Misimamo ya Ndani ya Vyama vya Siasa: Changamoto kwa Demokrasia, Uwajibikaji na Haki za Binadamu nchini Tanzania

DolphinT

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
2,366
Reaction score
3,457
Katika mfumo wa utawala wa kidemokrasia mathalani nchini Tanzania, vyama vya siasa vina nafasi ya kipekee katika kuongoza mchakato wa kisiasa na kutoa dira ya maendeleo kwa taifa. Hata hivyo, hali ya sasa ni ya hatari Kwa sababu misimamo ya ndani ya vyama hususani chama Cha mapinduzi, maarufu kama party caucus, imegeuzwa kuwa jukwaa la kulinda mamlaka ya kisiasa ya kikundi Cha watu wachache kwa gharama ya misingi ya demokrasia, utawala wa sheria, na haki za binadamu. Misimamo hii imefanikiwa kuchochea matumizi mabaya ya vyombo vya dola, kuua uhuru wa mihimili huru ya dola, na kuathiri imani ya wananchi kwa taasisi za serikali kama TAKUKURU na vyombo vya habari. Hali hii imekuwa dhahiri katika miaka ya karibuni hapa nchini Tanzania, ambapo chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinalaumiwa kutumia caucus zake kulazimisha maamuzi yenye mwelekeo wa kisiasa, kulinda madaraka isivyo halali na sio maslahi ya Taifa Kwa upana wake.

Mfano wa karibuni unabainishwa na matumizi ya misimamo ya chama dhidi ya haki za kisiasa ni kesi ya uhaini iliyofunguliwa mwaka huu dhidi ya Mheshimiwa Tundu Lissu, Mwenyekiti wa CHADEMA. Lissu alishtakiwa baada ya kutoa kauli za kuikosoa mifumo ya uchaguzi nchini, akiitaka serikali ianzishe mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki maarufu kama No reform no elections na uasi dhidi ya mifumo kandamizi isyotoa Haki na usawa wa Kidemokrasia katika taifa hili.

Hoja yake kwamba vyombo vya uchaguzi vimekuwa vikikiuka misingi ya haki kwa kupendelea chama tawala haijajibiwa kwa hoja, bali kwa njia ya mabavu na hila ya kisiasa, hatua ambayo wachambuzi wa siasa na wapenda Haki wa kidemokrasia wanaona kama “mfumo wa kutumia sheria kandamizi za kikoloni kuua demokrasia na kuondoa uwajibikaji wa waliyopewa dhamana Kwa mujibu wa katiba yetu. Mwanafalsafa wa siasa, Alexis de Tocqueville, aliwahi kusema kuwa "The health of a democratic society may be measured by the quality of functions it permits its opposition to fulfill." Tanzania inapopunguza nafasi ya upinzani kwa kutumia sheria za kikoloni na kandamizi , inajiondoa kwenye msingi wa demokrasia ya kweli na utawala Bora.

Si mahakama tu ambazo zimetajwa kuathiriwa na msimamo wa kisiasa wa chama tawala. Kumekuwa na ongezeko la hisia na ukweli usiacha shaka kuwa uteuzi wa baadhi ya majaji unafanyika kwa msingi wa utii wa kisiasa na matazamio ya ahadi za teuzi na vyeo siku za usoni na , si uwezo wa kisheria. Mfano wa Jaji Mustapher Mwanga, ambaye kwa sasa anasikiliza kesi muhimu dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA, umeibua maswali ya kimaadili na kiutendaji. Jaji huyo aliwahi kuwa sehemu ya timu ya uchaguzi ya Zanzibar, ambako uchaguzi wa mwaka 2020 ulikumbwa na tuhuma nzito za ukiukwaji wa haki. Uteuzi wa majaji waliowahi kushiriki shughuli za kisiasa kisha kuwapa kesi zinazohusu vyama vya siasa ni kinyume na misingi ya uwiano wa madaraka.

Montesquieu, mmoja wa waasisi wa nadharia ya mgawanyo wa madaraka, alisisitiza kwamba "There is no liberty if the judiciary power is not separated from the legislative and the executive." Tafsiri ya haya ni kuwa, bila mahakama huru, uhuru wa wananchi upo mashakani.

Aidha, Jeshi la Polisi limegeuzwa kuwa chombo cha propaganda ya kisiasa za chama tawala hasa Kamanda Muliro, badala ya taasisi ya ulinzi wa wananchi. Wakuu wa Jeshi hilo wamekuwa wakitoa kauli zinazotetea msimamo wa chama tawala, huku wakikandamiza haki za kisheria za v ya vyama vya upinzani hasa CHADEMA na asasi za kiraia.

