Boda ya Horohoro (Kenya - Tanzania) vyoo ni vichafu na abiria wanakoma kwa joto (AC hazifanyi kazi)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Wiki iliyopita nikiwa natoka Kenya kuja TZ kupitia boda ya Horohoro kuna mambo mawii niliyoona na yakanikata na kunifanya nitafakari kuhusu mamlaka zetu hizi za Uhamiaji.

Nilikuta mazingira ya vyoo ambavyo vinatumiwa na abiria ni vichafu na vinahatarisha hata afya ya watumiaji, kuanzia unapofika mazingira ya kuingia kwenye sehemu hizo za kujisaidia unakumbana na harufu kali ambayo inaweza kukufanya ukaahirisha unachoenda kukifanya huko ndani

Wakati naingia kulikuwa na watu kadhaa, nikawa naelekea katika moja ya choo kuna abiria alikuwa pembeni yangu akaniambia nisithubutu kuingia humo kwani naweza kusitisha hata haja yangu yenyewe, aliambia ni kichafu na kinatia kinyaaa.

Mazingira ni machafu kwa ufupi.

Nilipoingia ndani kwa ajili ya kufanya taratibu nyingine za kiusafiri abiria tukawa tunajipepea tu, joto kali AC zipo lakini hazifanyi kazi.

Nilihesabu AC zilizokuwepo eneo hilo kama sijakosea ni tatu au nne, zile kubwa, zote hazifanyi kazi.

Nilipomuuliza mmoja wa staff wa pale, kwamba kwa nini AC hazifanyi kazi na abiria tunateseka tu akanijibu “Ndiyo Serikali zetu hizi ndugu.” Kisha akaishia kutabasamu na kuondoka.

Nilikamilisha mambo yangu na kuondoka huku nikiifikiria idara hiyo, inamaana hawana hela ya kutengeneza AC au wanapuuzia, au mpunga umepigwa au uongozi unaona fresh tu kwa kuwa hakuna viongozi wakubwa wanaotumia mpaka huo mara kwa mara?

Nikakumbuka ni juzi tu hapa iliibuka ile video ya Watalii wakilalamikia huduma mbovu za idara moja ya Uhamiaji, kilichofuata wakatumia nguvu kubwa kukanusha.
 
Wiki iliyopita nikiwa natoka Kenya kuja TZ kupitia boda ya Horohoro kuna mambo mawii niliyoona na yakanikata na kunifanya nitafakari kuhusu mamlaka zetu hizi za Uhamiaji.

Nilikuta mazingira ya vyoo ambavyo vinatumiwa na abiria ni vichafu na vinahatarisha hata afya ya watumiaji, kuanzia unapofika mazingira
Sasa uhamiaji wanahusikaje na vyoo?
Au ulidhani kwenye mpaka ni uhamiaji tu, kuna mamlaka zingine eti
 
Horo horo nilipata matatizo sana na Uhamiaji pale. Ilikuwa wakati wa Uchaguzi. Nikarufi Dar nasikitika. Halafu baadaye nikasikia KANU imeshindwa, Mwai Kibaki ameshinda Uchaguzi. Nilifurahi sana.
Nilitoa rushes pale wakati nilikuwa sina kosa lolote,
 
Haya maswala ya usafi wa vyoo na mazingira ya kufanyia kazi, wengi tunayupuuza.
Hivi inakuwaje ofisi inayotoa huduma ina vyoo vichafu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom