Mimba ya mke wangu inanitesa

Mimba ya mke wangu inanitesa

Jina lako tu zimwimtu, avatar yenyewe utata mtutu, umeweka picha ya max...
haya panda miwa sasa nyumbani kwako
 
Last edited by a moderator:
hujawahi kuamshwa usiku wamanane unaambiwa "NASKIAJOTO NIPEPEE"muhusika sasa anaepepelewa katoa jicho kama nini olewako speed ipunguee,utakiona utaambiwa unamnyanyasa,mara humpendi...makasheshe kibao

Nilishawahi kuamshwa saa tisa usiku nikanunue chips kavu...thanks God kulikua na bar inayokesha karibu.......Mimba kiboko!:bange:

asante ndugu, navumilia tu huku nikidhani yataisha. itaniuma sana kama hali hii ikiendelea hata baada ya kujifungua..
zimwimtu,
Vumilia ndugu, mimba ndivyo zilivyo, kama unavyosoma kwa wazoefu hapo juu! Mie kuna siku niliagizwa mishkaki, bahati mbaya hapo ninaponunua siku zote nikakuta imeisha na nisaa 5.30 usiku, nikaamua kurudi maskani mikono mitupu. Nikakuta mtu yupo getini anasubiri, macho makavuuuuuuuuu, na haongei kitu! Ilibidi nirudi kwenda kuisaka, kuja kurudi tayari inasoma saa 7 usiku, kwa sababu niliifuata mbali.
Please nakuomba umvumilie kwa hiyo miezi mitatu iliyosalia
 
Last edited by a moderator:
niwe mkweli kwako mimba inaleta hasira za haraka na kutamani vitu vya ajabuajabu na maamuzi ya kijinga kwa baadhi ya wanawake,jaribu kumuelewa kwa kipindi hiki na usitegemee mapenzi makubwa kwani anakuwa na uchovu .jitahidi sana kuwahi na kama umeona ana hasira na maamuzi ya ajabu jitahidi kutokumtega na chochote.kila la kheri mweshimiwa ukipata mtoto utushirikishe tukupe hongera.
 
zimwimtu,
Vumilia ndugu, mimba ndivyo zilivyo, kama unavyosoma kwa wazoefu hapo juu! Mie kuna siku niliagizwa mishkaki, bahati mbaya hapo ninaponunua siku zote nikakuta imeisha na nisaa 5.30 usiku, nikaamua kurudi maskani mikono mitupu. Nikakuta mtu yupo getini anasubiri, macho makavuuuuuuuuu, na haongei kitu! Ilibidi nirudi kwenda kuisaka, kuja kurudi tayari inasoma saa 7 usiku, kwa sababu niliifuata mbali.
Please nakuomba umvumilie kwa hiyo miezi mitatu iliyosalia

haahaaaah..sikupatii picha mzee mzima ulivyofunga break kugeuza,sometimes nikikaa nikikumbuka huwa na cheka mwenyewe kama mwehu..sasa mie dogo anamika miwili mama hakumbuki hata moja
 
Teeh.... teh...!!!!!Pole yako ulitaka ukimpepea afumbe macho?,

mwenzangu we unaona raha tuuu.....kesho ofisini full kusinzoia kulala umelala mida imekwenda,bado haujatumwa akipendacho kukila asubuh hiyo..unaenda kazini sometimes umechelewa
 
Kuna jamaa alikurupushwa saa nane za usiku mkewe kamwambia anahitaji matango jamaa akabanwa kweli ikabidi akapige hodi kwa muuza matango kwa bahati nzuri akapewa!
Kuyaleta nyumbani akaambiwa ayakatekate kisha ampe akae nayo awe anayanusa maana anapenda harufu yake!
Chezeiya mimba wewe!

haaahaaaaaaahaaaa.....!!!
 
pole baba..

Vumilia baba,akishajifungua tu atabadilika.....
 
wadau naomba uzoefu wenu katika hili..

mke wangu ana mimba ya miez 6 sasa na ndo mimba yake ya kwanza. amepunguza mapenzi kwangu japo si saaana ila si kama zamani asiponiona atapiga simu weeee mpaka kero, siku hizi wala, nikichelewa nakuta keshalala wala hana habari na mim.

katika mimba yake hiyo ametokea kupanda kula miwa.. ebwana ikiksekana hakukaliki hom. huwa na kawaida ya kupitia miwa pale mwenge na kumpelekea kila siku. maana ukinunua mingi ukaweka kwenye frij hataki et iaisha utam (ilimradi visa tu)
sasa jana nilichelewwa kurudi kutoka job, kupita mwenge miwa hakuna, zunguka mpaka ubungo hakuna, ikabidi mwanawane kirud hom tu, kufika tu nikajitetea kuwa nilichelewa kurudi nikakosa miwa..,

weeee, aliporomosha matusi mpaka hasira, nikamwacha aongee tu maana nilimbembeleza anisamehe nitaitafta kesho maana ilikuwa saa nne tayari hakunielewa. mpaka akamwaga maji kitandani eti nisilale mpaka miwa ipatikane..,

basi nilizunguka mpaka saa 6 ndo nikaipata buguruni, hapo tuligonga hdi muuzaji keshalala nikidanganya nataka ya kutengenezea dawa.

jaman kuweni na huruma japo kidogo...., hivi baada ya mimba atabadilika kweli au ndo atabadilika mazima my wife wangu!!!...., naumia sana, kuna vituko kibao ila cha jana ndo kiboko...

nawasilisha.

Kwani hiyo mimba siyo yako?
 
