Niliapa kuyafuta machozi ya mke wangu mpaka naiaga dunia

mbagokizega

Senior Member
Oct 22, 2016
111
297
Nawasalimia kwa upendo.

Ninaomba nitoe ushuhuda ambao kupitia siku hiyo niliweka nadhiri ya kuyafuta machozi ya mke wangu na kumfanya ajivunie mimi kuwa mumewe pia ajifaharishe na ndoa hii.

Wakuu tar 1/6/2013 nilifunga ndoa nyumbani kwetu Tanga katika kijiji cha Mashewa Korogwe vijijini na baadaye kurejea Dar kuendelea na maisha na mke wangu ambaye mi naye makazi yetu ni hapa jijini kiukweli mi natokea katika familia ya kawaida ya wakulima hivyo harusi yetu ilikuwa ya hadhi ya chini, iliniumiza kumuona mke wangu akiny'ong'onyea na kutokwa na machozi japo hakusema sababu nini mi nilijua alifedheheka na kitendo cha marafiki zake waliokuja kuhudhuria harusi kutoka Dar watakavyomchukulia poa kwa kuolewa kwa harusi ya hadhi ya chini kiasi kile, chozi lake liliniumiza na maneno waliyokuja kuyasema huku mtaani Shilawadu wale yalimtia unyonge.

Ikanibidi nikae na mke wangu nimuelekeze kwamba thamani ya ndoa sio ufahari wa sherehe bali furaha, faraja, tumaini na amani ya moyo itakayopatikana katika muunganiko wetu nikamuasa kwamba historia ya sherehe yetu haiendi kuathiri chochote katika nyumba yetu vivo hivyo waliofanya sherehe za kifahari hazimaanishi kuwa ndo wataishi kifahari basi siku hiyo nikajiapiza kwamba kila sekunde ya pumzi yangu italenga katika kulifuta lile chozi lake na kumfanya ajivunie mimi kuwa mumewe na kumfanya aione ndoa yetu kuwa ndio chanzo cha furaha yake.

Nikaamua kuishi kama mume wa mtu, mwanaume niliyeishi na kumtunuku mwanamke mmoja kuwa ndio bora na anafaa kuishi nami, nikalipa mahari nikasafiri umbali kumfata yeye aje tuishi pamoja kwanini nisiishi nikiidhihirishia dunia kwamba huyu ndo niliyemchagua nikamuweka ndani? Nikakata shauri nikaanza kuuishi kama mume wa mtu, nikawa naithibitishia dunia kwamba mwanamke yule ndio mwanamke bora zaidi.

NIKALISHINDA JARIBU.

Hali ktk ndoa yetu ilikuwa ya furaha hatukuwa na kipato kikubwa lkn penzi letu lilikuwa ktk thamani ya juu tatizo likaibuka ktk suala la kupata mtoto, tulipanga soon baada ya ndoa tuanze kuwa na watoto lakini tulijaribu bila mafanikio.
Miaka miwili ya kutafuta mtoto mke wangu akakata tamaa kabisa basi ilinibidi nizidishe upendo kama nilivyoahidi kuwa nitamfuta machozi yale aliyoyamwaga, nilikuwa nafanya makusudi nikwaonesha majirani kuwa penzi letu bado linapumua kwa kumtoa out mke wangu kila siku na sio kwamba tulikuwa tunaenda kula bata ya malaki! Lah kuna wakati tulikuwa tunavaa halafu tunanyoosha miguu tu halafu tunafika sehemu tunaagiza soda mojamoja tunakunywa polepole tukimaliza haoooo tunarudi home, hilo lilimpa nguvu mke wangu pia liliwanyon'gonyesha maadui waliokuwa wanauandama umoja wetu sababu hatukujaaliwa mtoto.

Mke wangu ndio rafiki yangu mkuu na nyumbani ndo maskani nnayotumia muda mwingi kuwepo tukitaniana na kupiga soga kemkem, kwakuwa kushinda nyumbani kuna wakati kunachosha nikaanzisha tabia ya kusoma vitabu mbalimbali kupitia kwavyo nikajifunza kwamba ugonjwa wa UTI una mchango mkubwa kufanya wanawake wasishike ujauzito nikamueleza wife mwanzo hakuonesha kulitilia mkazo lakini nikamuelekeza kwamba mazingira ya kuchangia choo cha kulipia yanaweza kuwa sababu ya kumfanya awe na UTI sugu.

