Hiki ni nini? Naombeni ushauri nachanganyikiwa. Nimekopa Milioni 14 natakiwa kurudisha Milioni 39

muafi

JF-Expert Member
Oct 6, 2015
2,115
4,802
Nimevumilia ila nimechoka acha niwaambie, ndugu walimu nimekopa ABC bank shilingi milioni 14 nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi.

Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaani nakopa 14M narudisha 39?
Mimi kwakua nilikua nina dharula ya haraka sana nilienda ABC maana niliambiwa kule hauzunguki sana na nilipofika niliongea nao tu muda ule ule nikajaza fomu nikaondoka mkopo ukaingia kesho yake, najuta sikupata muda wa wenda kusoma makubaliano na wala hawakunipa nakala yoyote!

Hii sio haki serikali iko wapi jamani?

Nifanyeje naombeni ushauri wenu.

View attachment 2744997
 
NIMEVUMILIA ILA NIMECHOKA ACHA NIWAAMBIE, NDUGU WALIMU NIMEKOPA ABC BANK SHILINGI MILIONI 14 Nikatwe kwa miaka nane sawa na miezi 96, nakatwa shilingi laki nne na elfu 14 kwa mwezi,
Nimeshangaa kukuta kwenye salary slip deni ni milioni 39😥😥😥, nimelia sana yaan nakopa 14M narudisha 39? Hii sio haki serikali iko wapi jamani😭😭😭😭View attachment 2744878
Screenshot_2023-09-10-13-20-43-901_cz.hipercalc.jpg

Ni sahihi kimahesabu.

Embu tuambie mlivyokubaliana kwanza ili tuelewe
 
Walimu na mikopo ni damu damu...huo ni msalaba ndg...yaaani una kaz na safari ndefu....piga akil sana upate issue ya kukuongezea kipato eg.kilimo au extra work curriculum unless u lost maana ulisaini mkataba bila kuchek terms and conditions
 
Waalimu kabla ya kukopa uliza riba ni asilimia ngapi? Kama huwezi kujua hilo, waambie rejesho kwa mwezi litakuwa kiasi gani uzidishe kwa idadi ya miezi uliyekopa halafu jumla yake utoe kwenye mkopo waliokupitishia.

Mara nyingi huwa Wana take advantage ya umbumbumbu wa waalimu kwenye elimu ya fedha kwani wao huuliza tuu watapata kiasi gani na kwa muda gani tuu, suala la riba, gharama za mkopo kama loan processing fee, bima nk hawajui, na ukiuliza riba kichwa kichwa badala ya kukuambia riba kwa mwaka, anaigawanya kwa 12 anakuambia riba ya mwezi wewe ukiona digit ni ndogo inaingia mkenge.
 
Back
Top Bottom