Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Mimi nina masters nataka kuoa Darasa la saba

Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.

Mkuu una master ya tandale?
 
Kuna kosa umelifanya ila ukijerekebisha mtaishi vizuri. Katika ndoa ili muishi vizuri suala la elimu weka pembeni, ukifika nyumbani mastaz yako iache mlangoni. Ukitoa mifano toa ya kawaida, usianze unajua kuna PHILOSOFA mmoja au kuna PROFESA mmoja hapo ndoa itakuwa ndoana. Pangeni mambo yenu kwa kushirishana, cha msingi mfanye ajiamini kuwa wewe ni wake. Hata akikosea mrekebishe usihusishe kukosea kwake na elimu yake
 
Hahahaaaaaa, we Viol hufai kabisa! kumtetea kote huko shy land kwa upuuzi wake leo unajifanya ulikuwa umelewa? Acha hizo mkuu!
But, nimefurahi sana kwa kuwa na birthday kesho, kwani nina kijana wangu naye pia ni birthday yake kesho! Mwenyezi Mungu awabariki sana muwe na afya njema pamoja na mafanikio maishani mwenu!
HAPPY BIRTHDAY TO YOU GUYS!!!!

Thanks much mkuu,duh tar zimegongana 11/01

Mkuu kweli Jana nililewa nikaona jamaa anashambuliwa na wengi
 
Last edited by a moderator:
Uelewa wake ni bora kuliko elimu yake ya vyeti!!
There's a difference btn being educated and schooled !!
Smart mind do not need the approval of the so called FORMAL EDUCATION to justify its Capability of understanding & handling lyf challenges and alike!!!

Think of this Sir....
Just my Thoughts not Opinions!!!!
 
Hakuna mwenye uwezo kuoa darasa la saba kwani hayo madarasa yapo mengi. Oa mtu mke siyo majengo. Mke wa kukufaa ni yule ambaye roho yako imempenda naye akakupenda, mtu mwingine kati yenu ni doa kwa ndoa
 
Certificate,diploma,degree,masters,PhD hazitunzi mke wala mume oa unayempenda hizo ilimu zenu hazinaga inshu kwenye mapenzi
 
Ndoa nyingi za siku hizi zinaanzia kwenye uchumba, ndani ya uchumba una muda wa kuchunguza/kufahamu endapo utofauti wenu wa elimu utakuja kuleta madhara. Kudanganywa/kudanganya ni maamuzi ya nafsi yako tu. Ha siku moja kwenye mapenzi yawe ya uchumba au ndoa ukaona tatizo lakina ukasema haina tatizo.

Mkuu ukubali hujui haya mambo. Ndoa zinazoanza na uchumba zilikuwa zamani. Ndoa za siku hizi zinaanza na Uhawara. Vijana wanaanza kulalana kila mmoja akiishi kwa wazazi wake. Huu ni Uhawara, si uchumba. Na katika mazingira ya aina hii, niamini, huwezi kuujua uhalisia wa tabia za mwenzako kwa sababu kila mmoja huficha makucha yake ili mwenzie asimshtukie. Ukija kuoa/ kuolewa naye ndo makucha yanakunjuliwa na tabia zinajionesha kwa rangi zake halisi.
 
Hata hiyo unayoiita zamani uhawara ulikuwepo. Tabia ya mtu haifichiki hata siku moja. Hata uzifiche vipi hizo tabia zako, lakini mwenye nia ya kuzijua atazigundua tu. Tabia ni kama ngozi, utajua tu. Wengi wanagudua tabia za wenza wao kabla ya ndoa ila kwa kuwa washasugua sana lami kutafuta wanaimani litavumilika. TUnasema mbele kwa mbele.
 
Mavi yako yaani aliyekuambia kuoa kunaendana na ma degree nani.?watu tuna mashahada ya uzamivu tumeoa ma house girl ndoa miaka mia chereko tupu
 
Jamani wanajamvi naombeni Mawazo yenu. Kuhusiana na kichwa cha habari hapo juu, mie ni Muislam, nilioa Mwalimu wa Primary nikaachana nae baada ya kubaini anafanya Ngono na afisa Taaluma wa Jiji.
Nimepata binti aliyeishia Darasa la saba. Nipeni uzoefu haya Maisha yatakuaje kwa gepu hilo kubwa la elimu.

Nawasilisha.

Mim sioni ttz tena hawa ambao hawaja soma ndi wazuri sana maana hawezi kukusumbua labda upate yule ambaye kichwa yake inaendenda resi utafikiri kidonda kilichowekwa pilipili, pia kama ana mapenzi ya kweli na wew usikubali kumuacha hata kidog siku hizi hatuangali una elimu gana ila Nyota yake na yako zinaendana kwenye swala la mapenzi,,, ja je moyo wangu ukoje kwake
 
tabia ya mtu ya ndani iko palepale usidhani msomi mwenye nidhamu shule itambadilisha vilevile ukioa mke kwakuwa ni la saba 'E' basi atakuheshimu tena akishazoea ndo makucha yatachanua chanu.
wewe kama unaanza fikra potofu kwakuwa yule ana kazi ndio maana hata huyo hamtaishi. wewe angalia mke mwema sio MEMKWA au PHD
 
Mavi yako yaani aliyekuambia kuoa kunaendana na ma degree nani.?watu tuna mashahada ya uzamivu tumeoa ma house girl ndoa miaka mia chereko tupu

We mvulana kigori unaingiaje kwenye mijadala ya watu wazima! Watu wako serious we unaleta mizaha hapa!! Hamjafungua shule tu??
 
Ndoa ni ubia. Jitahidi mbia wako ajazilizie kule ambako wewe umepungukiwa. Ikiwa utakua na mbia wa kuongozwa tu, hutopata raha ya huo ubia.

Ikiwa huyo mtarajiwa wako anavyo unavyodhani vitakufaa na hadi sasa hamjapishana kauli/mawazo kutokana na tofauti ya elimu, basi anakufaa. Kama umeshaona dalili za kutofautiana na hata kuishi kama mtu na bosi wake, kimbia haraka sana.
 
Back
Top Bottom