NAANZA KUZIFATA KANUNI.

Mwezi wa nne tukaenda kumuona daktari akatuandikia sindano tano na vidonge, basi tukafanya tiba hiyo pia ktk pitapita nikasoma kuwa mbegu za maboga zinamaliza kabisa tatizo nikajipa kazi ya kila siku kumuandalia mbegu za kumeza nami nikifanya hivyo kwa muda wa wiki mbili baada ya hapo tukarudi kupima tukajikuta tuko sawa.

Nikamwambia mke wangu sasa ndo kipindi cha kushika ujauzito na utaushika kwa uwezo wa Mungu, basi nikasoma kitabu cha masuala ya afya kijachofundisha jinsi ya kupata mtoto wa jinsia unayoitaka, mi nikitaka mtoto wa kiume ambapo mafundisho hayo yamenifundisha kwamba naweza kufanikisha kutunga mimba ya jinsi niitakayo kwa kufanya mapenzi na wife siku ya 14 kutokea alipoanza mzunguko na siku hiyo nitaijua kwa kuwa mwanamke atakuwa na ute na ni siku anayotamani kukutana kimwili na mkao wa kufanikisha hilo ni mwanaume kuwa juu au mwanamke ainame na nikishakojoa nisichomoe uume ili kusiruhusu mbegu zisafiri sababu kitaalamu inasemekana mbegu za kiume huwahi kufa hivyo zijahitaji mazingira rafiki.

Kwa upande wangu ambaye ndiye nitapanda mbegu nilijiwekea utaratibu wa kula vyakula vinavyozalisha mbegu bora ambapo nilikuwa nafanya mazoezi kila siku asubuhi baada ya hapo nakunywa uji wa ulezi na maji lita moja, mchana nilikuwa nakula chakula eidha wali au ugali na mboga za majani na matunda au juisi ya kutengeneza pia nilikuwa nakunywa maji lita moja huku jioni nikinywa maziwa fresh au mtindi na kitafunio pamoja na maji mengi ktk vyakula nlivyokuwa nakula vilikuwa vina viungo vya kitunguu swaumu, tangawizi na amdalasini, pia zilikuwa hazipiti siku tatu bila kula samaki nnapozungumzia samaki mjue ni hata dagaa.

Nilisoma kitabu kinachoelezea siri ya wagiriki wa kale njia walizotumia kupata watoto wenye akili nikajifunza kwamba kuna kimelea ktk ubongo kinaitwa Merlyn ndicho kinafanya watu watofautiane kiakili na kimelea hiko kinapatikana ktk vyakula kama samaki, maziwa, nanasi, ndizi mbivu na karanga ndio maana mi nilikuwa nakula sana vyakula hivyo ili nitengeneze mbegu bora siku hiyo ya kupanda.

Mafundisho ya jamii za kiarabu na hata kiongozi wa dini ya kiislam ameshawahi kusema kwamba tunda la pera linanguvu kuubwa ya kutengeneza kiumbe kizuuuri likiliwa masaa machache kabla mwanaume hajamuingilia mkewe kumpa mimba.basi tar 3 mwezi wa 5 ndo ilikuwa siku ya tendo baada ya kuzitengeneza na kutokufanya mapenzi kwa wiki mbili tukafanya yetu.sikwambii nilipopata taarifa kuwa wife kanasa nilijionaje shujaa na kujisikia furaha.nakumbuka ilikuwa mwezi wa ramadhan ndo tulienda kupima.

NALEA MIMBA

Nikajifunza jinsi ya kulea mimba kwamba ktk kipindi chakutokea siku moja mpaka miezi 2 ni kipindi cha usumbufu pia ndo kipindi mwanamke anatakiwa kupatiwa chakula bora kitakachokwenda kumjenga mtoto vyakula hivyo ni ndizi,maini,mboga za majani na matunda haswa, tikiti na ndizi mbivu.

