Je, Soka linaweza kushirikiana vipi na Sekta ya Utalii ili kukuza utalii?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
SA Tourism ama Bodi ya Utalii ya Taifa la Afrika ya Kusini ilitangaza kuwa imepeleka proposal yake ya kutaka kudhamini moja ya timu kongwe iliyopo Jijini London, Uingereza. Fedha ambayo ilipigiwa hesabu ni dola milioni 52 za kimarekani katika mkataba ambao utakuwa ni wa miaka mitatu. Mkataba huo ndani yake kuna vipengele vitakavyowaruhusu SA Tourism kutanganza utalii wa Afrika ya Kusini wakiwa na timu hiyo.
SA-Tourism-board-members-resign.jpg

Hawa ni Tottenham Hotspur ambao ni timu kubwa sana duniani na ndani ya soka la Uingereza na Ulaya kwa ujumla, wakiwa na mataji X ya ligi kuu pamoja na kufika hatua ya X katika ligi ya Mabingwa Ulaya. Kitendo cha kutengeneza tu proposal na kuiwasilisha ndani ya uongozi wa timu sampuli ya Tottenham basi sio jambo la kitoto hata kidogo, Nigeria wala Ghana hawakuweza kufanya hili ila Afrika ya Kusini wameweza kuwasilisha offa yao.
thumbs_b_c_e4e6b7a97aaefe3215042222b6178ea2.jpg

Moja kati ya njia bora sana ya kutangaza biashara pamoja na huduma ni kupitia michezo, haswa michezo ya Mpira wa miguu, mpira wa kikapu, Cricket, Mapigano ya UFC pamoja na michezo ya langalanga maarufu kama Formula One, hii ni michezo ambayo inavutia watu wengi sana duniani, na inakusanya kiasi kikubwa sana cha mashabiki ambao ndani yake unaweza kupata na wateja wako. Pepsi sio mpumbavu kuweka pesa zake kuithamini Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), hata Total Energies walikuwa na macho ya kiroho kuidhamini Michuano ya African Cup of Nations.

Sasa ukishaelewa nguvu na mvuto uliopo ndani ya michezo mikubwa duniani ni vyema ukafahamu namna ya kurahisisha pia baadhi ya shughuli za kijamii ambazo zinaweza kupata wateja wengi aidha kupitia huduma au bidhaa fulani, unaweza kutazama umakini uliopo baina ya makampuni ya vinywaji ya Coca Cola, Pepsi, pamoja na Heineken ambao hawana muda wa kuchezea fursa.
image-3P11-EN-large-1x.jpeg

Udhamini wa timu au mwanamichezo fulani, mathalani pamoja na udhamini wa matukio ya kimichezo imekuwa ni sehemu kubwa sana ya mafanikio ya makampuni makubwa sana (Niliwahi kujiuliza Je kwanini huwezi kuona wanamichezo wakubwa wakitumia bidhaa ovyo ovyo kama walivyo wachezaji wengine), baadhi ya makampuni hutumia nguvu kubwa ya fedha katika kumdhamini mwanamichezo huku wakitegemea kupata wateja kupitia mwanamichezo huyo.
60c8c0aba5b7f.jpg

Nikupe mfano mzuri, Christiano Ronaldo ndo anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi mtandaoni, Jiulize tu, akipoweka chapisho kuwa ametembelea Hifadhi ya Serengeti, ushawishi wake utakuwa ni wa kiwango kipi? Chapisho lake litakwenda kupata kupendwa na maelfu ya watu ulimwenguni ambao wanamfuatilia mtindo wake wa Maisha. Dunia inamfahamu vyema kabsa kuwa ana ushawishi kwa watu zaidi ya bilioni moja, lakini je ni wangapi wanaomzunguka wanaongea naye kuhusu tu Afrika na vivutio vyake vya utalii? Unakuta soga ambazo anapewa ni kuwa kuna Malaria na Kipindupindu tu!? Utani kidogo!
cristiano-ronaldo-600-million-instagram-followers-sportstiger-1691160366894-original.jpg

