Mimi kama mdau wa utalii nina ombi Kwa TANAPA

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Wakuu habari za weekend,

Last week nilienda kupumzika mbugani mikumi, na nikalala kwenye bandas za Tanapa.

Mambo ambayo nimejionea Aisee ni mambo ya aibu Sana hasa tukijua kuwa Tanapa inakusanya ela nyingi Sana kutoka kwa watalii.

Bandas zote zina matatizo, na hata mhusika mwenyewe anakwambia kabisa wakati unafanya uchaguzi ulale kwenye bandas gani.

Mfano me nilitaka kulala room ya mwanzo kabisa akanambia Ac mbovu, na Feni mbovu duuh, nikachagua nyingine, akanambia hiyo Ac mbovu Ila fen mzima haha, nikataka nyingine akanambia hiyo vyote vipo Ila hakuna maji ya moto na Choo hakiflush vizuri hahaha.

Nikalala room yenye Ac Tu but Choo kizima, sasa hiyo Ac yenyewe hakuna remote it's like bandaz zote wanatumia remote moja.

Ac I think hazina service Kwa muda mrefu, Tv ipo Tu imekaa kama mapambo nayo haina chochote.

Hayo mashuka sasa ndio balaa ni kama ya gest za sinza zile za elfu 15.

Sasa nashindwa kuelewa why wanashindwa kufanya maintenance? How come dunia ya Leo hata WiFi hakuna? Na kule ndani ni porini network za simu ni ishu.

Najua kuna wadau wa Tanapa kwenye hii JF please wafanyie kazi mapungufu ni mengi Sana.
 
Sema bei ya kulala kabla ya kulalamika? Bei zake ni kama za guest za sinza lazima ziwe za viwango hivyo hivyo!

Huwezi lala mbugani kwa hizo bei? Ukitaka kiwango lipa kiwango! Hayo yamewekwa temporary kwa ajili ya wanafunzi na mafrongo...
 
Wazungu huwa hawalali humo hivyo basically ni kwaajili y wanafunzi na watanzania wa low budget.

Kama unavyoolewa sisi watanzania wenyewe kwa wenyewe tunaonana km mbwa fulani hivi ndio maana tunalazwa kwenye mabanda sababu budget ni ndogo..

Pole sana hata sisi huwa tunagombana nao sana sabbu y miundombinu hifadhini ikiwa mibovu na huwa wanarekebisha.bila kuongea hata kama wanaona kuna tatizo hawatekelezi.
 
Bei zake Kwa sinza unapata lodge ambayo unapata na chai asubuh
 
Wazungu huwa hawalali humo hivyo basically ni kwaajili y wanafunzi na watanzania wa low budget....
Kama unavyoolewa sisi watanzania wenyewe kwa wenyewe tunaonana km mbwa fulani hivi ndio maana tunalazwa kwenye mabanda sababu budget ni ndogo....
Pole sana hata sisi huwa tunagombana nao sana sabbu y miundombinu hifadhini ikiwa mibovu na huwa wanarekebisha.bila kuongea hata kama wanaona kuna tatizo hawatekelezi.

Sasa hakuna maana ya kupiga kelele za utalii wa ndani coz mtanzania wa kawaida hawez kwenda kulala room ya usd 600
 
Kwahivyo haya uliyosema hapa yana justify facilities kuwa mbovu? Daah......my Tanzania people

Hey cost defines quality “idiot” wame target wanafunzi, sogea hapo pembeni angalia office zao, hata vyoo vya public, they are so clean, wakiongeza tu kiwango wewe huwezi lipa!

Weka bei umelipa bei gani? Mbona huwezi!
 
Bei zake Kwa sinza unapata lodge ambayo unapata na chai asubuh

Absolutely, jamaa analalama kila kitu, mie nimeenda mbugani mara 1000 Sijui hata hayo mabanda yako wapi!

Na, why wanayaita mabanda? Kwa sababu Kuku wanaweza pia kuhifadhiwa huko, Ac ya nini?
 
Wazungu huwa hawalali humo hivyo basically ni kwaajili y wanafunzi na watanzania wa low budget.

Kama unavyoolewa sisi watanzania wenyewe kwa wenyewe tunaonana km mbwa fulani hivi ndio maana tunalazwa kwenye mabanda sababu budget ni ndogo..

Pole sana hata sisi huwa tunagombana nao sana sabbu y miundombinu hifadhini ikiwa mibovu na huwa wanarekebisha.bila kuongea hata kama wanaona kuna tatizo hawatekelezi.

Ajalazwa kwenye Banda na mtu, amechagua kulala kwenye Banda!
 
Back
Top Bottom