Mke wangu kawa chanzo cha kuvunjika kwa ndoa ya jirani yangu

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,720
100,079
Wakuu,

Naandikaga Uzi huu nikiwa nimefedheheka Sana, kuna depression naifeel kabisa kufuani mwangu maana hata jamii sasa inanitizama tofauti Sana.

NI HIVI,
Kuna binti mmoja hapa mtaani Ni shoga yake na wife wangu kaolewa mwaka Jana kwa harusi na Jamaa mmoja ni Ticha wa shule ya sekondari kajenga Hapa Hapa mtaani kwetu.

Kabla ya kuolewa na ticha,
Huyu binti Alishazalishwa mtoto mmoja wa kike na jamaa mmoja asiyejulikana, binti anasema jamaa alikua ni mchaga.

Kwa maelezo ya binti,
Ni kwamba uyo baba wa mtoto wake alienda South Africa kutafta maisha tangu 2015 alimuacha akiwa na mimba ya miez 8 na hajawai kurudi kabisa Wala Hawana mawasiliano yoyote na uyo mzazi mwenzie.

Na kweli Miaka yote 6 binti yupo Hapa mtaani anaishi TU kwa kujitegemea kwa deiwaka za kupika kwenye saiti mbalimbali za ujenzi, Yaan pakiwa mahali ujenzi unaendelea, ataomba kazi ya upishi kwa mafundi na kulipwa kwa kila sahani ya chakula.

Asipofanya huo upishi,
Basi atapiga vibarua vingine vya saidia fundi, kulima bustani, kukata majani ya ng'ombe, na shughuli nyngn Ndogo ndog za kuunga unga ili kupata kula.

Sometimes akikosa kabisa atakuja kwa wife amsaidie kazi mbili tatu ili mradi apate hata chakula Chake na mwanae na maisha yanasonga.

Akipata kazi za mbali,
atamuacha binti yake kwa wife siku mbili tatu ataenda mbali uko kufanya vibarua vyake, akirudi anamchukua binti yake na kuendelea na maisha yake.

Hata huyu mme aliemuoa bila shaka walikutana kwenye hivyo vibarua maana hata nyumba ya uyo ticha alojenga, yule binti kawapikia sana mafundi wake.

Kuna kipindi Nilikua namkuta sana pale anapika maana ticha aliniungisha Sana material za ujenzi kipind chote mpaka anamaliza nyumba yake. Nilikua nafanya delivery.

Sijui nini kiliendelea hapo katikati,
Ila nakumbuka mwaka jana binti alituletea kadi ya mwaliko wa harusi, na Kwasababu ya ukaribu wangu na uyo ticha, afu ukaribu wa wife na uyo binti. Tulishauriana tuwasapoti vizur.

Mimi na wife Tulichangia kadi ya kamati kabisa, na wife Aliparticipate sana kwenye kamati mpaka harusi nzima inaisha. Mi nilikuwa bize sana, sema nilihudhuria tU siku ya harusi kama wengine.

Na ticha rasmi akamhamishia binti kwenye nyumba yake mpya na wakaanza kuishi Kama MKE na mme.

Nasisi tukawa Kama family frendi na majiran zao wa karibu sana.

Sasa Always simu ya wife wangu huwa iko under my surveillance 24/7.

Sio kwenye calls, sms hadi WhatsApp. (Hapa Msinipopoe kwann namspy wife, Kila abiria achunge mzigo wake )

sasa Hivi karibuni
Nilikuja gundua Simu ya wife wangu karibu wiki nzima Kuna namba ngeni huwa Anaongea nayo Sana, tena muda ambao ndiyo nakua nmeenda kazini (saa 2asbh- saa 5 asbh).

Wikend ilopita asbh
wife katoka church Ikabidi kumuuliza.

"Huwa Ni Nani uyu namba yake inaishia na 23 mnawasiliana sana nnapokua nmeenda kazini na dkk zote hizi mnakuaga mnaongea nini"

Wife akanambia sio yeye anayepiga Hii namba, ni shoga ake mama D ndo huwa anaazima Simu Yake kuwasiliana.

