Military Politics: Is Magufuli in danger?

Jeshi la Wananchi Tz, (JWTZ) ni chombo adhimu, angalau bado linaheshimika. Kuna sababu nyingi za kuliheshimu jeshi letu, ingawa sababu hizo zinagawanyika katika makundi makuu mawili. Moja, ni sababu zitokanazo na kazi za jeshi lenyewe. Hapo kuna nidhamu ya jeshi na wanajeshi (bila kujali wachache wanaoharibu taswira hiyo), misheni mbalimbali za ndani na nje zilizofanikishwa na jeshi letu, shughuli mbalimbali za kijamii katika kujenga taifa pamoja na kutoa huduma za kijamii (elimu, afya nk)

Pili, ni sababu zinazotokana na wananchi wenyewe. Hakuna namna wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kuheshimu na kulienzi jeshi lao. Na kwa bahati nzuri, watanzania wamekuzwa kwa namna hiyo, ya kuliheshimu jeshi.

Natambua kuna baadhi ya watumishi wa jeshi wanaotumia 'sare' na vitambulisho vyao kujinufaisha mitaani, na wakati mwingine kufanya vitendo vya uonevu kwa raia. Hao ni wajinga wachache ambao leo sioni haja kuwajadili.

Pamoja na hayo, kuna jambo la kustua ambalo kama halitadhibitiwa, jeshi hili adhimu litageuka kuwa janga taifa; kutumiwa hovyo na serikali.
Narudia kwa msisitizo; "Kutumiwa hovyo na serikali".

Tulianza kuona jambo hili wakati Rais Magufuli akiwatunuku kamisheni wanajeshi waliohitimu mafunzo kule Arusha, Septemba mwaka 2017. Kwenye shuguli hizo za kijeshi, Rais alionekana kujadili jambo na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, liloashiria kuwapo kwa mpango wa kufanya tukio la kisiasa.

Mpango unaoatajwa kuwapo ni ule wa kuwaita watu walioandaliwa (miongoni mwa wananchi waliohudhuria) ili wamsifie Rais kwa maneno waliopandikizwa. Baada ya Gambo kushindwa kuandaa mpango huo, Rais alisikika akimtukana mkuu huyo wa mkoa. Ilikuwa ni ishara mbaya kwa matukio hayo kufanyika kwenye shughuli za kijeshi.

Haikuwa bahati mbaya, matukio ya aina hiyo yanaendelea. Inaonekana ni kama hulka ya serikali ya awamu ya tano kulitumia jeshi, hata kwenye mambo yasio ya lazima.

Kutumia jeshi kwenye sakata la korosho, ni muendelezo wa matumizi ya hovyo ya jeshi. Pamoja na mikurupuko mingine, karibuni tutaona mpango huo ulivyoleta matokeo mabaya.

Tunaambiwa pia, jeshi limepewa kazi ya kulinda maduka ya kubadilishia fedha, eti kuna operesheni maalum ya kudhibiti wanaotakatisha fedha, inastua.

Je! Serikali haina mifumo ya kudhibiti utakatishaji fedha badala yake inatuma wanajeshi wakae kwenye milango ya maduka ya kubadilisha fedha? Natamani kujua taaluma za wanajeshi waliosimama kwenye milango ya maduka kama wana ufahamu wa masuala ya utakatishaji fedha.

Rais ana wasiwasi?
Matumizi ya jeshi, au kukimbilia kutumia jeshi katika mambo yanayoweza kufanywa na taasisi zingine, ni ishara ya nini? Wasiwasi? Hofu? Ulimbukeni wa madaraka? Au vitisho?

Ikiwa sababu ni wasiwasi na/au hofu ya kushindwa kuongoza, maana yake tayari umeshinda kuongoza. Hapa nirejee maneno ya Profesa Mkandala, kwamba kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wa hiari. Ikiwa Rais anatumia jeshi kwa kukosa imani na taasisi zingine, maana yake ameshindwa kuongoza taasisi hizo.

