Naanto Mushi
JF-Expert Member
- Oct 16, 2015
- 6,236
- 15,603
Ukweli huyu ninayemuita mke wangu, hatuna ndoa kamili ya kanisani, pamoja na kuishi miaka 8 na kubahatika watoto wawili (Miaka 7 na miaka 3).
Sasa msukumo wa ndoa umekuwa mkubwa sana kutoka pande zote, na yeye mwenzangu naona hii kukosa ndoa inampa sononeko maana wazazi wake wanaogopa nisije nikamuacha (japo hii sababu sioni kama ina mashiko, kwasababu hata ukiwa na ndoa unaachika tu).
Ukweli mwingine ni kwamba, sababu haswa ya kutokufunga ndoa mpaka sasa, ambayo naijua mwenyewe ni kwamba, mi sio mtu wa shereha kabisaaaa.
Yaani kila nikikaa chini nikajifikiria kwamba nipo sijui navalisha pete ya uchumba, sijui nipo natoa mahari, sijui nipo mbele ya kadamnasi ya kanisa na padri pale mbele, sijui nipo kwenye ukumbi watu kibao. Yaani sijioni kama naweza lolote hapo na sipendi hayo mambo.
Ninachokifikiria kichwani ni kufunga ndoa isiyokuwa na kelele, nilitaka kufunga ya serikali, naona mwenzangu akagoma, anataka ya kanisani.
Sasa hapa wazo limenijia nakumbuka kuna zile ndoa zamani zilikuwa zinafanyika mkesha wa mwaka mpya au krismasi kama sijasahau, maana ni kipindi nipo mdogo, enzi hizo nahudhurua kanisani. Unakuta kuna ndoa kama sita hivi za haraka haraka. Hiyo ndo naona inanifaa kwa sasa.
Embu kwa wakatoliki wenzangu naombeni utaratibu wa ndoa hii ya fasta fasta isiyohitaji kelele. Ila ubaya mwingine ni kwamba mimi pia sio mtu wa kwenda jumuiya... yaaaaniiiii
Asanteni, naombeni ushauri ili nimalize hili jambo