Nikaomba namba Yake mama D na kumpgia kuwa aje nyumban kwangu mara Moja namhitaji. Kweli akaja.

Nikamuita pemben na kumuuliza kuhusu Iyo namba, akanambia uyo ni mzazi mwenzie yaani baba D. Nikamuuliza una uhakika? akasema ndio.

Nikamwambia Piga Hapa Hapa kwa simu ya wife muongee kdg nimskie, kweli akampigia jamaa ikiwa loudspika wakaongea mawili matatu ikawa imeisha hivyo, nikamruhusu aondoke.

Ila Sasa baada ya kuondoka nikabaki najiuliza maswali.

- Kwanini atumie Simu ya wife na wakati Simu yake anayo?

- Kama ni kuishiwa vocha labda siku Moja, kwann ni wiki nzima mfululizo?

- Kuna nini anaficha mpaka aongee na mzazi mwenzie kwa Siri namna Hii?

- Usikute anamcheat ticha kwa mzazi mwenzie afu dalali mkuu Ni wife wangu?

- Hivi ticha akija kujua Hii kitu atanichukuliaje Mimi na familia yangu?

Anyway,
Ikabidi Kumuita Tena binti
na kweli akarudi na nikamuuliza maswali yote Hapo juu.

Akajitetea kwamba
" Baba D mwezi wa 6 alinipigia anasema namba yangu kaipata facebook na ndo amerud toka South Africa anataka tuoane ili tushirikiane kumlea D.

Nikamwambia nishaolewa tayari akaelewa. Baadae mme wangu akagundua tunawasiliana wakajibizana Sana kwenye Simu na kunambia niifute namba yake na kuiblock kabisa.

"Kwaiyo Ndo nikawa nawasiliana nae kutumia Simu ya mama G, ila ni kuhusu maendeleo ya mtoto wetu na sio mambo ya mapenzi na nilifanya hivyo ili nisimkwaze mme wangu. Nisamehe sana Kama nmekukosea baba G"

Nikamwambia,
"Hujanikosea Mimi Bali umemkosea huyo mmeo, Hiki unachofanya ni uhuni na utovu wa nidham kwa mmeo.

Heshimu kauli ya mmeo. Kama jamaa anataka kumuona au kuongea na mwanae, mpeleke mtoto kwa Bibi yake jamaa akaongee nae uko uko na sio hiki unachokifanya kupitia mgongo wa mke wangu".

Akasema sawa kanielewa, tukaagana na akaondoka.

Nikarud kwa wife na kumwambia
"Iwe mwanzo na mwisho kurudia hiki ulichokifanya, sitaki familia yangu iwe chanzo cha migogoro kwenye ndoa za Watu."

Wife Akasema "sawa nmekuelewa" ikaisha hivyo.

Sasa Jana asubuhi nikiwa kazini nikapigiwa simu na wife niende nyumban kuna Tatizo, nikamwambia nitakuja. Sijakaa sawa mwenyekiti wa mtaa nae ananipigia niende nyumban kuna matatizo, nikajua this is serious.

Nikaweka mambo yangu sawa, nikaenda.

Nmefika home nakuta watu hawapo, naambiwa wako kwa mwenyekiti,

Sio mbali Sana, nikaenda tu kwa mguu.

Nimefika kwa mwenyekiti namkuta wife, binti, yule ticha na jamaa mmoja na mwanamke mmoja wako wanaendelea kutoa maelezo mmoja baada ya mwingine nami nikaketi nikasikiliza.

Kwa maelezo ya pale,
Inaonekana Binti alikwenda kukutana na mzazi mwenzie mazingira ya nyumban kwangu kwa ajili ya maongezi na kumuona mtoto.

Na hiyo jana ilkua ni Mara yao ya 3 jamaa anafika pale wanakutana na kuongea.

But this time
Mchaga alikuja na dada yake lengo bi kumshawishi binti warudiane wakaishi wote, iliposhindikana baada ya binti kumueleza kwamba keshaolewa na hawezi kumuacha mme wake(ticha).

Basi mchaga na dada yake yake wakawa wanalazimisha waondoke na mtoto wao, na hapo hapo ndipo mzozo zaidi ukaibuka na kupelekea binti na dada yake mchaga wakaanza rushiana Maneno, matusi Kisha kupigana na kujaza watu.

Mchaga, wife na baadhi ya waliofika wakawa wanaamulia ugomvi ule.

Sasa Mzozo ulivyokua mkali zaidi,
ticha kapigiwa Simu na majiran na kufika pale. katika majibizano ya hapa na pale.

Ticha na Mchaga nao wakaanza kupigana ngumi na kupelekea kujaza watu zaidi Hadi mwenyekiti wa mtaa kuitwa na kufika pale, kisha kuwaamulia na kanipigia Simu Mimi niende kwake.

Kwa maelezo ya ticha,
Ni kwamba lawama zote anazielekeza kwa MKE wangu maana ndio kiunganishi kikuu na chanzo cha ugomvi wote ni yeye kuwa daraja la kuwakutanisha na wale jamaa.

Ticha Anasema kuna siku alisikia kwamba Huwa wanakutana pale kwangu na kumfata kumuuliza MKE wangu UKWELI wa habari hizo, ila MKE wang alikana kata kata hizo habari, nae kwa kumuheshimu akapotezea.

Leo mchaga anasema mwenyewe mara ya 3 wanakutania pale kwangu. Ameumia na Amejiskia vibaya Sana.

Ticha akahitimisha kwa kusema kua alishamuonya Sana MKE wake ila amekaidi uku akiendelea na nyendo zake za Siri na mzazi mwenzie.

Ni wazi kabisa MKE wake bado ana mapenz na mzazi mwenzie, hivyo hawez lazimisha kuwa nae tena na amemuachia rasmi mchaga wakaishi wote, mchaga akakubali ila binti kakataa uku akilia na kusema bado anamhitaji mme wake. Ticha akaondoka.

Kiukweli ticha baada ya kuondoka pale nilijihisi hasira sana kila nikimuangalia wife anavyojieleza vitu having mashiko, nikaona kama nikiendelea kukaa pale kumsikikiza naweza mzaba makofi mbele ya mwenyekiti afu iwe fedhea tena.
Ni Bora niondoke pale kuepusha Shari.

Nikamuaga Mwenykiti kuwa natoka Mara moja, pale nmeacha milango ya Gari wazi kuna documents muhimu ila sikawii Sana, nikaenda kuwasha gari na kuondoka Moja kwa moja mpaka dukan kwangu nikaingia stoo nikajifungia na kutuliza KICHWA mpaka muda wa kufunga alipofika.

Jioni nimefika nyumbani
Namkuta yule binti na mwanae wakiwa na wife seblen wanaangalia TV.

Sikuwasemesha nikapitiliza moja kwa Moja mpaka dining kuchukua maji baridi ya kunywa na kumfata shemej yangu jikoni (mdogo wake na wife) na kumuuliza kuhusu yule binti na mwanae wamefata Nini hapa.

Akasema
"Ticha kampiga na kumfukuza na begi lake Moja kwa Moja, Na Ndo kaja hapa kwa dada analia, wako seblen wanajadiliana wafanyeje"
nikasema "sawa" nikapitiliza mpaka chumban kwangu kulala, nimefumba macho hata usingizi hauji maana nna hasira sana na wife afu nawaza sana ticha ananichukuliaje kwa kuamini familia yangu kuhusika kushiriki kumvunjia ndoa yake.

Haukupita muda Sana wife nae akaja kulala, Nikamwamsha na kumwambia
"Nakupa siku ya kesho tu,
uyo binti sitaki kumuona hapa,
Fanya arudi kwa mume wake na warudiane haraka sana."

akasema
"Anarudije sasa na mme wake mkorofi kampiga na kumtupia begi lake nje"

Nikamwambia
"Atarudije au watarudianaje Hilo mimi Halinihusu, nnachojua wee Ndo chanzo Cha yote. Ikishindikana wao kurudiana na wewe nikirudi jioni nisikukute, uende kwenu."
Hakujibu chochote, Basi nikalala zangu

Leo alfajir Kama kawaida nmekuja dukan kwangu, kwenye saa 3 nmempigia shemej yangu (mdg wake na wife) kumuuliza Kama binti bado yupo nyumban akanambia kwamba wameondoka na wife kwenda kwenye jumuia kanisani.