Je! Ni vitisho? Kama ni vitisho, Rais anamtishia nani? Haiwezekani kutumia jeshi kuwatisha watu mmoja mmoja ambao wanaonekana kuwa maadui (wa kisiasa). Jeshi linapotumika kwa lengo la vitisho, maana yake wanaotishiwa ni wananchi. Kuwatisha wananchi unaowaongoza ni ishara ya kushindwa kuongoza.

Bado natafuta kujua lengo la matumizi ya jeshi yasiyo ya lazima.

Mwisho, mimkumbushe Rais Magufuli na wafuasi wake, madaraka ni kama mchanga. Kadiri unavyoukumbatia mchanga kiganjani ndivyo unavyokuponyoka, na ukilegeza vidole pia unakuponyoka. Unahitaji kuwa mtu wa kiasi (gentle), mtu wa hekima na maarifa.

Ni vema kujua kwamba hakuna mahala pengine baada ya jeshi. Ikiwa matumizi haya ya jeshi yana lengo la kujitutumua, kutunisha misuli, maana yake umejitutumua hadi mwisho, na umetunisha misuli hadi mwisho, kwa kuwa jeshi ndio mahali pa mwisho. Hakuna pengine pa kukimbilia. Kutumia jeshi badala ya taasisi zingine ndio tafsiri ya kuyakumbatia madaraka (kama mchanga kiganjani) kwa nguvu zote, kifuatacho ni madaraka hayo kukuponyoka.

Ni vema hatua za haraka zikachukuliwa kudhibiti matumizi haya ya jeshi yasio ya lazima.
Nimeandika.
Lengo ni kulidhoofisha kwa kuliondolea kujiamini mbele ya Presidency.Maafisa wa ngazi za chini wanapomuona CDF amegeuzwa kama Mkuu wa Idara fulani serikalini kunawafanya wasijione special kama zamani.Unapotumia jeshi kukusanya korosho kazi inayoweza fanywa hata na wanafunzi wa Shule unadhani ni bahati mbaya??
 
Asante sana Dr Cyrillo.

Kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wa hiari.
 
Nilipotoa mfano wa kusimamia maduka ya Bureau de Change kule Arusha, wote tunajua haikuwahi kutokea. Kabla ya jeshi, kuna Polisi, Takukuru na FIU (Financial Intelligence Unit). Swali ni je! Vyombo vyote hivyo vimeshindwa? Sikatai kwamba jeshi lina wajibu wa kufanya kazi ile, swali ni je! Tumeshafikia wakati wa kutumia jeshi. Kama jibu ni ndio, basi hali ni tete. Kama jibu ni sio, tunarudia kwenye mada yangu, Matumizi ya hovyo ya jeshi letu.
Rais kapaniki na jeshi ndio nguvu yake ya mwisho kabisa sasa likiboronga na hili sijui atakimbilia wapi.
Tatizo ni yeye mwenyewe wala sio tasisi za serikali. Inaonekana tasisi za serikali zimegoma hazimpi ushirikiano. Na kwanini hazimpi ushirikiano mpaka kukimbilia jeshini??
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Sisi watanzania ;nadhani tuna tatizo lingine nje ya elimu tunayosoma.
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Tatizo la hii nchi kila mtu anataka amsaidie maamuzi Rais bila hata kujua katiba na sheria zinasemaje. Tuna watu wa ajabu sana.

Hawajui jeshi linaweza kuja hata nyumbani kwao kulinda ama kukagua na kamwe weledi wa jeshi hautoshuka. Wajaribu kuushusha waone nini kitawakuta
 
Dharula ni nini kwako ndugu???

Maana maelezo yameainisha kwamba jeshi jwtz linatumika badala ya polisi, kuelekeza nguvu katika usimamizi wa mitihani???hivyo kuna upungufu wa polisi.au ni dharula gani ulihisi katiba ikimaanisha!!!

Hayo ndio majukumu ya keshi jwtz wakati huu wa amani,nyinyi mnaotaka kuleta tafsili nyingine za vichwani mwenu ndio mnajichanganya.
Hata Gambia watu kama nyinyi walikuwepo.
 