Basi likatokea tatizo la wife kuumwa umwa yani wiki moja hoi kitandani siku mbili mzima wa afya ikanibidi niongeze muda wa kukaa nyumbani mana hatuna mfanyakazi wa ndani, kikawa kipindi cha kuamka alfajiri kusafisha nyumba kumtengea maji ya kuoga wakati anaenda kuoga mi namuandalia nguo za kuvaa na wakati anavaa mi namuandalia kifungua kinywa tunakunywa halafu mi naelekea kazini na nikiwa kazini haupiti muda bila kumjulia hali na ukifika mda wa kutoka kazini silembi ni moja kwa moja nyumbani niwahi kumpikia chakula cha jioni mana mchana nlikuwa namuagiza bodaboda ampelekee chakula.

Siku za weekend huwa natumia kushinda nyumbani.tukishinda kuangalia tv na miongoni mwa kipindi tunachopendelea ni mapishi cha itv tukiangalia na baadae tunakipika chakula hiko pamoja pia ndio siku za kufua.sikuwahi kumuonea noma mtu kufua nguo za mke wangu uani nlikuwa najiachia huku nasikiliza oldskull hiphop za kina rundmc,common,mc right,coolio,naughtyby nature,2pac huku wife akiwa pembeni kazi yake ni kunisaidia kusuuza.

Mke wangu alikuwa ametumia miezi miwili ktk hali hii huku marafiki wakinishauri nimpeleke kwao akaugulie akishajifungua nimrudishe kiukweli sikutaka hilo kwakuwa huyu ndiye mwanamke niliyejiamijisha kuwa nampenda kiasi cha kufunga naye ndoa niliona kuna umuhimu wa kuidhihirishia dunia kuwa hisia zangu zilikuwa kweli sio fashion tu, ikabidi tumpe mtu fremu na vilivyomo tukapata kiasi kadhaa tukanunua bodaboda mbili zilizotumika kidogo, nashukuru Mungu tukapata madereva waelewa ambapo kila wiki tulikuwa tunaingiza elfu 82 kwa pikipiki zote mbili, tukawa tunajadili pamoja matumizi yetu na kujiwekea akiba tukaweza kufungua mradi mwingine wa nguo za mitumba za watoto napo mambo yakatuitikia kiasi cha kushangaza ama kweli katikati ya upendo wa watu Mungu yupo katikati yao.

Huku nyumbani tulikuwa tunauza juisi ya kupima na barafu, tulishirikiana kufunga mabarafu na kutengeneza juice ambapo kwa siku tulikuwa tunapata faida ya 20 elfu ukitoa nalighafi tulizotumia. Kiufupi kupitia ukaribu na kusikilizana tukaweza kuanzisha miradi mingine miwili ijayotuingizia pesa namkumbushaga mke wangu kuwa ni siesie tuliofunga harusi ya kifukara leo tuna ndoa yenye furaha na tunaelekea kubadilisha historia inayoumiza ya umaskini wetu.

Mwezi wa tatu wa tumbo waifu akarejea ktk hali yake mzuri shujaa nilikuwa mimi niliyemuhudumia kwa kujitolea ninafarijika na chozi la mke wangu akimshukuru Mungu kwa kumpa mimi kuwa mumewe. Wakati wote sikuwahi kuwa mbali na Mungu nikifunga na kutoa sadaka kwa ajili ya wife na kiumbe chetu tumboni pamoja na umoja wetu kiujumla. Wife amekuwa akiniandalia msosi mzuuri mida ya kufuturu akinishukuru pia kwa kunuia kufunga kwa ajili yake, shukurani yake ilikuwa inaambatana na vilio.

Kipindi chote naendelea kufuata kanuni za mlo mzuri wa kujenga mtoto mwenye afya njema ya akili na muonekano mzuri plus na funga na sadaka naamini mke wangu atajifungua salama.ktk kipindi cha ujenzi wa uhusiano imara nimejifunza mbinu za kumuongezea thamani mke wangu ikiwemo kutoshitaki jambo lolote upande wangu hata tunapokoseana na mara zote niwapo na ndugu zangu huwa namsifia kwamba mi ni miongoni mwa wanaume wenye bahati nikimtaja yeye kuwa nguzo yangu hii ilifanya ndugu zangu kumheshimu sana na kiukweli inaleta raha kuona mpenzi wako anapatana na nduguzo.