Turudi kwenye mada kuu! Tanganyika tupo nyuma sana linapokuja suala la kutangaza vivutio vyetu, kiasi kwamba wageni ndo wanakuwa mstari wa mbele kwenye kuelezea Hifadhi ya Katavi ina Wanyama wazuri na maua ya kuvutia, yaani Bongo Zozo anazungumzia Vivutio vyetu utadhani ni mzawa kumbe hata sio mzawa wa Tanganyika (*nazungumzia Tanganyika kwa sababu Zanzibar wanaelewa wanachokifanya mpaka watu mashuhuri wanafika Pemba na Unguja kimya na kuondoka Kimya kimya bila hata Millard Ayo kufahamu kuwa kuna mtu fulani alifika Zanzibar).
pic-bongo-zozo.jpg

Lengo kuu la Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini ni kupanua wigo mkubwa wa Utalii wa Afrika Kusini haswa ndani ya Uingereza, wao wanaamini kuwa uwepo wao ndani ya Tottenham utafungusa pazia kubwa la watu haswa ndani ya Ulaya kuanza kwenda kutazama vivutio vya utalii ambavyo vipo ndani ya Afrika Kusini. Lakini Afrika Kusini watakuwa sio watu wa kwanza kufanya hivyo, kwani 2013 Malaysia wao waliwadhamini Cardiff City.
3b8f2cdb-abba-45f5-b5ed-b1de050c9777_1600x900.jpg

Rwanda majirani zetu walijiwahi na kuweza kula shavu kwa Arsenal, watu wa soka watakuwa wameona “Visit Rwanda”. Qatar Foundation wao wanatoa pesa kwa FC Barcelona huku Qatar Airways wakiwadhamini PSG.
G-arsenal sleeve.jpg

2016 Bodi ya Utalii ya taifa la Puerto Rico wakajipenyeza na kuingia kwa FC Sevilla huku wakitia saini makubaliano na Kampuni ya Serikali inayoitwa La Compania De Puerto Rico ambapo lengo kuu ni kuitangaza Puerto Rico, na mbele ya jezi yao Fc Sevilla watakuwa wakiwa na maneno SeePuertoRico.com lakini kabla ya Puerto Rico, Fc Sevilla walikuwa wakivaa jezi zenye mdhamini Visit Malaysia ila punde baada ya kushinda taji lao la pili la UEFA Europa, takwimu za Fc Sevilla zikapanda maradufu na kuongezeka zaidi ya mara 2.5 hivyo kuongeza thamani ya udhamini kitu ambacho Visit Malaysia walishindwa kuendelea kudhamini tena timu hii.
pepe-castro-posa-tras-el-acuerdo-con-puerto-rico--sevillafc.jpg

Ukitazama kwa ukaribu kinachoendelea kwenye kampuni za Qatar Airways pamoja na Fly Emirates basi utashangaa kuona akili za hawa waarabu kwani wanaonesha jerui ya fedha kwa kudhamini timu kubwa duniani. Kuanzia PSG, AC Milan, Barcelona, Arsenal, Real Madrid, pamoja na X, ambapo udhamini wao unaziongezea thamani sana timu hizi huku pia wakitangaza kampuni zao pamoja na mataifa yao.
530286292.0.jpg

Kweli Tanzania tumeshindwa kuandaa proposal ya kudhamini timu ambayo inatangaza vivutio vyetu huko nje, au ndo tumeridhika na takwimu za TBC na Safari Channel kuwa watalii wanamiminika kumbe ni uongo mtupu? Sitaki kulaumu kuwa serikali ya CCM ndo wanaohusika ila hata sisi wanatanganyika kweli imekuwa ngumu kutumia nyezo zetu kuonesha uzalendo wa taifa letu pendwa.

