Chanzo ni Gazeti la Tanzania Daima,
Mtoto wa kikwete aitetea chadema
Asema ni chama cha watanzania kwa ajili ya watanzania.
Mtoto wa rais jk,Miraji jakaya kikwete,amekitetea chama cha CHADEMA akipinga chama hicho kuhusishwa na vurugu mbalimbali zinazotokea nchini,zikiwemo zile za wamachinga zilizotokea jijini mbeya hivi karibuni.
Mtoto huyo wa Rais alionyeshwa kukerwa na watu wenye mtazamo wa kukisingizia chama hicho kikuu cha upinzani kwa kuhusishwa na vurugu wakati hali halisi inaonyesha wazi kuwa wananchi wenyewe awalizishwi na hali ya mambo ilivyo na hivyo kuamua kuwa mstari wa mbele kupigania haki zao.
Miraji aliweka wazi msimamo wake huo kupitia mtandao wa facebook akichangia mjadala mzito uliohoji kwanini chadema kinazingiziwa kuanzisha vurugu.