Mwezi wa nne tukaanza clinic na tokea hapo hakuna siku aliyowahi kuhudhuria clinic mwenyew bali tuliongozana, siku za kwenda cliniki tunavyokamiaga sasa tunavaaga sare zetu za nguo za kitenge kutoka kwa fundi wetu Sinza Vatican au style yeyote kali kiasi tukitoka huko nje unaweza kudhani ni couple ya mafisadi kumbe mitumba ya Karume na Mwenge na mishono kwa fundi wetu wa bei chee.

Maandishi yote hapo juu kuonesha tunavyofurahia penzi haimaanishi hatugombani! Tunakosana saana lakini jinsi tunavyovivuka vikwazo na kurudi kuwa pamoja ndio maana kuuubwa zaidi ya kupendana.

NAJIANDAA KUPOKEA MTOTO.

Wakuu wiki ya tatu ya mwezi wa 2 natarajia kupokea mtoto nimekuwa nikiendelea kufunga na kutoa sadaka nikimuomba Mungu atufanyie usalama.

Kuna kitu nataka nikiseme kwamba wengi ktk jamii yetu wanaamini kuandaa vitu kwa ajili ya mtoto ni kukufulu lakini mimi naamini ni kuonesha kwa vitendo jinsi ninavyomuamini Mungu kwamba atatufanyia usalama ndiomaana tumeandaa vitu kibao kwa ajili ya mtoto

Naelewa mtoto huyo akija sisi ndo tutakuwa dhamana ya kuelekea ktk ndoto zake akitutegemea ktk kila kitu hivyo tumejiandaa kuwa wazazi bora binafsi nitaendelea kutimiza ndoto yangu ya kuwa mume bora na hatimaye baba bora nimeanza kusoma vitabu vya wanafalsafa akina maria montessori vinavyoeleza jinsi ya kulea akili ya mtoto ije kuwa kubwa.

Ktk yoote ninayoyaishi changamoto kubwa ni jamii, jamii yetu haituhamasishi kuwa wanandoa bora, wazazi bora, marafiki na majirani wana mtazamo tofauti kwa wanaume wanaojali wake zao na familia zao.

Kama lipo la kujifunza jifunze kupitia sisi.
Ni sie sie tuliofunga harusi ya kifukara kijijini ndio wenye ndoa yenye furaha na tumeinuka kiuchumi tukitaraji arobaini ya mwanetu tutaifanyia kwetu.

Naomba mumuombee mke wangu ajifungue salama salimini na amani ktk ndoa yetu iendelee.

Nitarudi kuwapa mrejesho
 
hongera sana mkuu...mwenyezi Mungu akupe akiri, busara na mafanikio...naamini kitapatikana kiumbe bora kitakachokuja kuibadilisha dunia...abarikiwe saana mwanao mtarajiwa...naomba kwa Mungu awe wa kiume kama sisi ili aje atusaidie kupambana na harakati za kimageuzi.
 
Mkuu Nina roho ngumu ila nimesoma Uzi wako mpaka chozi limenitoka nimetamani muda ufike nipate mke na Mimi nikawe mume bora na baba bora wa familia yangu.

Jambo LA kumshukuru mungu ni mkeo amepewa ufahamu mkubwa ameyashinda maneno ya marafiki na majirani maana hawa mama zetu ni wepesi mno wa kutingishwa na maneno ya watu.

Mungu awatangulie kiongozi ndoto zenu na zikatimie
 
Hongera sana Mkuu.
Kuna wale wanawake wanaosema wanaume wa aina hii wameisha .
Na wengine wanasema wanaume wote wanafanana.
Wanawake, Mwanaume wa aina yako na ndoto zako yupo .
Ni wewe tu kuchagua na Kumuomba Mungu akupe unayemuhitaji.
Jumapili Njema.
Kabisaaaa....wapooo
..
 
Hongera mkuu...hiyo miaka miwili mwingine angeshaenda kuzaa nje..lkn umeonyesha ukomavu wa kutaka kujua tatizo ni ni mpk mkatatua pamoja..chanzo cha yote hayo ni sala.maelewano...na kuvumuliana..
Mungu awabariki zibeni masikio kbsaa msisikie ya walimwengu....
 
Back
Top Bottom