Mr.Junior
JF-Expert Member
- Sep 8, 2013
- 11,774
- 9,959
Alichokosea ni kusema vile mbele za watu.Leo wakati rais Magufuli anapokea ripoti ya makanikia amesema kwamba walifuatilia mawasiliano ya mtu ambaye alikuwa anawasiliana na mtu anayeitwa Mwanyika na kumuomba data, hii maanake ni kwamba serikali kwa kushirikiana na kampuni za simu zinaingilia mawasiliano ya watu.
Kwa lugha nyingine ni kwamba mitandao ya simu inatoa siri za wateja wake kwa serikali aidha kwa hiari yao au kwa kulazimishwa, je uhuru wa faragha ya mteja upo wapi? Na kwanini mitandao hii inakubali kutoa siri za wateja wao kwa watu wasio husika, kuna haja ya kuendelea kuwa wateja wa mitandao hii inayotoa siri za wateja wao?.