Mkuu, Uzi wako umenipa nguvu ya kuoa form 4 wangu maskini, maana nilikuwa najiuliza sana juu ya chaguo langu."hivi ni kweli ndo naenda kuoa huyu mwanamke, mbona kama hatufanani?" nikimaanisha kielimu..! mie nna kadigrii kangu yeye form 4 leaver...hata kazi hana ukiondoa kumsaidia mama ake kuuza duka la vipodozi....na kinachoniumiza kichwa zaidi kuona rafiki zangu wengi wa karibu wameoa wake ambao ni wasomi wenzao..wengine tayr hao wake zao wakiwa na kazi zao na wengine bado wanapambana kutafuta ajira...but wana degree zao mkononi.
Nikimfikiria huyu wangu wakati mwengine nachoka kabisa..maana mawazo wakati mwngine yanafika mbali kbs,najiuliza kwa mfano akikutana na wake wa marafiki zangu hatojisikia vibaya? kuona wenzake wana elimu ya kutosha hlf yeye ndo hivo tena...najiuliza hata stori zao zitaendana kweli?
Ila nimeamua kuoa tu maana nishamtia tamaa sana na sio yeye tu hadi mama yake na baadhi ya ndugu zake wa karibu..nikimuacha kwa kigezo cha elimu nahisi si sababu madhubuti na Mungu anaweza hata kunipa mtihani katika maisha yangu ya ndoa kwa hao wengine.coz huyu mtoto hana shida she is cool, heshima,mapenzi na hana tamaa...sio omba omba wa hela,mpk wakati.mwengine najisikiaga aibu naamua kumgaia hata kama hajaomba...na tena anashukuru hata ukimpa buku 5 anaona nyingi...cjui huko mbele itakuaje naomba Mungu asibadilishe tabia na fikra zake.
Sent using
Jamii Forums mobile app