Huyo wa la saba akikutana na mashangingi ya jiji utalia. Waendesha bodaboda wafyatua tofali wauza bucha wrote wake. Angalia tu mwanamke msomi anayejitambua.
Yupo single kuna kipindi alikuwa anatafuta, we ongea kiutu uzima tu yawezekana akawa bado hajapata!kwani yupo singo? ila naogopa nae atangonoka na bosi wake afisa elimu taaluma wa jiji.... maana huko maofisini ni sheeedaahhh. tuoe wapi sasa? ila huyo wangu wa class seven ni swala tano.
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.
Nawasilisha.
Oa tu mbaba. Kwa kuwa wataka kuboresha, nataka nikujulishe kwamba huyo wa sasa kwako ni poa b'coz machachari ya uyo educated umeyeona. Wada educated wanapoanza kuchomoza ktk kipato, wanang'ara, afu wanataka kung'ara zaidi...sio vibaya, mbaya kulegeza kwa bawabu beberu ambapo wana amini ni njia ya kutokea. Hakushirikish mume coz ushiriki wako utamzui asilegeze na yy shida yake ni kupa anachotaka tu...ndo tabu inapokuja...kichocheo Sura yake na shape.
Cku zote ni rrraaahisi sana kumuongoza mjinga kuliko mwerevu....na ndio maana hata ktk nchi yetu werevu ni wapiga kelele tu na wajinga ndo wanaongoza nchi...matokeo ndo hayo hwataki kustaafu, na kila mpango hautekelezeki.
UKIMUOA huyo aliye chini kielemu...mpige msasa wa english coz tu...mambo shwari. Muongoze, mpe maelekezo/ makatazo atatii bila hiyana. Atakuwa mnyenyekevu daima na milele. KUWA NA WEW NDO ATAWARINGIA WADADA wenzake ambao wamesoma but hawaolewi. Kuolewa HESHIMA.
yaani kilaa eneo ni matatizo, rafiki yangu swala kubwa ni kumuomba mungu tu akupe mke mwema....huyo wa chuo kikuu hatatembea na bosi wake?
Hakuna uhusiano kati ya elimu na mapenzi. Wewe Oa tu hakuna shida. muhimu ni tabia na matendo yenu je vinaendana. Ni kuepuka dharau, kejeli, magigambo/majivuno au kusemama kwa kuingiza kigezo cha utofauti wa elimu. Unaweza kuwa na elimu kubwa lakini mapenzi hujui, unaweza kuwa na eimu ndogo lakini mapenzi unajua, kwa hiyo mnatagemeana.
Hujui unachokinena. Tuulize tuliowahi kujidanganya kama wewe, tutakupa uzoefu. Kama unaongelea mapenzi ya boyfriend na girlfriend basi uko sawa. Lakini kama una maanisha maisha ya commitment kama mume na mke wanaoanzisha familia kuna mahusiano makubwa kati ya elimu (upeo wa kuelewa na kuchambua mambo) na mapenzi. Ukibisha basi jaribu japo ni sawa na kuthibitisha ukali wa sumu kwa kuionja!!
unaweza kuwa na master na bado wa la saba akakuzid akili.elimu na akili ni vitu viwili tofauti.