Hii pia inastahili kuitwa low IQ post, kwa hiyo wanajeshi wanaojenga Madaraja, kuokoa watu, kusaidia wagonjwa, hata kufundisha Watoto kusoma na kuandika Shuleni ni matumizi mabaya ya jeshi? Hivi unajua kuna wanajeshi walimu na Madaktari na wanatibu watu? Hivyo wanaoenda kutibiwa Lugalo ni matumizi mabaya ya jeshi?
Au unafikiri Jeshi kwako ni kushika mtutu tu wa Bunduki?
Ccm ni janga kwa Taifa na ile elimu bure tutegemee ujinga na upumbavu kuongezeka mtaani kama wewe.
 
Jeshi la Wananchi Tz, (JWTZ) ni chombo adhimu, angalau bado linaheshimika. Kuna sababu nyingi za kuliheshimu jeshi letu, ingawa sababu hizo zinagawanyika katika makundi makuu mawili. Moja, ni sababu zitokanazo na kazi za jeshi lenyewe. Hapo kuna nidhamu ya jeshi na wanajeshi (bila kujali wachache wanaoharibu taswira hiyo), misheni mbalimbali za ndani na nje zilizofanikishwa na jeshi letu, shughuli mbalimbali za kijamii katika kujenga taifa pamoja na kutoa huduma za kijamii (elimu, afya nk)

Pili, ni sababu zinazotokana na wananchi wenyewe. Hakuna namna wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kuheshimu na kulienzi jeshi lao. Na kwa bahati nzuri, watanzania wamekuzwa kwa namna hiyo, ya kuliheshimu jeshi.

Natambua kuna baadhi ya watumishi wa jeshi wanaotumia 'sare' na vitambulisho vyao kujinufaisha mitaani, na wakati mwingine kufanya vitendo vya uonevu kwa raia. Hao ni wajinga wachache ambao leo sioni haja kuwajadili.

Pamoja na hayo, kuna jambo la kustua ambalo kama halitadhibitiwa, jeshi hili adhimu litageuka kuwa janga taifa; kutumiwa hovyo na serikali.
Narudia kwa msisitizo; "Kutumiwa hovyo na serikali".

Tulianza kuona jambo hili wakati Rais Magufuli akiwatunuku kamisheni wanajeshi waliohitimu mafunzo kule Arusha, Septemba mwaka 2017. Kwenye shuguli hizo za kijeshi, Rais alionekana kujadili jambo na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, liloashiria kuwapo kwa mpango wa kufanya tukio la kisiasa.

Mpango unaoatajwa kuwapo ni ule wa kuwaita watu walioandaliwa (miongoni mwa wananchi waliohudhuria) ili wamsifie Rais kwa maneno waliopandikizwa. Baada ya Gambo kushindwa kuandaa mpango huo, Rais alisikika akimtukana mkuu huyo wa mkoa. Ilikuwa ni ishara mbaya kwa matukio hayo kufanyika kwenye shughuli za kijeshi.

Haikuwa bahati mbaya, matukio ya aina hiyo yanaendelea. Inaonekana ni kama hulka ya serikali ya awamu ya tano kulitumia jeshi, hata kwenye mambo yasio ya lazima.

Kutumia jeshi kwenye sakata la korosho, ni muendelezo wa matumizi ya hovyo ya jeshi. Pamoja na mikurupuko mingine, karibuni tutaona mpango huo ulivyoleta matokeo mabaya.

Tunaambiwa pia, jeshi limepewa kazi ya kulinda maduka ya kubadilishia fedha, eti kuna operesheni maalum ya kudhibiti wanaotakatisha fedha, inastua.

Je! Serikali haina mifumo ya kudhibiti utakatishaji fedha badala yake inatuma wanajeshi wakae kwenye milango ya maduka ya kubadilisha fedha? Natamani kujua taaluma za wanajeshi waliosimama kwenye milango ya maduka kama wana ufahamu wa masuala ya utakatishaji fedha.

