Taja mtaa korofi na hatari kiusalama katika mkoa wako kuwasaidia wageni pindi wafikapo mkoani kwako.
Iringa ni Kitanzini na Isoka
Vipi hapo majengo wale wapiga nondo wamesha staafu? Na wale wakuvizia madolali pale custom je?Hahaaa habari ya hapa tulipo mkuu, Tunduma kila mtu ni mjanja dhidi ya mwenzie!
Sultan Area sio kiivyo, Vibandani siku hizi pamekuwa na unafuu kidogo ingawa zamani palikuwa hakupitiki usiku. Hiyo barabara ya kwenda Moro hotel nilishawahi kukabwa maeneo ya uwanja wa gofu walikuwa kama saba hivi, wale vibaka karibu wote nilikuwa najuana nao ila wao hawakunitambua usiku huo nikiwa natoka mazoezini, walichukua wallet iliyokuwa na IDs, kesho yake waliniletea wenyewe vitu vyangu bila hata kuwatafuta. Huwa nawalinda sana na hizi mia mbili mia mbili wakiwa na njaa zao, ndio maana sikupata tabu ya kupata vitu vyangu.
mwanza mitaa korofi na hatari kiusalama ni mabatini na shede
Huko ndo kubaya sana siku hizi. Si unajua diplomats wengi wanaishi huko? Baso vibaka wanavizia wanapokua wanatembea kwa miguu ile jioni, wao vibaka wanakuwa na bodaboda ama magarisiku hizi hadi masaki/obay watu wanaporwa
tabora mwanza road hasa ukivuka reli jirani na kiwanda cha nyuzi hatari sana