Msaada wa kisheria kwa mayatima hawa

mjarrab

Senior Member
Nov 13, 2015
108
55
Ndugu wana Sheria, Nimeombwa niwasilishe kwenu ombi la Msaada wa kisheria kwa Mayatima hawa ambao wanataka kupata mwanga wa kisheria kama kuna uwezekano wa kupata urithi wa haki za Merehemu baba yao.

Baba yao alifanya ushirika wa kufanya kazi na Mjomba wake kwa kufungua kampuni ya Ujenzi, huyo Mjomba anaishi nje ya nchi.

Mjomba al alimiliki share ya kampuni ya asilimia 50,Marehemu alimilikia asilimia 49 na mke wa Marehemu alimiliki asilimia 1 ya kampuni.

Kama ilivyo kawaida ya kampuni ya ujenzi inahitaji kuwa na rasilimali kubwa ikiwemo vifaa,
wamiliki baada ya kuwekeza fedha zao pia waliweka dhmana baadhi ya rasili mali zao kama viwanja nyumba na mashamba katika taasisi za kifedha ili kupata mtaji zaidi wa kuendesha kampuni.

Kampuni ilipata mitambo ya uwendeshaji na mtaji wake, Marehemu ndiye aliye kuwa muendeshaji mkuu wa kampuni kwa sababu yeye ni mtanzania.

Hivyo tenda zote za kazi alikuwa akiomba yeye na kusimamia kazi xa kampuni yeye. Na kampuni ilikuwa ikipata tenda na faida iliyo patikana walikuwa wameigawa sehemu mbili, sehemu moja ni kulipia madeni na sehemu ya pili ni kuimarisha kampuni kwa kuiongezea vifaa.

Marehemu aliendesha kampuni kwa muda wa miaka mitano kwa ufanisi mkubwa kwa sababu kazi zilikuwa zinapatikana na madeni yalikuwa yakipunguzwa na kampuni kuimarishwa. Kwa Bahati huyu baba akatangulia mbele ya haki kwa ghfla akiiacha kampuni ikiwa hai na inafanya kazi na kuingiza faida kwa sababu Mjomba wake anaishi nje ya nchi ikawa si rahisi kuisimamia kampuni hivyo ,ikaonekana kampuni iendelee chini ya usimamizi wa mdogo wa marehemu mpaka mtoto wa marehrmu atakapo pata uwezo wa kuisimamia.

Huyo mdogo wa marehemu hakuwa na ufanisi katika kampuni, akaanza kuwafuta kazi baadhi ya wafanyakazi, na kuwatupia lawama kuwa wafanyakazi wanaihujumu kampuni.

Familis ya marehemu wakaona wamwachishe kijana wao wakiume chuo ili akashike nafasi ya baba yake katika kampuni.

Kijana alipo fika kwenye kampuni akakutana na huyo baba yake mdogo ambaye hukupendezewa na huyo kijana kuja kushika nafasi hivyo akaanza mtungia tuhuma za uongo kwa huyo mjomba wa nje nchi,
Mtoto wa marehemu baada ya kuona hakubaliki kushika nafasi ya baba yake katika kampuni akaamua kujitoa kufanya kazi katika kampuni hiyo.

Na kufungua kampuni yake binafsi kwa vyanzo vyake binafsi. Mtoto wa Marehemu alipo dai familia yake ipewe sehemu ya mali ya baba yao kama urithi wao wajitoe katika kamouni, jambo hilolikaleta mzomzo kwa mjomba wao by pamoja na huyo baba mdogo aliye shika nafasi ya kaka yake katika kampuni.

watoto wa marehem wanaamini kuwa huyu baba mdogo ameiyumbisha sana kampuni kwa usimamizi wake mbovu na mipango yake mibovu, kwani amekwisha fanya maamuzi ya kununua magari yaliyo tumika ambayo hayakuwa na ufanisi katika kampuni.

Huyu baba mdogo amajijengea picha ya uaminifu kwa mjomba wao kiasi kwamba huyo mjomba anamuamini sana na wamefungua kampuni yao ya pembeni ambayo inahamisha baadhi vifaa kutoka katika kampuni ya awali ambayo marehemu alikuwa na shere ya asilimia ya 49.

Watoto Mayatima wanapo dai haki yao ya kurithi sehemu ya share ya baba yao huambiwa kuwa hakuna pesa kampuni haina pesa hata vikiuzwa vitu vyote hawawezi kulipa madeni, labda warithi madeni wanaambiwa watoto hao.

huyo Mjomba kwa kigezo cha kuwa kampuni aliyo share na Marehemu kwa kuwa ina madeni na yeye ndiye anawajibika kuyalipa anahamisha mitambo na kuipeleka kwenye kampuni yake nyingine na kwa kuwa marehemu aliwekeka dhamana ya nyumba na viwanja kwa jina la kampuni huyu mjomba anampango wa kuuza hizo aset kwa madai ya kulipia madeni ya kampuni, anasrma anakuja kufunga rasmi kampuni na kuuza aset zote zilizo wekezwa!

Ndugu wana Sheria ,waroto hawa mayatima wanapoteza kila kitu kwa njia hii. Je! sheria inawalinda vipi waweze kupata haki ya marehemu baba yao?

Huku ikizingatiwa kwamba wakati baba yao anafariki kampuni ilikuwa inafanya kazi kwa faida na kujikuza
Lakini sasa wanaambiwa kampuni imefilisika na ilhali wanaona wazi kuwa kampuni haiombi tenda na haipati kazi kwa sababu ya msimamizi wa sasa hawezi.

Sasa watoto hawa wanaomba kujuakutoka kwenu namna gani wanaweza kupata haki yao kwa mujibu wa sheria,?

Naomba kuwasilisha

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom