Mimba ya mke wangu inanitesa

Mimba ya mke wangu inanitesa

Nikawaida mbona. Ni hormones tu hizo. Akishajifungua atarudi kawaida. Kila mimba inakuja tofauti. Vumilia tu, your almost there
 
Ndo raha ya mtoto hiyo asikudanganye mtu ukikumbuka karaha zote hizo ndo unajua thamani ya mtoto atakayezaliwa yaani mimi nikiwaangalia wanangu huwa nafurahiiiiiiiiiiiiii. Nawe vuta subira tu utafurahia sana.

Ila daaa umenizidi kusumbuka, mimi wala sikusumbuka sana mimba zote mbili, ni mapenzi tu yalikuwa yanapungua kiasi tu.
 
hujawahi kuamshwa usiku wamanane unaambiwa "NASKIAJOTO NIPEPEE"muhusika sasa anaepepelewa katoa jicho kama nini olewako speed ipunguee,utakiona utaambiwa unamnyanyasa,mara humpendi...makasheshe kibao

Teeh.... teh...!!!!!Pole yako ulitaka ukimpepea afumbe macho?,
 
wadau naomba uzoefu wenu katika hili..

mke wangu ana mimba ya miez 6 sasa na ndo mimba yake ya kwanza. amepunguza mapenzi kwangu japo si saaana ila si kama zamani asiponiona atapiga simu weeee mpaka kero, siku hizi wala, nikichelewa nakuta keshalala wala hana habari na mim.

katika mimba yake hiyo ametokea kupanda kula miwa.. ebwana ikiksekana hakukaliki hom. huwa na kawaida ya kupitia miwa pale mwenge na kumpelekea kila siku. maana ukinunua mingi ukaweka kwenye frij hataki et iaisha utam (ilimradi visa tu)
sasa jana nilichelewwa kurudi kutoka job, kupita mwenge miwa hakuna, zunguka mpaka ubungo hakuna, ikabidi mwanawane kirud hom tu, kufika tu nikajitetea kuwa nilichelewa kurudi nikakosa miwa..,

weeee, aliporomosha matusi mpaka hasira, nikamwacha aongee tu maana nilimbembeleza anisamehe nitaitafta kesho maana ilikuwa saa nne tayari hakunielewa. mpaka akamwaga maji kitandani eti nisilale mpaka miwa ipatikane..,

basi nilizunguka mpaka saa 6 ndo nikaipata buguruni, hapo tuligonga hdi muuzaji keshalala nikidanganya nataka ya kutengenezea dawa.

jaman kuweni na huruma japo kidogo...., hivi baada ya mimba atabadilika kweli au ndo atabadilika mazima my wife wangu!!!...., naumia sana, kuna vituko kibao ila cha jana ndo kiboko...

nawasilisha.

Pole ndugu, hiyo ni mimba tu vumilia akishajifungua atarudi kwenye hali yake ya kawaida, mimi nilipokuwa mjamzito mume wangu alikuwa akirudi nyumbani bila mahindi ya kuchoma yaani halali atatafuta popote mpaka apate, siku moja alichelewa kwenye kikao akakuta wachoma mahindi wamefunga, alipokuja nyumbani akanielezea kiukweli sikumuelewa yaani nilianza kulia kama mtoto mdogo.

Akanibembeleza yaani sikujiskia kabisa kunyamaza, ikabidi awashe gari saa nne hiyo akaenda hadi Tegeta akapata mahindi ambayo hayajajomwa akanunua alipofika nyumbani ikabidi tuwashe mkaa tuanze kuchoma yaani yaliiva saa saba usiku ndio moyo wangu ukatulia nikala nikalala.
 
Nilishawahi kuamshwa saa tisa usiku nikanunue chips kavu...thanks God kulikua na bar inayokesha karibu.......Mimba kiboko!:bange:
Bora hizo chips zinapatikana muda wote, miwa ni kimbembe mkuu..,
 
pole ndugu
hiyo ni mimba tu vumilia akishajifungua atarudi kwenye hali yake ya kawaida,mimi nilipokua mjamzito mume wangu alikua akirudi nyumbani bila mahindi ya kuchoma yani halali atatafuta popote mpaka apate,siku moja alichelewa kwene kikao akakuta wachoma mahindi wamefunga,alipokuja nyumbani akanielezea kiukweli sikumwelewa yani nilianza kulia kama mtoto mdogo,akanibembeleza yani sikujiskia kabisa kunyamaza,ikabidi awashe gari saa nne hiyo akaenda haditegeta akapata mahindi ambayo hayajacomwa akanunua alipofika nyumbani ikabidi tuwashe mkaa tuanze kuchoma yani yaliiva sa saba usiku ndo moyo wangu ukatulia nikala nikalala
I can see myself in your husband, nashukuru sana kwa mawazo yako, hapo sasa naamini yataisha. Thanks mtende.
 
Kuna jamaa alikurupushwa saa nane za usiku mkewe kamwambia anahitaji matango jamaa akabanwa kweli ikabidi akapige hodi kwa muuza matango kwa bahati nzuri akapewa!

Kuyaleta nyumbani akaambiwa ayakatekate kisha ampe akae nayo awe anayanusa maana anapenda harufu yake!
Chezeiya mimba wewe!
 
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
 
Nilishawahi kuamshwa saa tisa usiku nikanunue chips kavu...thanks God kulikua na bar inayokesha karibu.......Mimba kiboko!:bange:

Poleni sana wa ndugu hizi mimba zinamambo kweli..
 
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
dah! hili alo kiboko jamani...., ila utaenda tu. maana hasira zao ni balaa
 
Yaani huyo wako cha mtoto mimi mama angu alikuwa hataki kusikia harufu yoyote ile ya mafuta miezi tisa yote hakuna kupaka mafuta wala manukato

Pia alikuwa anapenda kula chakula alichopika baba tu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Duh, hii nayo kiboko, mleta uzi, vumilia tu, akishajifungua yote hayo yataisha na wote akili yenu itakuwa kwa new baby
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
 
Back
Top Bottom