Mimi ni Mkristo nataka kufunga ndoa ya mitala nafanyaje?

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,577
18,904
Habari wanajf

Mimi ni mkristo moja kati ya ndoto zangu ni kuwa na wake wawili mmoja muislamu mwingine mkristo. Hii kitu imekuwa ikija kichwani hivi karibuni kwasababu nimekuwa na bahati ya kupata mabinti wa kislamu tena unakuta ni wife material wanastahili kuwekwa ndani na nimekuwa nikidumu nao kwenye mahusiano kwa muda mrefu.

Shida inakuja kwa Wazazi wao ili nioe binti zao ni lazima eti niibadilishe dini kwanza sasa hiki kitu sikitaki. Kwanini nataka mmoja awe wa kikristo mwingine muislamu? Kwababu ili kutocomplicate vitu especially kwa upande wa mke wa kislamu abakie na dini yake na watoto nitakaozaa nae wafate dini ya mama yao hapo nitakuwa nimewaridhisha Wazazi wake.

Naombeni ushauri nifanyeje nioe ndoa ya namna hii ya mke mmoja wa kikristo mwingine wa kislamu
 
Sasa unaomba ushauri wa kidini au kijamii? Yaani unataka kuoa na dini yako ibariki hiyo ndoa au wewe kinachokukwamisha ni kipi?
 
Kuna Wakristo kadhaa wana wake zaid ya mmoja cha msingi uwe na msimamo

Hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa Mkristo mzuri tu na alikuwa na wake wawili na hata alipokufa alizikwa kwa heshma zote za kanisa

Hayati Samwel Sitta sio tu alikuwa Mkristo mzuri bali alikuwa ni mmoja wa Wazee wa kanisa lakin alikuwa na Wake wawili na hata alipokufa alizikwa kwa heshma zote za imani yake mmoja unaoa kanisani. mwingine bomani au kimila

Kuna Mzee mwenzangu wa kingoni yeye ana wake watatu na ni mkristo na kanisani kama kawaida na hata zile Jumuiya za kila Jumamosi asubuhi zinazunguka kwa wake zake wote watatu ila Ngawira kwa maana ya rasilimali fedha anazo za kutosha
 
kuna Wakristo kadhaa wana wake zaid ya mmoja cha msingi uwe na msimamo

Hayati Edward Moringe Sokoine alikuwa Mkristo mzuri tu na alikuwa na wake wawili na hata alipokufa alizikwa kwa heshma zote za kanisa

Hayati Samwel Sitta sio tu alikuwa Mkristo mzuri bali alikuwa ni mmoja wa Wazee wa kanisa lakin alikuwa na Wake wawili na hata alipokufa alizikwa kwa heshma zote za imani yake

mmoja unaoa kanisani. mwingine bomani au kimila


kuna Mzee mwenzangu wa kingoni yeye ana wake watatu na ni mkristo na kanisani kama kawaida na hata zile Jumuiya za kila Jumamosi asubuhi zinazunguka kwa wake zake wote watatu ila Ngawira kwa maana ya rasilimali fedha anazo za kutosha
Dini ya kikuristo haina msimamo wako after worldly wealth......
 
Sheria ya ndoa ina mapungufu sana. Nikupe maujanja kama ifuatavyo.

1. Huwezi funga ndoa hiyo kwenye dhehebu ulikofungia ndoa. Ilaa, jua tu kuwa mpaka sasa hakuna database ya waliofunga ndoa. Hivyo ukihama kanisa au dhehebu mfano ukitoka katoliki au lutheran aukienda pentekoste unafufunga tuuu, assemblies unafunga. Nk. Hapo ni kama mkeo ameridhia na hatakufanyia kosa.
2. Ukihama mikoa. Umko mwanza. Kafungie mtwara...songea tena mbinga hukooo....nk

Mbona maujanja ni mengi tuuu.

Sent from my SM-N986B using JamiiForums mobile app
 
Turudi kwenye tamaduni zetu mke mmoja ni utamaduni wa kizungu. Fanya kile ambacho moyo wako utakupa furaha . Hapa duniani hatuishi kwa kumshikia mtu mwingine zamu ya kuishi.

Kuishi hapa duniani ni kwa zamu kwahiyo hakikisha unaitumia vizuri zamu yako kabla hujafa kupisha zamu za wengine kuishi.
 
kuna Wakristo kadhaa wana wake zaid ya mmoja cha msingi uwe na msimamo
Asante mkuu kwa kunipa moyo kwa mkristo haina shida kwenye kuoa vip kuhusu manzi wa kislamu ni aina gani ya ndoa nioe
 
Suala la mke mmoja lilikua ishauri sio sheria..sasa kwa nini uwake tamaa jamaa..wewe oa hata kumi chamsimgi tunza familia yako hasa watoto wako wapate huduma zao stahiki kama elimu malazi,chakula mavzi n.k

#MaendeleoHayanaChama



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wanajf

Mimi ni mkristo Moja Kati ya ndoto zangu ni kuwa na wake wawili mmoja muislamu mwingine mkristo.Hii kitu imekuwa ikija kichwani hivi karibuni kwasababu nimekuwa na bahati ya kupata mabinti wa kislamu Tena unakuta ni wife material wanastahili kuwekwa ndani na nimekuwa nikidumu nao kwenye mahusiano kwa muda mrefu shida inakuja kwa Wazazi wao ili nioe binti zao ni lazima eti niibadilishe dini kwanza sasa hiki kitu sikitaki.kwanini nataka mmoja awe wa kikristo mwingine muislamu? Kwababu ili kutocomplicate vitu especially kwa upande wa mke wa kislamu abakie na dini yake na watoto nitakayozaa nae wafate dini ya mama yao hapo nitakuwa nimewaridhisha Wazazi wake

Naombeni ushauri nifanyeje nioe ndoa ya namna hii ya mke mmoja wa kikristo mwingine wa kislamu
Hujawahi kuwa M-Kristo usijidanganye. Ukristo sio dini.,


JESUS IS SAVIOR
 
Yaani ushauri wa kuoa nani unakuja utafuta JF!

Huna wazazi au ndugu wa kuwashirikiaha jambo muhimu kama hili?
 
Back
Top Bottom