Mkuu mbona wewe cha mtoto mimi nilikuwa naambiwa nisioge eti anapenda harufu yangu nisipooga, hawa viumbe wakiwa na mimba wanatukomoa sana we vumilia tu bado miezi mitatu.
 
Kawaida hata usiwe na shaka!! Ila miezi 6 bado anakuwa msumbufu?? Hiyo mara nyingi trimester ya kwanza(ile miezi mitatu ya kwanza).

Kaza uzi mzee hormones hizo!! Mie wa kwangu tunahesabu siku tu hapa,,,,, tunatanua njia kama Kenya mpaka siku ya uchungu!!!
 
pia miwa sio mizuri kwa mama mjamzito mtoto anazaliwa akiwa amekatikakati just ushauri tu.
 
Ha ha ha ..Mimi kuna wa jirani yangu yeye alikuwa anataka chipsi tena za mangi mtaa wa tatu, na ole wake
alete za mtu mwingine balaa...kumbe anazijua!

Mwisho wa reli alikuwa anaambiwa kila jioni aje na miguu ya kuku ya kukaanga na jamaa mwenyewe 'braza men"!!
anawaza namna atakavyopita Uswazi kwenye vigenge kununua!

ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha:heh::heh::heh::heh:
 
mwenzangu we unaona raha tuuu.....kesho ofisini full kusinzoia kulala umelala mida imekwenda,bado haujatumwa akipendacho kukila asubuh hiyo..unaenda kazini sometimes umechelewa

Usipime ndugu,
Mimba imenisotesha kinoma, nashukuru kajifungua salama, mwezi jana.
Cha kuchekesha zaidi, alikuwa hataki kusikia harufu ya dawa ya kung'arisha viatu (nyie mnaita kiwi). Kwa hiyo ilikuwa napiga kiwi asubuhi sana mjini, then naposhuka kwenye gari jioni navaa sandals na kuacha viatu kwenye gari ili harufu ya kiwi isisikike. We acha tu ndugu. Mimba zina vijimambo sana.
 
Inawezekana ni sababu ya mimba, japo amezidi kudeka. Kuwa mvumilivu ila mwerevu.
 
Hapo sio mimba tu inayomfanya afanye hivyo. Kuna lingine limejificha nyuma ya pazia.

Ni mimba tu kamanda, pole sana baba mtarajiwa zimwimtu. Mimi wife alikuwa anapenda nyama ya kuchoma yaani hata kipande kimoja mapenzi yanakuwa mazuri na malezi kama ya mtoto. Kuna siku aliniambia nimchukulie ila sikufanikiwa kupata maeneo ya jirani na sikuwa na usafiri binafsi na muda ulikuwa wa vibaka, nilijipeleka bila hitaji lake yaani alilia hadi ikabidi nitembee umbali wa KM 3 tena kwa staili ya kukimbia kidogo nilirudi nikakuta bado kilio kinaendelea ila baada ya kuona nyama alifurahi hadi akaninawisha miguu kwa upendo. Ushauri baada tu ya kujifungua atarudia hali yake ya kawaida hasa hamu ya kitu fulani inakata mara ila itamchukua miezi 3 hadi 6 kurudia ile hali ya awali uliyoizoea.
 
pia miwa sio mizuri kwa mama mjamzito mtoto anazaliwa akiwa amekatikakati just ushauri tu.

Siyo kweli.....huyu mama mtarajiwa anapenda miwa ili kumaintain sukari yake ya mwili kwani baadhi ya wamama wajawazito wanapata tatizo la sukari kupungua kutokana na matumizi ya mtoto...my wife alikuwa anatumia pipi au sukari kila akihisi huo upungufu.
 
wadau naomba uzoefu wenu katika hili..

mke wangu ana mimba ya miez 6 sasa na ndo mimba yake ya kwanza. amepunguza mapenzi kwangu japo si saaana ila si kama zamani asiponiona atapiga simu weeee mpaka kero, siku hizi wala, nikichelewa nakuta keshalala wala hana habari na mim.

katika mimba yake hiyo ametokea kupanda kula miwa.. ebwana ikiksekana hakukaliki hom. huwa na kawaida ya kupitia miwa pale mwenge na kumpelekea kila siku. maana ukinunua mingi ukaweka kwenye frij hataki et iaisha utam (ilimradi visa tu)
sasa jana nilichelewwa kurudi kutoka job, kupita mwenge miwa hakuna, zunguka mpaka ubungo hakuna, ikabidi mwanawane kirud hom tu, kufika tu nikajitetea kuwa nilichelewa kurudi nikakosa miwa..,

weeee, aliporomosha matusi mpaka hasira, nikamwacha aongee tu maana nilimbembeleza anisamehe nitaitafta kesho maana ilikuwa saa nne tayari hakunielewa. mpaka akamwaga maji kitandani eti nisilale mpaka miwa ipatikane..,

basi nilizunguka mpaka saa 6 ndo nikaipata buguruni, hapo tuligonga hdi muuzaji keshalala nikidanganya nataka ya kutengenezea dawa.

jaman kuweni na huruma japo kidogo...., hivi baada ya mimba atabadilika kweli au ndo atabadilika mazima my wife wangu!!!...., naumia sana, kuna vituko kibao ila cha jana ndo kiboko...

nawasilisha.

Acha mchezo na mimba!

Juzi nimeenda pokea mihogo stendi imetumwa kutoka dar, eti ya hapa haina ladha! mihogo ya elfu 5, inasafirishwa kwa elfu 10, unawasha gari unatembea 25km kuifuata!

Mimba zinatesa sana.
 
Back
Top Bottom