Mimi binafsi mawazo yangu ni haya:
  • Kwa Bunge:​
  • Bunge la Tanzania lina majukumu mapana sana ya kufanya nchi itembee na ipige hatu kila wakati, wao ndo wanaotuwakilisha wananchi kwenye kutoa maamuzi ya mambo magumu kwa mustkabali mzima wa watanganyika (*wazanzibar wao wana baraza lao la wawakilishi). Waunde kamati maalumu ya kutanganza utalii, kamati ambayo ndani yake wawepo watu wazalendo haswa, sio machawa kama kina fulani waliopiga debe Masai waondolewe kwenye maskani yao, kamati ichaguliwe na wananchi kwa uwazi kabsa bila upendeleo.​
  • pic-career-profile.jpg
  • Binafsi naweza kusema kuwa kamati iwe na hawa watu (Adam Mchomvu {Msanii}, Amil Shivji, na Aliko Shamte {Waandaaji wa Filamu, Mbwana Samata {Mwanasoka}, Aunt Maria Sarungi {Mwanaharakati na wengine ambao wana akili timamu na wenye fikra pana kwenye maendeleo ya utalii sio wapiga dili.​
  • TFF na Utalii​
  • Nilipata kufurahi sana niliposikia kuwa Mchezo wa watani wa jadi baina ya Simba na Yanga ni moja ya mchezo mkubwa na wenye kusisimua Afrika Mashariki na Kati, yaani ukiachana na mtanange baina ya Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs basi Tanganyika tuna majaabu yetu, ila cha kusikitisha ni kwamba katika umati mkubwa sana Afrika ambao unafuatilia michezo ya Simba na Yanga hakuna hata punje ya kuonesha kuwa Tanganyika tuna vivutio gani aidha kipindi mchezo unaendelea au hata wakati wa mapumziko.​
  • Hoja yangu ni kwamba ligi zetu za Tanganyika zitangaze vivutio vyetu katika michezo yake, nitakupa mfano, Kama Simba amekwenda Mwanza kucheza na Geita Gold kwenye uwanja wa CCM Kirumba, basi mabango ya uwanja yatangaze vivutio vilivyopo Mwanza, kama ni Saanane na Makumbusho za Mwanza.​
  • Yanga akienda Mbeya kucheza na Lipuli basi uwanjani kuwepo na matangazo ambayo yataonesha kuwa TFF wapo bega kwa bega na bodi ya utalii kuwatangazia na kuwahimiza watangayika na dunia kuwa kuna vivutio vya utalii ndani ya Iringa kama vile hifadhi ya Ruaha.​
  • Pia kwa nafasi nyingine, kwanini serikali kupitia TFF isiweke utaratibu wa timu zetu ambazo zinakwenda kwenye michezo yake nje ya nchi kubeba ujumbe wa nchi kuhusu utalii, kama vile, kuvaa jezi maalumu kutangaza utalii, nitawakumbusha kuwa, Barcelona amewahi kucheza na watani zake Real Madrid akiwa amevaa mdhamini tofauti na Sportify, hawa jamaa walivaa nembo ya Bwana Mkubwa Drake, na ilikuwa ni jezi maalumu kwa mechi moja tu, jezi yenye mchoro wa OVO.
  • 4574a362-5df2-4742-9bc5-f1dfced64f49_alta-libre-aspect-ratio_default_0.jpg
  • Sasa kwanini Simba na Yanga wakiwa wanakwenda Misri wasivae Jezi ambao ndani yake itaonesha kuwa Tanganyika tuna jambo letu kuhusu Utalii, kwa siku moja tu, Serikali kupitia Bodi ya Utalii na TFF kwa kuomba ruhusa ya CAF tunaweza kuanza kutumia timu zetu kuwapatia taarifa watu duniani kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanganyika sio Kenya, wajue kuwa sehemu kubwa ya Ziwa Nyaza lipo Tanganyika sio Uganda. Tutafute mbunifu ambaye atatengeneza jezi maalumu yenye ujumbe kwa dunia.​
  • Serikali iache ubabaifu.​
  • Ni jambo la kusikitisha sana kuona serikali ikijitapa kuwa inalenga utalii wa ndani, kwamba watanganyika na wazanzibari ndo waanze kutembelea vivutio kisha wageni ndo wapate moyo. Venice Italia inapokea watalii zaidi ya X lakini watalii hao sio wakazi wa Italia bali ni kutoka nje ya Italia huku kiwango kikubwa wakiwa ni kutoka Uingereza, sasa wao unadhani hizo kaulimbiu za utalii wa ndani hawawezi ehh!? Utalii wa ndani wakati Maisha ni magumu ni sawa na kututusi tu, yaani mtu atoke Iringa afunge safari kwenda Serengeti kutazama Wanyama, na bado nyuma yake anadaiwa kodi ya pango na hajalipa PAYE?​
Mafanikio ya Utalii wa Tanganyika yapo kwa Watanganyika wenyewe!
Mungu ibariki Afrika! Mungu ibariki Tanganyika!
 
Back
Top Bottom