wadau naomba uzoefu wenu katika hili..
mke wangu ana mimba ya miez 6 sasa na ndo mimba yake ya kwanza. amepunguza mapenzi kwangu japo si saaana ila si kama zamani asiponiona atapiga simu weeee mpaka kero, siku hizi wala, nikichelewa nakuta keshalala wala hana habari na mim.
katika mimba yake hiyo ametokea kupanda kula miwa.. ebwana ikiksekana hakukaliki hom. huwa na kawaida ya kupitia miwa pale mwenge na kumpelekea kila siku. maana ukinunua mingi ukaweka kwenye frij hataki et iaisha utam (ilimradi visa tu)
sasa jana nilichelewwa kurudi kutoka job, kupita mwenge miwa hakuna, zunguka mpaka ubungo hakuna, ikabidi mwanawane kirud hom tu, kufika tu nikajitetea kuwa nilichelewa kurudi nikakosa miwa..,
weeee, aliporomosha matusi mpaka hasira, nikamwacha aongee tu maana nilimbembeleza anisamehe nitaitafta kesho maana ilikuwa saa nne tayari hakunielewa. mpaka akamwaga maji kitandani eti nisilale mpaka miwa ipatikane..,
basi nilizunguka mpaka saa 6 ndo nikaipata buguruni, hapo tuligonga hdi muuzaji keshalala nikidanganya nataka ya kutengenezea dawa.
jaman kuweni na huruma japo kidogo...., hivi baada ya mimba atabadilika kweli au ndo atabadilika mazima my wife wangu!!!...., naumia sana, kuna vituko kibao ila cha jana ndo kiboko...
nawasilisha.