Akhsante mkuu
Unayosema ni mambo makubwa sana na jamii inaangamia pasipo kujua kwamba milki za giza zipo kazini, watazameni kwa macho mawili watoto wanaozaliwa na miujiza......nasisitiza watazameni na ukuaji wao!
Nikirudi kwa viongozi wa dini wanaopotosha kama ulivyoeleza...ni hakika.....kipindi kirefu kilichopita walinitembelea viongozi fulani wa dini fulani na kuniambia kuwa ili waaminike katika ibada inatakiwa kipawa hivyo niwasaidie.
Niliingia kwa wakuu na nifanya maagano kwa niaba ya viongozi wale wa dini na nikawapatia jinn mmoja wa kuogofya na mwenye nguvu na ubabe hata kwa majini wenzake, nikawapatia watu wale na kwenda kuongoza ibada kama kawaida......ila kila walipokuwa wakiombea watu jinn yule ndiye aliyekuwa akijibu maombi na sio Mungu.
KIVIPI?
Wenye mapepo walianguka wenyewe kwa kumuogopa jinn yule wa kifalme, vifungo vya kichawi alivifungua yeye, majini wabaya wa waumini walikimbia wenyewe kwa kumuogopa huyo bwana na nyumba ya ibada ikasifika kiasi kwamba wale viongozi wakanawiri.
Je, ni haki? Mungu anapenda kuona nafasi yake inafanyiwa dhihaka?
Niishie hapa.