Military Politics: Is Magufuli in danger?

Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.
Vema 100%
 
Dictators handbook unacho? Kisome vizuri.
 
Sasa awatume majenerali katika operesheni,na baadae igundulike wamesababisha hasara ya mamia ya mabilioni,na yeye ajipange kuwapeleka mahakamani,hapo ndio wanajeshi watatumia survival technique ili wasipelekwe kortini
Kazi yao ni kulinda mipaka ya Nchi, na sio kubeba magunia.

Kuwatumia hawa kama tambaa
La kufutua miguu sio sahihi hata kidogo.

Wanapatisha hasara, alafu huna cha kuwafanya.
 
Kuna kazi zao muhimu, za kufanya sasa Raia wa kawaida wafanye shughuli gani? Maana wajeda sio wanasiasa kulinda mabenki hufanywa na kampuni za ulinzi sasa ukitumia wajeda Raia wengine watapata wapi kazi.
Jukumu la polisi ni kulinda raia na mali zao, jukumu la jeshi ni kulinda mipaka ya nchi.

Majukumu hayo yapo kisheria.
 
Kweri kaabisa poti
Wafanye kazi haswaaa maswala ya kukaa na kunywa Pombe ambazo zimeondolewa kodi na baadhi ya bidhaa utadhan wao ni RAIA wa Brunei hiyo sio sawa yani na korosho wabangue tu kwa Meno sindoukakamavu wenyewe huo mbona wanapasuaga mawe kwa vichwa? Na kila asubuhi inabidi wawe wanadeki na Barabara za lami maana hili ni jeshi letu
 
We pusi wa uchochoroni, hujui kuwa Misri, Pakistan India na nchi nyingine wana kitu kinaitwa Military Industrial Complexes mfano wa mradi wa Nyumbu au Mzinga.

Hizi mnazoona siyo initiative ya jeshi. Jeshi wakilinda maduka watakuwa na muda gani kudesign vifaa vya kijeshi!
Watadesign mashine za kuhesabia shilling mia
 
Wafanye kazi haswaaa maswala ya kukaa na kunywa Pombe ambazo zimeondolewa kodi na baadhi ya bidhaa utadhan wao ni RAIA wa Brunei hiyo sio sawa yani na korosho wabangue tu kwa Meno sindoukakamavu wenyewe huo mbona wanapasuaga mawe kwa vichwa? Na kila asubuhi inabidi wawe wanadeki na Barabara za lami maana hili ni jeshi letu
Hiki ndicho hasa alimaanisha mleta post, kwa komenti kama hii, in a long run, kutatokea kundi la Watu kama wewe ambao wataendelea kumsifu raisi kwa matumizi ya jeshi. Hii itamfanya aongeze kasi na majukumu zaidi. Kwa sababu hawa watu hawako trained kufanya hizi shughuli za kiraia, wapo watakaoanza kupingana na hizi amri na kurejea viapo vyao na wapo watakaoungana na raisi. Huu mgogoro suluhisho lake ni wananchi kuungana na upande usio wa raisi na haya ndo yanayoitwa mapunduzi
 
Nahisi jiwe alikuwa anapenda sana kuwa mwanajeshi labda nafasi akakosa sasa anaona kulifanyisha kazi ambazo sio anafurahi coz liko chini yake anajihisi na yeye ni mjeshi. Tangu nimepata akili ni yeye tu nimemuona akivaa sare za jeshi kwani waliopita hawa kuwa na uwezo wa kuvaa kombat za jeshi ?
 
Majukumu ya Msingi ya JWTZ
  • Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.
  • Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.
  • Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.
  • Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  • Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chochote cha siasa. Hata hivyo mwanajeshi ana haki ya kupiga kura kama raia yoyote na kuchagua chama au kiongozi anayeona anafaa.

Swali: Je awamu hii ya tano inaheshimu haki hii ya mwanajeshi?
 
huyu bwana pia inawezekana amewaweka wale wazee wa kitengo mfukoni, sasa anatafuta namna ya kudela na wajeda!

sasa kwa sababu hawa hawaingiliki, anatumia njia hii ili waone anawajali
 
Uaminifu hauusiani kabisa na Kuwa wa taasisi maalufu Uaminifu ni malezi na utamaduni,nionavyo tumeacha kuthamini taaluma za watu wetu pia tumeanzisha kutokuaminiana tunaona kila mtu ni mbaya huku tukitelekeza matakwa ya kisheria.
 
Nchi hii bwana watu wameamua kukaa kimya hawmshauri Rais kabisa masikini Rais wetu kila kinacho mjia kichwani ndio anafanya.
Nami hua nashangaa sana,hi ile dhana ya urais ni taasisi siku hizi haipo?.kwamba amekua ni jeshi la mtu mmoja?.watamua/atajiuaa kwa msongo
 
Labda tu unapata shida kuelewa nilichokiandika na ndio maana unakuja na hiyo tafsiri potofu.

All in all, ninachojaribu kubainisha hapa ni kuwa hakuna mwanadamu asiyefanya kosa (No one is infallible) na kwa mantiki hiyo basi kumfanya mtu anayeshikilia taasisi ya urais aonekane kama isiyeweza kutenda kosa ni sawa na kumkufuru Mungu.

Wewe ndiye uliyepata shida kuelewa nilichoandika...hoja yangu was against kejeli, matusi, dharau kwa rais, Head of state na Amiri Jeshi Mkuu...Lakini wewe unakuja na hoja mbovu na yenye mweleko wa ugaidi na kishetani kwamba watu sisi ni vema tupungue...maana ya neno hilo ni moja tu kwamba watu kama sisi tufe ili mbaki nyie mnaojiona mko sahihi kwa hoja zenu...it is ridiculous and a shame...utasemaje wenzio wapungue???!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom