Kosa kubwa tunalolifanya kabla ya kufunga ndoa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,561
3,471
Nimejaribu kutafakari ni kwanini kasi ya kupeana talaka na migogoro ya kwenye ndoa imeongezeka mara dufu katika zama hizi kuliko kipindi chochote kile na nilichokibaini ni kwamba kuna mahali tunakosea.

Ikumbukwe kuwa watu wanapoamua kuishi pamoja kama mke na mume au kufunga ndoa ni moja ya maamuzi magumu sana katika maisha ya mtu licha ya mazoea na tamaa zinazotusumbua wengi. Kufunga ndoa kwa njia yoyote ile (kimila, kiutamaduni, kidini n.k) ni uamuzi wa kuwekeza maisha au uhai Kwa mwingine, ni kuigawanya imani yako mara mbili.

Tatizo tunalichukulia suala hili kwa wepesi kuliko lilivyo jambo ambalo kwa kweli limegharimu matarajio ya wengi na pia limesababisha vifo na maradhi mengi kwa watu. Ili nisiwachoshe niende kwenye kiini kwa kusema;
Tunachokosea ni kutokuwekeza kabisa katika kupata maarifa ya ndoa kama tunavyowekeza katika kupata maarifa mengine yanavyotusaidia kuwa mainjinia, wanasheria waalimu n.k.
Kama mtu anasoma miaka 23 hadi 25 Ili kuwa na shahada ya juu ya udaktari bingwa wa Binadamu tena katika ugonjwa mmoja tu ni dhahiri kuwa suala la maarifa mengine tumelipa uzito sana.

Leo vijana wengi hatupitii mafunzo ya jando na unyago ambayo Kwa kiasi fulani yaliwasaidia wazazi wetu, Watu tunaoana tukiwa hatuna maarifa yoyote licha ya ukweli kuwa maarifa ni nguvu "information is power".Tunaingia mahali ambapo tunawekeza maisha na muda wetu tukiwa hatuna maarifa.

Tunapooana hatuoani kimwili tu, kuna mambo ya kiroho pia yanaingiliana. Tatizo ni pale tunapoingia tukiwa hatuelewi chochote, hali hii ni zaidi ya hatari. Watu hatuoni kiroho "spiritual dimension" hatuna maarifa ya kimwili na wakati huo tunataka kufungamana maisha yetu.
 
Hakuna mwenye script ya ndoa
Kuwa na taarifa na maarifa sahihi kunaweza kusaidia kuliko kupuuzia. Hakika suala hili halina mtaalamu wake ila maarifa na taarifa sahihi kabla ya kuingia ni nyezo muhimu kwa vijana kuliko hali ilivyo sasa
 
Nimejaribu kutafakari ni kwanini kasi ya kupeana talaka na migogoro ya kwenye ndoa imeongezeka mara dufu katika zama hizi kuliko kipindi chochote kile na nilichokibaini ni kwamba kuna mahali tunakosea.

Ikumbukwe kuwa watu wanapoamua kuishi pamoja kama mke na mume au kufunga ndoa ni moja ya maamuzi magumu sana katika maisha ya mtu licha ya mazoea na tamaa zinazotusumbua wengi. Kufunga ndoa kwa njia yoyote ile (kimila, kiutamaduni, kidini n.k) ni uamuzi wa kuwekeza maisha au uhai Kwa mwingine, ni kuigawanya imani yako mara mbili.

Tatizo tunalichukulia suala hili kwa wepesi kuliko lilivyo jambo ambalo kwa kweli limegharimu matarajio ya wengi na pia limesababisha vifo na maradhi mengi kwa watu. Ili nisiwachoshe niende kwenye kiini kwa kusema;
Tunachokosea ni kutokuwekeza kabisa katika kupata maarifa ya ndoa kama tunavyowekeza katika kupata maarifa mengine yanavyotusaidia kuwa mainjinia, wanasheria waalimu n.k.
Kama mtu anasoma miaka 23 hadi 25 Ili kuwa na shahada ya juu ya udaktari bingwa wa Binadamu tena katika ugonjwa mmoja tu ni dhahiri kuwa suala la maarifa mengine tumelipa uzito sana.

Leo vijana wengi hatupitii mafunzo ya jando na unyago ambayo Kwa kiasi fulani yaliwasaidia wazazi wetu, Watu tunaoana tukiwa hatuna maarifa yoyote licha ya ukweli kuwa maarifa ni nguvu "information is power".Tunaingia mahali ambapo tunawekeza maisha na muda wetu tukiwa hatuna maarifa.

Tunapooana hatuoani kimwili tu, kuna mambo ya kiroho pia yanaingiliana. Tatizo ni pale tunapoingia tukiwa hatuelewi chochote, hali hii ni zaidi ya hatari. Watu hatuoni kiroho "spiritual dimension" hatuna maarifa ya kimwili na wakati huo tunataka kufungamana maisha yetu.
Ndoa ni ubatili, ndio ni ufala, ndoa ni ushetani kataa ndoa kataa kuoa, kataa, lakataa likitii, leketee, lokotoo, lukutuu kataa kuoa kuoa ni ushetani mkubwa
 
Haki sawa imeua ndoa nyingi....

Katika serikali yeyote lazima awepo mkubwa na mdogo iwe ya kisiasa,kiimani,kitamaduni at kimahusiano..

Shida mwanamke anapotaka kumuongoza mwanaume au wote walingane kivyovyote, kifedha, kimaamuzi, kiutawala na kimajukumu.....🤔🤔🤔
 
Haki sawa imeua ndoa nyingi....

Katika serikali yeyote lazima awepo mkubwa na mdogo iwe ya kisiasa,kiimani,kitamaduni at kimahusiano..

Shida mwanamke anapotaka kumuongoza mwanaume 🤔🤔🤔
Well said!...tatizo hatuelewi sawa kwenye nini?...
 
Wala hatuhitaji kuwa na degree,masters au Phd ya ndoa.Wanandoa wakijua haya yanatosha kufanya ndoa idumu.Upendo, kuchukuliana,uvumilivu na kujishusha.
 
Vijana wa sasa wanaoa kwa sababu wanaamini hapo ndo hawazini, Ili kutimiza matakwa ya dini, Ili asionekane muhuni, ili afuliwe na kupikiwa, Ili akipate kidubwasha muda wowote akitaka.
 
Back
Top Bottom