akamwambia nataka kukupa shavu usimamie kuuza mashirika yote ya umma. Akawa anamkumbushia stories za Pugu waliposoma pamoja.

Tanzania si serikali tu. Hata mtu binafsi kuna kipindi ulikuwa unaweza kuongea na mainjinia wa kampuni za simu wanakupa mawasiliano ya siri.

Kuna kipindi mpaka benki zilikuwa zinatoa siri za wateja.

Kwa hiyo siwezi kushangaa Magufuli akim tap Lissu.

Ingawa vikevuke kama Lissu anamtumia maombi Mwanyika, ni rahisi sana Magufuli kupata habari kutoka kwa Mwanyika bila hata kuhitaji an actual tap, inawezekana Magufuli akawa anasema tap kwa maana ya tap ya kupata habari kutoka kwa Mwanyika.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna kipindi Lisu alikamatwa akasema Simu zake bado zipo central nadhani kipindi hiki ndipo zilipoangaliwa anawasiliana na nani na kama haku delete mawasiliano ya maandishi walisoma
 
sasa wasipodukua mawasiliano..itakuwa nini maana ya serikali?Serikali ikiamua kukufuatilia inaweza kuanzia taarifa zako zote zamawasiliano hadi miamala yote ya pesa hadi wake na michepuko yote ulonayo
Hahaha kweli kabisa mkuu serikali ni kila kitu. Hivi kama mtu unataka kuatarisha maisha ya wananchi usidukuliwe ye ni nani?
 
kwani RAIS alimtaja TINDU LISSU?

Si kila kitu lazima kutaja jina. Kamsema mtu alikuwa mwanasheria wa mazingira sasa hivi anaropoka.

Ni wazi huyu ni Tundu Lissu.

Lakini, zaidi ya hilo.

Hata akiwa si Tundu Lissu, hoja ya msingi haibadiliki.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Back
Top Bottom