Mishahara ya watumishi serikalini mwezi huu kunani?

Mishahara ya watumishi serikalini mwezi huu kunani?

Leo haipiti mkuu.. Usijali we jipange tu. Ndio tunamalizia hapa..
 
daah...hii nchi majanga....mshahara wenyewe ukitoka hautoshi...yaan
 
eti mshahara umechelewa siku sijui 1 mtu anakuja jukwaani kuanzisha uzi? huyu akistaafu itakuaje sasa? au teknolojia inavyo kua kwa kasi wakapunguzwa kazi na kuwa replaced na mashine? hawana ubunifu wowote wamekaa ofisini kama mizoga tu ndio maana taasisi nyingi za serikali hazina kabisa ufanisi
Akistaafu si analipwa penseni yake na other benefits
 
Natabiri ukitoka watu watapangana kwenye ATM za NMB kama foleni za kununua sukari ama kwa babu loliondo.
 
Mimi nashukuru mshahara kuchelewa,kesho wilayani kwangu kuna mwenge na tumeawbiwa kila mtumishi lazima achangie sh 3000/=na kununua tracksuit sh 30,000/= na nilazima kwenda kukesha kwenye mwenge kwani utjakuwa kijiji jirani
Sasa hiyo elfu tatu na kununua tracksuit ambayo ni Mali yako mwenyewe ugumu huko wapi.wakati hiyo elfu thelathini hata kuonga haitoshi
 
Hizi jitihada za serikali hii ya awamu ya 5 kila zikitekelezwa ni wa chini ndio wanaumia. Walianza na sukari, wakaumia hadi wa kule Buturi kwetu kwa bei ya sukari kupanda mara 2 na 3. Likaja zoezi la watumishi hewa, sasa wanaoumia ni watoto wetu kwa wazazi kukosa hela ya matumizi kwa wakati. Naona serikali haijawa na kalenda ifanye nini hapa na isifanye nini pale. Wahusika nao ni bubu hadi rais anaposema ndiyo utwawasikia wakitekeleza bila kutafakari. Muda mwingine kama namkumbuka JK vile1!!
 
Msisingizie kuchelewa kwa mishahara nyie, tunajua imetoka njooni mlipe madeni hapa dukani
 
Back
Top Bottom