Ikiwa haya yatafanyika, basi ndoa zitadumu

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,962
6,897
Hey there,

Inakuwaje wadau wa humu ndani... Hope mpo poa na kama kuna tatizo lolote yeyote alienalo basi maombi yangu kwake ni Mungu amfanyie wepesi. Twende kwenye mada.

Marriage/Ndoa imekuwa ni big issue hasa humu kwenye platform ya JF, Huku kukiwa na makundi mawili (wanaounga mkono ndoa na wanaopinga ndoa). Kila mmoja akiwa na sababu zake ambazo anaziona ni za msingi.

Binafsi mimi siwezi kuchagua side ya kuunga mkono kutokana na mapungufu yalio katika pande zote mbili. Kwani ukichunguza ni kwamba mfumo wa kuifanya ndoa iwe ume-base sana katika kumkandamiza mwanaume kwa kiasi chake na mapungufu hayo utayaona pindi tu inapofika hatua ya kutokuelewana baina ya Mume na Mke kutaka kuivunja ndoa. Sitaki kubase sana hapo maana sababu zaweza kuwa nyingi na pengine nyingine zikawa zimesabishwa na mwanaume mwenyewe ila ninachoamini ni kwamba kwa kuwa kwenye ndoa kuna sheria basi hata mwisho wake huamuliwa kwa kuzingatia sheria inasema nini na hapo ndipo kulipo na mapungufu fulani.

Okay twende direct kwenye point, Kutokana na wingi wa idadi ya kuvunjika kwa ndoa na wengi wetu wanaume kufika hatua ya kuiona ndoa haifai katika maisha yao, Basi ni kwanini kisingeongezeka kipengele cha kusainishana "Mkataba" baina ya wanaohitaji kuingia kwenye ndoa (Mwanamke na Mwanaume)

Hapa namaanisha kwamba mkataba huo utaorodhesha kila kitu ambacho wanakihisi kinaweza kuleta mgogoro wa aina yoyote baina yao. Hapo namaanisha kwamba Mkataba huo upitishwe kisheria kabisa ambapo wapenzi hao kila mmoja atapewa asome na kuweka sahihi ya kukubali au kukataa katika vitu ambavyo vimeorodheshwa kwenye mkataba huo.

Mkataba utakuwa kwenye format ya kumuhusu muhusika unaekwenda kufunga nae ndoa, Mfano;- Mkataba wa kumuhusu mume atakaopewa mwanamke kuujaza⬇️

-Kwa kazi anayofanya mumeo itamlazimu kutokulala nyumbani, Je utaweza kumudu hiyo changamoto?
Ndiyo ⬜ Hapana ⬜.

-Kutokana na tabia ya mumeo anasema kwamba ni mnywaji wa pombe hivyo wakati mwingine anaweza kurudi akiwa amelewa chakari, Je utaweza kumudu hiyo changamoto?
Ndiyo ⬜ Hapana ⬜.

Huo hapo juu ni mfano wa moja ya maswali ambayo yanaweza kuwepo katika mkataba huo husika.

Kwahiyo sasa mikataba itakapokuwa katika format hiyo basi itakuwa ikieleza undani wa mtu na tabia zake au aina ya maisha ambayo pengine bila huo mkataba ungejikuta unaingia kwenye ndoa ndipo unakuja kugunduq kwamba umekosea kuoa au kuolewa. Mkataba utaweza kuweka makubalino thabiti ya kila kitu ambacho kitahusiana na maisha yenu mtakapokuwa wanandoa.... Mkataba utahusisha kila kitu hadi kumtambua nani atakaekuwa na jukumu la kuhusumia familia kwenye kila kitu au kama mtashirikiana 50/50 n.k

So kwa mtazamo wangu nahisi kukiwekwa kitu kama hicho basi ndoa itaheshimika na hakuna ambae ataingia kwenye ndoa kama fashion, Pia kuwekwe taratibu za adhabu ikiwa mtu ataenda kinyume na makubaliano ambayo atakuwa ameyafanya.... Ikiwa mtu tajibu "No" katika kipengele chochote ambacho pengine kwa mwenza wake ni "YES" basi kufunga ndoa kusipitishwe hadi wakajadiliane wote either kubadili nyenendo ya muhusika au mmoja wapo kukubali kuvumilia hali hiyo.

Naandika haya yote sio kupoteza muda ila ni kwa kuwa Ndoa ni makubaliano na kiapo cha watu wawili kuishi pamoja milele katika shida na raha hivyo haitakiwi kuchukuliwa juujuu bali ni jambo zito ambalo linapaswa kuwekewa uzito wa hali ya juu ili kupunguza matokeo mabaya tunayoyaona kwenye maisha ya sasa. Wanasaini mikataba watu kwenye mambo madogo ya muda mfupi sembuse ndoa ya Milele... Ebu tuacheni masihara na ndoa bana, Dunia ya sasa sio kama ya zamani ya sasa imechangamka sana kila Mtu anataka kuwa pale, Kila Fish anataka kuwa kambale... Ukitaka kuishi kienyeji kwa kukariri walivyoishi mababu zetu utakuwa unaweka mapazia kwenye milango ya fahamu zako.

RE•PITIENI POST YANGU YA MASHUKA NA MAPAZIA MNIUNGISHE WAKUU SINA MCHONGO MWINGINE HAPA TOWN

23YRS WITH BIG ISSUES
•FLAMES WAS HERE
 
Aisee ndoa imekua ngumu kiasi hiki?


NB: Weka link ya Mapazia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom