Mimba za kuzimu

Mimba za kuzimu

Unachojua wewe ni makanisa na misikiti tu.

Tatizo linaanzia hapo.

A little knowledge is dangerous indeed. Utashi wako unaanzia na kuishia katika makanisa na misikiti.

I have been to Dharamsala.

Hujathibitisha kwamba mungu wako huyo yupo. Huwezi.

Kwa sababu hayupo.

Na dunia yako yote imejengeka katika uongo huo.

Ndiyo maana unaamini katika ujinga kama uchawi.
Umerudi pale pale kuwa wewe pekee upo kinyume na dunia nzima na wote ni wajinga, nilishaeleza huko juu kuwa mjanja ni wewe peke yako.
Na pengine nimepata faida katika mjadala wetu bwana mdogo maana nilikuwa nikisikia kuhusu wapagani ila leo nimethibitisha, tukiachana na sisi tuliokosa upeo kuamini uwepo wa Mungu.......wewe hua una imani yeyote unayoabudu au?
Nijuze mkuu nipate kuelewa vema watu wa aina yako wanakwenda vipi
 
Utasemaje mimi pekee?

Umezunguka nchi ngapi duniani mpaka leo useme mimi pekee?

Mimi mpagani?

Unafahamu maana ya mpagani ni nini? Mpagani ni mtu mwenye imani fulani ya kidini. Mimi sina imani ya kidini. Wewe mwenye kuamini mungu yupo uko karibu na mpagani kuliko mimi nisiyeamini kuwapo kwa mungu wala imani yoyote ya dini.

Utaniitaje mimi mpagani?

Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Au unaamini hadithi ya uongo isiyothibitishika tu?
 
Utasemaje mimi pekee?

Umezunguka nchi ngapi duniani mpaka leo useme mimi pekee?

Mimi mpagani?

Unafahamu maana ya mpagani ni nini? Moagani ni mtu mwenye imani fulani ya kidini. Mimi sina imani ya kidini. Wewe mwenye kuamini mungu yupo uko karibu na moagani kuliko mimi nisiyeamini kuwapo kwa mungu.

Utaniitaje mimi mpagani?

Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaweza kuthibitisha kwamba mungu yupo?

Au unaamini hadithi ya uongo isiyothibitishika tu?
Naamini uwepo wa Mungu

Huamini uwepo wa Mungu

Uthibitisho wa muumini ni katika vitabu vya dini

Kwako vitabu vya dini ni hadithi za kutunga

Nini hapa tunaweza tukaafikiana? Tusiwe kama watoto wanaotupiana lugha chafu humu kila leo........kila mtu ashike alichonacho maisha yaendelee
 
Ukishakileta JF, hujashika ulichonacho.

Umekileta kichambuliwe.

Nimekutaka uthibitishe uwepo wa mungu.

Umeshindwa.

Unaamini katika kitu ambacho huwezi kukithibitisha.

Huna tofauti na mtoto anayeamini katika hadithi ya kufikirika kwamba baba yake anaweza kuipiga dunia nzima.

Kiukweli imani ya mungu kwa watu wazima ni imani ile ile ya huyu mtoto iliyovikwa nguo za kiutu uzima tu.

Wishful thinking.

Hakuna mungu. Amka. Acha imani za kijinga hizo za kuwapo kwa mungu na uchawi.
 
Ah! Sioni ni nini tunajadili ila kukushauri tu ni kwamba walioleta dini walizipigania na bado wanazipigania, hivyo wewe nawe ukitaka tuache ujinga huu usijibane nyuma ya keyboard ingia mtaani komboa watu waeleze sera zako kuwa hakuna mungu......naam hutakosa walio wako
 
Unajuaje kwamba una uwezo wa kunishauri mimi?

Na kama huoni ni nini tunajadili, utawezaje kunishauri?

Na kama hujajibu swali langu la kuthibitusha kuwepo kwa mungu unawezaje kupata kifua cha kunipa ushauri?

Unajuaje kwamba siko mtaani?
 
Utoto mtupu na kila ninavyojibu maswali ya kitoto yanazidi katika ligi hii ya kitoto
 
Ujumbe murua kwa wanao mkufuru Mungu kwani kwa kila jambo unapaswa kumwona Mungu akusaidie sasa unakuta kila kukicha dada zetu miguu na njia kwa waganga, huko akiambia nipe p.... au t... GO hawezi kataa mwisho wa siku wanaambulia magonjwa nk
Waganga mbona wanawakamua sana hao wadada...Tatizo kubwa watu hawapati mafundisho yakutosha kwenye Imani kuhusu Mungu wao ndio maana wanakwenda kwa waganga...nakama MTU umefundishwa vzr habari za MUNGU wakweli Mganga au MTU anaekwenda kwa Mganga unampuuza sana
 
Ndg mshana jr;
Tahadhari yako nimeifurahia sana, ila unapowaambia watu kuwa wajihadhari na hao wanaojiita manabii sijakuelewa. Ina maana kuwa tusiwakubali tena hao manabii?? Tusipo wakubali manabii tuwaendee wanani?? Sitetei nabii yeyote kwani ninavyo amini mimi ni kwamba, kama kweli huyo ni mtumishi wa Mungu aliye hai, Mungu mwenyewe atamtetea tu. Mungu hatazuiwa na mshana jr au yeyote.
Sisemi kuwa manabii wote ni waongo, ila Neno la Mungu linasema; Kwa matunda yao, mtawatambua. Kwa maneno mengine ni kuwa, tunaweza kuwatofautisha tu kwa matunda yao. Mungu wetu hadhihakiwi, hivyo hawezi kumdhihaki mtu yeyote. Yaani mama amemwomba mtoto, tena kwa uchungu mwingi, miaka 38, halafu Mungu wetu ambaye tunajua jina lake ni UPENDO. amdhihaki, abebe mimba miezi 9 halafu aje kujifungua hizo sura ulizoweka kwenye picha zako. HAPANA. Nasema, haitotokea kamwe.
Kama umemwendea nabii wa kweli, atamwomba Mungu kwa uchungu naye Mungu atakupa mtoto. Ombeni watoto kwa manabii wa kweli. Ishara; Nabii wa kweli hataomba fedha wala zawadi yeyote kwako. Ameambiwa kuwa, ulipewa bure, toa bure. Nimpe pesa kwani yeye ndiye ananipa huyo mtoto??
Mganga, wa kienyeji, hana uwezo wowote wa kukupa mtoto. Akikupa, labda mama ulilala naye na mbegu yake ikarutubisha yai lako. Akikupa mtoto kwa dawa, umempata huyo mshana jr aliyekuambia. Muogope huyo mganga kwani anauwezo na huyo mtoto kwani ni wake sio wako. Akimtaka saa yeyote kama hukutimiza sharti lake anamtwaa. Ni wake maisha yote.
Ingawa umeandika mengi na maswali kumuuliza Mshana Jr mimi nataka nikwambie jambo 1 kuhusu hawa wahuni wanaopenda kujiita Manabii hawa ni matapeli wakawaida kabisa....sasa kumetokea huo ujinga has a wanawake wanaibiwa sana wengi wao badala yakwenda kwa Waganga wanajificha kwenye KOTI la kutabiriwa hii ni style ya uaGUZI....Ninachofahamu khs Huduma ya unabii nikwamba NABII kabla hajajakukuambia kwamba MUNGU amenionyesha kitu flan kwako kitatokea nini kawaida anaanza MUNGU mwenyewe kukuonyesha the NABII akija kukwambia nikama cornfimation tu lkn watu wengi hawajui hii mambo
 
mimi nimewashuhudia hawa watoto wa kwa waganga wengi sana na wengine ni ndugu zangu kabisa.. ukweli ni kwamba sijawahi kuona tatizo lolote kwao...watoto hawa kwa kihehe huitwa vana vasuke... yaani watoto wa kuobwa. watoto hawa pindi wanapozaliwa huwa na masharti ulani, kwa chochote unachotaka kumfanyia inabidi uwasiliane na mganga.. ili uepukane na masharti yote haya basi itabidi umkomboe huyo mtoto.. ukishamkomboa basi huyo mtoto atakuwa na hatakuwa na shida yoyote.

kabla ya kuwajua hawa watu nilikuwa najiuliza mwisho wake huwa unakuwaje... baadaye nikajuwa maana pia nina ndugu zangu wenye watoto hawa, mpaka kesho sijawahi kusikia kitu chochote cha ajabu, nimecheza nao na kukua nao. wanakuwa na kufa kama wengine, wanakula kama wengine, kifupi hawana tofauti ya watoto wengine.

hayo ni yale niliyoyashuhudia kwa watoto wa kuobwa kwa waganga... lakini pia niliwahi kumshuhudia mama mmoja ambaye amewahi kuomba mtoto kwenye kanisa lake na madai yake ni kwamba alimuomba mungu. mama huyu alikuwa na mtoto mmoja na alipata matatizo ya Kizazi chake hivyo uwezo wa kuzaa tena hakuwa nao kabisa....baada ya kwenda kwenye maombi huyu mama alivimba tumbo yeye akadai mimba na akawa anaenda kliniki nako wakasema ni mimba... akailea hiyo mimba yake kwa bidii.. baada ya miezi tisa kufika ile kwenda hospitali kujifungua... ikabidi afanyiwe upasuaji.. baada ya upasuaji wakakuta minyama tu ambayo haikuwa na dalili yoyote kuwa kilikuwa kiumbe zaidi ilikuwa kama uvimbe hivi.
Inawezekana mtoto asipate shida ktk ukuaji sababu Wazazi au walezi wanafata mashart lkn atakaokuwa mkubwa kwenye maisha yake lazima kuna baadhi ya vitu havitamwendea sawa kama wanadamu wengine...sababu ya Asili yakuzaliwa kwake huo ulimwengu aliotokea unakuwa na uHALALI nae so aidha inawezakuwa Shule....Uchumi...wake....au...ndoa kupata watt nk Hawezi kuwa kamili
 
Jamii forum ni zaidi ya uijuavyo aise,ila ndugu zangu naomba kujua ,kuna vifo vingi sana vinatokea sasa hivi vya watu kudondoka bafuni na kufariki katk kupita pita kuna stori kuwa hivyo ni vifo vya kishirikina@ naombeni mtujuze wadau
Kuna kitu wachawi wanaiita hukumu ya Kifo hii ukifanyiwa ndio unakufa kwenye mazingira hayo unayosema
 
Ingawa umeandika mengi na maswali kumuuliza Mshana Jr mimi nataka nikwambie jambo 1 kuhusu hawa wahuni wanaopenda kujiita Manabii hawa ni matapeli wakawaida kabisa....sasa kumetokea huo ujinga has a wanawake wanaibiwa sana wengi wao badala yakwenda kwa Waganga wanajificha kwenye KOTI la kutabiriwa hii ni style ya uaGUZI....Ninachofahamu khs Huduma ya unabii nikwamba NABII kabla hajajakukuambia kwamba MUNGU amenionyesha kitu flan kwako kitatokea nini kawaida anaanza MUNGU mwenyewe kukuonyesha the NABII akija kukwambia nikama cornfimation tu lkn watu wengi hawajui hii mambo

Kwa sababu unazo zijua weye, hukutaka kuusoma vizuri uzi wangu ukalinganisha na wa mshana jr. Nimemuuliza, ina maana sasa tusiwasikilize tena manabii?? Nawe pia nakuuliza, hakuna tena manabii??
Kwamba wapo matapeli sijakuuliza hilo. Swali langu ni kuwa; Je hakuna tena manabii duniani?? Miye naamini kuwa wapo manabii wa Mungu bado duniani. Lakini ukitaka kutapeliwa utatapeliwa tu. Kama mtu atasimama aseme kuwa kati yetu wawili tu kuna mchawi na miye sio mchawi wala siujui uchawi, hakika ntajua kuwa huyu ni mwongo. Na kummaliza, namwambia afanye atakalo na huyo mungu wake.
Nilisema; Neno la Mungu wangu linasema; Kwa matunda yao mtawatambua. Sio kwa akili zetu wala kwa kusema hawapo bali kwa matunda yao.
Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu huku unadai fedha mbele kabla hujaniombea nifanikiwe. Niombee, nikifanikiwa nakuja toa shukrani. Mkumbuke Naaman wa biblia, alitoa zawadi kwanza au baada ya kupona?? Mambo ingine twajitakia wenyewe.
Kama mwanamke unaenda kuombewa mtoto, unaambiwa funga mlango, vua nguo ubaki uchi, haya lala chini, panua miguu nakuwekea dawa, funga macho usiangalie dawa..... wewe ni mjinga na hao wapo wengi.
 
Asant jichawi,ila nasikia hata ukipona hakuna dawa ht ukienda hospital hutapona labda kwa maombi tu...
 
Utoto mtupu na kila ninavyojibu maswali ya kitoto yanazidi katika ligi hii ya kitoto
Kama ya kitoto ungeweza kiyajibu kirahisi.

Hujaweza kuyajibu, hayawezi kuwa ya kitoto hivyo.

Thibitisha mungu yupo.
 
Mshana jr labda nikwambie kitu kimoja ni kweli kuna watoto wa kuzimu na wengine wa kawaida tu ambao mwanamke anakuwa kizazi chake kimechukuliwa kishirikina hivyo kukaa bila kupata mtoto kwa mda mrefu na hapo ndio anapoanza kutafuta mtoto kwa nguvu kupitia kwa waganga na nk sasa mtu aliyechukuliwa kizazi kishirikina kuna namna ya kumrudushia hasa pale sie waganga tunapojua kuwa kizazi hiki kimechukuliwa kishirikina ambapo matibabu yake nitayaelezea kama kutakuwa na mwenye swali ktk hili .Sasa mganga anajuaje kuwa huyu hawezi kupata mtotokabisa hutoka na mwenye Shida kwenda sehemu ambayo ni tambalale hapo iwe mwenye Shida ni me au ke hucholewa fuara na kutakiwa kukojoa mkojo kisha humwaga dawa ktk lile duara baada ya hapo mganga huita majini wa eneo lile kulingana na mtawala wa siku hiyo kwa wale wenzangu watakuwa wanaelewa nini mana ya mtawala baada ya hapo huondoka kisha kesho Yake hurudi tena ile sehemu sasa kama mtu ni mgumba na hawezi kupata mtoto utakuta picha ya mtoto haijaungana ila kama ni wa kupata mtoto utakuta picha imeungana basi Huyo anaweza kupata mtoto ila sasa kuna wengine ambao baada ya kuona hawezi kupata mtoto na yy kutaka apate ndio pale mwanamke anapopewa mtoto wa kuzimu au kutakiwa kutoa kafara ya kifaranga cha kuku kwa kwenda kukizika kaburini hapo akishamaliza hutakiwa amtafute mama mjamzito kisha mimba halisihuamia kwa Yule aliyeomba mtoto na ile fek huamia kwa mjamzito hapo ndio unakuta wengine wanazaa vitu vya ajabu
 
WADAU,
Nimesoma michango ya wengi sana na nimejifunza mengi. Japo mimi si MTAALAM kama Mshana Jr au Jichawi lakn natoa yangu ili mjifunze ktk huu uzi.

1. KANUNI.
Ukitaka Kuyajua Ya Shetani Basi Mwabudu Mungu Usiwe Vuguvugu.

2. Ukitaka Kuyajua Ya Mungu Basi Mwabudu Shetani Usiwe Vuguvugu.

MFANO.
Huwezi Kuwa Shabiki Wakweli Wa Simba Usiwajue Wachezaje Wa Yanga Na Vivyo Hivyo Huwezi Kuwa Shabiki Wa Yanga Usiwajue Wachezaji Wa Simba.

Ukishasimama Ufalme Mmoja Wa Kiroho Yani Ukaamua Kuegemea Kwa Mungu Au Shetani, Basi Utayajua Ya Upande Uliopo Na Upande Wa Adui Yako.

Kinachotufanya Wengi Tushindwe Kuwatofautisha Manabii Wa Ukweli Dhidi Ya Wale W Uongo Ni Kwasababu Tupo Vuguvugu Yani Sisi Si Moto Wala Baridi. Hapa Ndipo Hawa Manabii Wa Uongo Wanapotupiga Bao, Lakn Kama Tutasimama Thabiti Ktk Ufalme Mmoja, Basi Kila Kitu Kitakuwa Wazi Kwetu.

Mshana Jr na Jichawi Wanayajua Haya Coz Walishachezea Moja Kati Ya Hizi Club Na Pengine Walikuwa 1st Eleven Ndio Maana Wao Kuyajua Haya Imekuwa Rahisi Kwao.

Mungu Awatie Nguvu Mtupe Shule Ya Kutosha Japo Hamtoi Vyeti hahahahahahah.
 
yaa ni lazima kama ilivyolazima kudumu kwenye maombi muda wote pindi unapotaka msaada toka kwa MUNGU

mshana jr lazima ujue kila pande zina mafanikio na hasara zake.... ukihukumu moja kwa moja sijui waganga wabaya huko sahihi kwasababu babu zetu waliishi kwa njia hizo na walifanikiwa kwa njia hizo... hata waganga tunaowasema haimaanishi wote ni mashetani kama wewe unavyotaka kuwaaminisha umma, makanisani tumeshuhudia sio kesi moja ni nyingi watu wakipata kile ambacho hawakutarajia,

kwahiyo hata hao waganga wengine ni mashetani na wengine ni uwezo wanao waliopewa na MUNGU
Ungerejea hiyo post vizuri nafikiri ungemuelewa vyema sana mtoa uzi.
Muhusika kagusa wanaojiita manabii na si waganga japo waganga pia wapo waovu.
Pia kasema wapo wanaotumia mitishamba na wala hawahusishi na imani ya kishirikina.

Mwisho wa cku akamaliza akisema, JIHADHARINI, akiwa na maana tuwe makini na pia tuchukue tahadhari maana wengine si wema na hawajatumwa na Mungu kama tuzanivyo.
 
WADAU,
Nimesoma michango ya wengi sana na nimejifunza mengi. Japo mimi si MTAALAM kama Mshana Jr au Jichawi lakn natoa yangu ili mjifunze ktk huu uzi.

1. KANUNI.
Ukitaka Kuyajua Ya Shetani Basi Mwabudu Mungu Usiwe Vuguvugu.

2. Ukitaka Kuyajua Ya Mungu Basi Mwabudu Shetani Usiwe Vuguvugu.

MFANO.
Huwezi Kuwa Shabiki Wakweli Wa Simba Usiwajue Wachezaje Wa Yanga Na Vivyo Hivyo Huwezi Kuwa Shabiki Wa Yanga Usiwajue Wachezaji Wa Simba.

Ukishasimama Ufalme Mmoja Wa Kiroho Yani Ukaamua Kuegemea Kwa Mungu Au Shetani, Basi Utayajua Ya Upande Uliopo Na Upande Wa Adui Yako.

Kinachotufanya Wengi Tushindwe Kuwatofautisha Manabii Wa Ukweli Dhidi Ya Wale W Uongo Ni Kwasababu Tupo Vuguvugu Yani Sisi Si Moto Wala Baridi. Hapa Ndipo Hawa Manabii Wa Uongo Wanapotupiga Bao, Lakn Kama Tutasimama Thabiti Ktk Ufalme Mmoja, Basi Kila Kitu Kitakuwa Wazi Kwetu.

Mshana Jr na Jichawi Wanayajua Haya Coz Walishachezea Moja Kati Ya Hizi Club Na Pengine Walikuwa 1st Eleven Ndio Maana Wao Kuyajua Haya Imekuwa Rahisi Kwao.

Mungu Awatie Nguvu Mtupe Shule Ya Kutosha Japo Hamtoi Vyeti hahahahahahah.
Nimeupenda huu uchambuzi wako Prosper asante sana
 
Back
Top Bottom