Kiukweli hii naiona Kama ni dharau kubwa sana kwa maelekezo niliyokwishampa tayar khs kumrudisha uyu binti na ndoa yake kwa mumewe.

Nimedhamiria Kama kweli nikirudi jion na kumkuta binti nyumban kwangu, itabidi waondoke wote maana Itakua inaonekana kama nmeoa wake wawili.

MKE wangu ntamrudisha kwao, kama wakiamua wakaishi wote uko kwao na shoga yake sawa TU itakua juu yao.

Siwezi beba lawama ya kuvunja ndoa ya watu Kisha MKE wa mtu aliyefukuzwa akaishi kwangu.

Wakuu,
Sijui Kama nitakua nmekosea sana kwa maamuzi haya, nmefikira Sana hiki suala na akili yangu imefikia hapo.

Kama Kuna la ziada kunishauri nawakaribishen wakuu
 
Wakuu,
Naandikaga Uzi huu nikiwa nmefedheheka Sana, kuna depression naifeel kabisa kufuani mwangu maana hata jamii sasa inanitizama tofauti Sana.

Mama D akili hana wallah

Unachwa na mimba unaolewa halafu aliyekuacha anakuja kukusababisha uachwe tena unakubali😃😃😃

Wanaume mkiwa mnatafuta wake za kuoa mnaangaliaga nini?? Heshima, akili na upendo au mnaangalia yale makelio😎😎😎


Halafu baba G DeepPond ongea na mama D utayajua mengi ya mama G🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️
 
Mke wako jembe sana. Umewekeza mno kwa michepuko ukasahau kujenga nidhamu ndani ya ndoa yako. Mwanakulitaka mwanakulipata, mwanakulitafuta mwanakulipewa. Mwanakulitikita mwanakulitokota. Hamia kwa mama J
 
Mama D akili hana wallah

Unachwa na mimba unaolewa halafu aliyekuacha anakuja kukusababisha uachwe tena unakubali😃😃😃

Wanaume mkiwa mnatafuta wake za kuoa mnaangaliaga nini?? Heshima, akili na upendo au mnaangalia yale makelio😎😎😎


Halafu baba G DeepPond ongea na mama D utayajua mengi ya mama G🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️🚶‍♀️
Ni wewe kabisa huyuu😆
 
Mama D akili hana wallah

Unachwa na mimba unaolewa halafu aliyekuacha anakuja kukusababisha uachwe tena unakubali

Wanaume mkiwa mnatafuta wake za kuoa mnaangaliaga nini?? Heshima, akili na upendo au mnaangalia yale makelio


Halafu baba G DeepPond ongea na mama D utayajua mengi ya mama G
Note taken
 
I feel your pain, tuliza akili mkuu, Ila amini mkeo nae Ana makando kando yake mengi tu. Hawezi kuwa kuwadi bila yeye kukuwadiwa. Pia inaonesha huna sauti kwake amekumeza.

Mwendee ticha mweleze ukweli jinsi unavyoumia. Mwombe msamaha, Ila mkeo mrudishe nyumbani kwa muda, ili kuweka sawa taswira ya jamii kuwa umekwazika na tabia ya mkeo.

Pole Sana, ndo ndoa hizo mkuu
 
Binadamu bhana,kweli tuna vichwa ngumu...,kwann uwasiliane na MTU ambaye hakukupa thamani...ivi wanajua maana ya ex kweli? Inaumiza sana....kiukweli masingle mom tuacheni tu hata msituoe...tumekubuhu..khaa
Utasikia si mwanae !!😂😂😂 Wanawake Wana matatizo jamaa kakukimbia kanuona choko siku mbili tatu amaenza kutunzwa na jamaa na kupewa thamani kijana wa ovyo anakutaka Tena nawe unamfuata
 
Back
Top Bottom