Mimi ni mvivu kweli, naombeni ushauri

Wadau nina shida moja katika maisha yangu. Mimi ni mvivu halafu huwa natake easy kila kitu, kitu ambacho kinanisababishia hasara nyingi maishani.

Kuhusu darasani nina akili za kutosha toka primary top ten ilikuwa hainikosi hata chuo sikuwahi kupata supp, hata kuna wakati somo moja lililamba robo tatu ya darasa, tena nilikuwa nimelazwa, nikatoka hospitali asubuhi nikaingia saa tisa kwenye paper nikapata zangu B. Niliosoma nao humu wanaweza kunikumbuka.

Sasa tatizo linakuja kwenye maisha, mimi ni mvivu. Kuamka nitashtuka tu saa kumi na moja najiongeza kidogo kidogo hadi inafika saa moja najiandaa kivivuvivu hivo hivo. Mara nivae nguo hii mara nione sijapendeza nivue hadi saa mbili natoka nduki kwenda job maana sio mbali, kwahiyo hapo naacha chumba kikiwa rafu maana muda wa kupanga na kutandika kitanda unakuwa hamna hadi nirudi jioni.

Nikialikwa kwenye party najiandaa kivivu hadi wakati mwingine naacha tu maana muda unakuwa hamna tena sherehe imeisha.

Nikienda benk sihesabu hela, jana nimeibiwa elf 10 duka la kubadilishia fedha maana sikuhesabu, kwenye daladala nilipewa hela feki hivi hivi maana hata sikuangalia.

Naombeni ushauri nifanyeje maana mimi mtu mzima nahitaji kuwa na familia na kuwa mama bora. Ndio maana nilitamani kuadopt mtoto ili niwe busy nae, haya maisha ya kuishi peke yangu yananilemaza jamani nifanyeje?

Natamani kuwa active. Hapa nimeandika hivi nimechoka kweli yaani.
Una jinsia gani?
 
Back
Top Bottom