Mifano unaoibua mashaka ni uteuzi wa IGP Simon Sirro kuwa Balozi kabla ya kustaafu, pamoja na Ernest Mangu aliyeteuliwa kuwa balozi nchini Rwanda baada ya kutumikia kama Mkuu wa Jeshi la Polisi. Teuzi hizi zinajenga dhana ya "malipo ya kisiasa" kwa viongozi wa vyombo vya usalama waliotumikia kwa utii wa chama badala ya taifa.

Katika hali ya kidemokrasia, vyombo vya usalama vinapaswa kuwa huru na vya kitaalamu na wakuu wake kutoteuliwa katika nafasi za Utumishi wa umma mara baada au wakati wa Utumishi wao Ili kueupuka upendeleo.

Profesa Mahmood Mamdani aliwahi kusema: "A politicized police force is the first sign of the death of civil society." Kwa muktadha wa Tanzania, matamko ya polisi dhidi ya shughuli za vyama pinzani, na kukataa kuwepo kwa utekaji au mauaji ya kisiasa, yanaashiria hali hiyo ya hatari na kudidimia Kwa utawala Bora na Demokrasia pamoja na utawala wa Sheria katika nchi ikiyostaarabika

Mbali na hayo, Bunge la Tanzania limepoteza sifa yake kama chombo cha uwakilishi na ufuatiliaji wa matumizi ya serikali pamoja na kusimamia serikali.

Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma na matumizi yasiyoelezeka hazijawahi kujadiliwa kwa kina bungeni na hatua stahiki kuchukuliwa Kwa wahusika.
Viongozi wanaotajwa katika ripoti hizo wameendelea kubaki madarakani bila kuwajibishwa wakiwemo mawaziri na watendaji wengine.

Pia, hoja nyeti kama ongezeko la deni la taifa zimekuwa zikipuuzwa au kuzimwa kwa msimamo wa chama tawala Kwa dhamira kubwa ya kulinda madaraka dhidi ya maslahi ya wananchi.

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina, alipotoa hoja ya uwajibikaji na kuuliza maswali ya msingi kuhusu matumizi ya fedha za umma ongezeko la deni la taifa na waziri Mwigulu kushindwa kutoa majibu juu ya mifumo na taratibu za ukopaji, alisimamishwa na hatimaye kufukuzwa bungeni, akituhumiwa kwa “kukosa nidhamu ya chama.” na hivi karibuni Mwenyekiti wa Chama na Rais kumbafaza hadharani.

Vilevile, Mchungaji Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe, alipohoji kwa uwazi juu ya utekaji na mauaji ya raia, alitishiwa hatua kali zisizo za kisheria, ikiwa ni pamoja na kufunguwa kanisa lake kuhudhuria vikao vya Bunge bila kuzingatia taratibu za haki ya kusikilizwa na kujua kwamba yeye ni mwakilishi wa wananchi na maswali yake ni maswali ya wananchi.

Kwa ujumla, hali hii imezaa mfumo wa siasa wa woga, ukimya, na udhibiti wa taasisi, ambapo kila anayesema ukweli au kutoa hoja mbadala dhidi ya misimamo ya chama anachukuliwa kama msaliti au mpinzani wa maendeleo. Katika mazingira kama haya, demokrasia huwa haina maana, kwani kama alivyosema Noam Chomsky, "If we don’t believe in freedom of expression for people we despise, we don’t believe in it at all." Uhuru wa kujieleza, kutoa hoja mbadala, na kusimamia mamlaka ni nguzo ya kila taifa lenye maendeleo ya kweli.
 
"The health of a democratic society may be measured by the quality of functions it permits its opposition to fulfill.".
 
Shida iko katika mfumo wa demokrasia,nchi nyingi hususani afrika kunamfumo wa demokrasia wakilishi,hapa ndo tatizo lilipo!lengo kuu la katiba ni usitawi wa watu.kama tunania ya kweli itungwe shelia ya kuwawajibisha wabunge ambao wakichaguliwa kuwawakilisha watuwao wakifika bungeni wanageuka kuwa machawa wa watawala.
 
Shida iko katika mfumo wa demokrasia,nchi nyingi hususani afrika kunamfumo wa demokrasia wakilishi,hapa ndo tatizo lilipo!lengo kuu la katiba ni usitawi wa watu.kama tunania ya kweli itungwe shelia ya kuwawajibisha wabunge ambao wakichaguliwa kuwawakilisha watuwao wakifika bungeni wanageuka kuwa machawa wa watawala
 
Back
Top Bottom