Nimejaribu kuanzisha biashara mbalimbali lakini huwa hazidumu. Naombeni ushauri

Alicia leon

Member
Apr 19, 2021
52
113
Habari Wana JamiiForums,

Nimekuja hapa nikiomba mawazo yenu, ushauri na msaada ikiwezekana. Katika maisha yangu nimejaribu sana kutafuta kazi sehemu mbali mbali bila mafanikio, na hata nikipata haidumu kabisa inatokea changamoto naikosa, nimekuwa mtu wa kutamani sana na Mimi niweze kuwa na sehemu moja ya kujipatia riziki lakini inashindikana, na sitaki kukata tamaa licha ya changamoto zote hizi.

Nimejaribu kuanzisha bihashara mbalimbali lakini huwa hazidumu, hata nilianzisha ya kufua na nilipostigi humu Kuna watu baadhi walijitokeza nikawafanyia kwa ufasaha lakini baadae ikatokea changamoto nikashindwa kuendelea. Nashindwa kuelewa ni kitu gani kinanizunguka kwenye maisha yangu na mtaji wangu, inafika kpindi nakosa hata pesa ya kula kwa siku lakini Muumba wetu anazidi kunipa nguvu ya kuendelea kusimama Tena na kupambana.

Na kipindi hiki cha mfungo kwangu kimekuwa ni kigumu sana kwa kukosa pesa ya kujikimu kwa kipindi kizima. Naombeni mnigaie ushauri nifanye nini niweze kusimama imara kwa uthabiti, mwenr kazi pia naomba anisaidie ili niweze kujikimu.

Naombeni mawazo yenu na ushauri wenu maana akili yangu imefikika mwisho kuwaza Mimi ndugu zangu. Nimechoka.
 
Sasa ujarishaa tumbo lako tu unachoka ungekuwa na watoto ungepata akili watu wanawatoto watatu na ni majobless ila wanapambana mpaka ukucha wa mwishooo.........ur not alone tupo wengi ila sometimes shida zikuletea dharau na wew dhizarau utatoboa........
 
Ukisoma masimulizi ya waliofanikiwa kwenye biashara mfano Elon Masks ama Macdonald's wanasema Kuna wakati hali ya biashara iliwaendea vibaya hadi wakatamani ku-quit biashara

Lakini pamoja na kuanguka mara kadhaa, lakini hatimaye alisimama Tena na kufanikiwa.

Endelea kujipa muda, utafanikiwa Siku Moja

Ukiona biashara hiyo ya Laundry (Ufuaji) hailipi kulingana na Msimu, jaribu kufanya biashara nyingine

Kila la heri Mkuu 🙏
 
Habari Wana JamiiForums,

Nimekuja hapa nikiomba mawazo yenu, ushauri na msaada ikiwezekana. Katika maisha yangu nimejaribu sana kutafuta kazi sehemu mbali mbali bila mafanikio, na hata nikipata haidumu kabisa inatokea changamoto naikosa, nimekuwa mtu wa kutamani sana na Mimi niweze kuwa na sehemu moja ya kujipatia riziki lakini inashindikana, na sitaki kukata tamaa licha ya changamoto zote hizi.

Nimejaribu kuanzisha bihashara mbalimbali lakini huwa hazidumu, hata nilianzisha ya kufua na nilipostigi humu Kuna watu baadhi walijitokeza nikawafanyia kwa ufasaha lakini baadae ikatokea changamoto nikashindwa kuendelea. Nashindwa kuelewa ni kitu gani kinanizunguka kwenye maisha yangu na mtaji wangu, inafika kpindi nakosa hata pesa ya kula kwa siku lakini Muumba wetu anazidi kunipa nguvu ya kuendelea kusimama Tena na kupambana.

Na kipindi hiki cha mfungo kwangu kimekuwa ni kigumu sana kwa kukosa pesa ya kujikimu kwa kipindi kizima. Naombeni mnigaie ushauri nifanye nini niweze kusimama imara kwa uthabiti, mwenr kazi pia naomba anisaidie ili niweze kujikimu.

Naombeni mawazo yenu na ushauri wenu maana akili yangu imefikika mwisho kuwaza Mimi ndugu zangu. Nimechoka.
maisha ni fumbo kubwa ambalo kulifunua inahitaji hekima na ufahamu wa juu sana

"Ulivyo ni matokeo ya jinsi unavyofikili unachofikili"

Mafanikio ya kudumu huanzia NDANI ya MTU, and vice versa (i.e anguko au kutokufanikiwa kwa mtu huanzia NDANI kwa Maana ya moyoni)

Kuna vitu viwili ni muhimu sana katika maisha ya MTU yeyote mwenye akili

1/ malengo > dira ya MAISHA ya MTU
2/ mpango > njia au barabara au ramani ya kuifanikisha dira ( way to achieve our goals)
NDANI ya mpango kuna mikakati ya kiutendaji ya huo mpango

Kama hatujakaa chini na kuset hivi vitu kwa umakini na usahihi hata tupewe 1BILLION nothing we can achieve na sio lahisi kuset hivi vitu inahitaji Hekima na ufahamu na maarifa pamoja na muda na USAFI WA KIROHO (UTAKATIFU/HAKI)😁

Ndio maana vijana wengi leo wanatafuta ajira kwasababu hawana malengo NDANI yao bali wana mpango mmoja t wa kuajiliwa na mtu wa aina hi akishaajiliwa Hawezi kupata financial freedom b'se atakua ni mtu wa kusubiri mshahara mwisho wa mwezi autumie kwasababu hana malengo yoyote 🙆🏻‍♂️

majukumu yanaongezeka kadri siku zinavyokwenda ila mshahara upo fixed ndio maana civil servants wengi wanakufa masikini au maisha yao ni duni Sana

Ushauri
Ukitaka mafanikio ya kudumu Zingatia sana USAFI WA KIROHO (UTAKATIFU/HAKI) B'se Hapa ndipo penye kila kitu cha MAISHA ya mwanadamu kuanzia kesho yetu, malengo ambayo MUNGU ameweka NDANI yetu na mipango au wazo au Neema ambayo MUNGU ameweka NDANI yetu kwaajili ya kutimiza malengo ambayo ameweka ndani yetu na vitu vyooooooooote kwaajili ya kufanikiwa vipo NDANI ya USAFI WA KIROHO (UTAKATIFU/HAKI)
 
Tukiacha ya kufua, umewah kufanya biashara gani na uliifanya kwa muda gani

Na ktk muda uliofanya biashara, umejifunza chochote tukiacha hizo changamoto zako za kiiman?
Ndiyo nimejifunza mengi sana mkuu. Namshukuru Mungu, naendelea kupambana licha ya changamoto zote hizo.
 
Back
Top Bottom