Rais ana wasiwasi?
Matumizi ya jeshi, au kukimbilia kutumia jeshi katika mambo yanayoweza kufanywa na taasisi zingine, ni ishara ya nini? Wasiwasi? Hofu? Ulimbukeni wa madaraka? Au vitisho?

Ikiwa sababu ni wasiwasi na/au hofu ya kushindwa kuongoza, maana yake tayari umeshinda kuongoza. Hapa nirejee maneno ya Profesa Mkandala, kwamba kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wa hiari. Ikiwa Rais anatumia jeshi kwa kukosa imani na taasisi zingine, maana yake ameshindwa kuongoza taasisi hizo.

Je! Ni vitisho? Kama ni vitisho, Rais anamtishia nani? Haiwezekani kutumia jeshi kuwatisha watu mmoja mmoja ambao wanaonekana kuwa maadui (wa kisiasa). Jeshi linapotumika kwa lengo la vitisho, maana yake wanaotishiwa ni wananchi. Kuwatisha wananchi unaowaongoza ni ishara ya kushindwa kuongoza.

Bado natafuta kujua lengo la matumizi ya jeshi yasiyo ya lazima.

Mwisho, mimkumbushe Rais Magufuli na wafuasi wake, madaraka ni kama mchanga. Kadiri unavyoukumbatia mchanga kiganjani ndivyo unavyokuponyoka, na ukilegeza vidole pia unakuponyoka. Unahitaji kuwa mtu wa kiasi (gentle), mtu wa hekima na maarifa.

Ni vema kujua kwamba hakuna mahala pengine baada ya jeshi. Ikiwa matumizi haya ya jeshi yana lengo la kujitutumua, kutunisha misuli, maana yake umejitutumua hadi mwisho, na umetunisha misuli hadi mwisho, kwa kuwa jeshi ndio mahali pa mwisho. Hakuna pengine pa kukimbilia. Kutumia jeshi badala ya taasisi zingine ndio tafsiri ya kuyakumbatia madaraka (kama mchanga kiganjani) kwa nguvu zote, kifuatacho ni madaraka hayo kukuponyoka.

Ni vema hatua za haraka zikachukuliwa kudhibiti matumizi haya ya jeshi yasio ya lazima.
Nimeandika.
Pumba tupu umeandika. Huna akili za kuchambua ila umejaa uasi.
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Kakushikia nani ubongo?
 
Yeye ni Bosi wa kila kitu. Anaelewa vema matarajio ya watanzania na nani mwadilifu atakaye fanikisha. Hata timu ya Taifa nadhani tungemuunga mkono wachukuliwe wajeshi waweze kutetea Taifa ktk michezo.
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Ikitokea hivyo unavyosema, halafu mtawala huyo akaitwa dictator uchwara atakuwa ameonewa?
 
Mbona mme panic jamani, kwani amiri jeshi mkuu ni nani? Jeshi linalinda raia wake nyie mnalalmika. Mimi ningelalamika nayi kama jeshi lingepiga raia/wananchi. Lakini halikufanya hivyo na mimi sikupata taharuki yoyote, kwani hao jamaa nimeishi nao lugalo area H sioni tabu kiivyo kuwaona mitaani.
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Hoja ya hovyo kabisa hii.
 
Hii ya kulinda maduka ya fedha ndio imenishangaza zaidi, inaonekana ni kwa jinsi gani serikali iko hoi kifikra hadi kiuchumi.
Kwa utawala huu alidhani ni nani mjinga akafiche hela za magumashi huko bureau de change?
 
Mwandishi wa thread hii nimeota kuwa ni mkubwa fulani serikalini.

Ni busara sana mnavyotoa madukuduku yenu hapa kwa kuwa Manyota in charge huwa anapitia huku mara kwa mara.
 
ni rahisi kujua wewe ni mtu wa aina gani kwa kauli yako hii...kumuombea mwenzako apungue yaani unamuiombea kifo,,kumwambia mwenzako ni kauli za shari...ni bahati mbaya mno kwa nchi yetu kwa mtu kutoa kauli za aina hiyo..baadala ya kuleta hoja wewe unaendeshwa na mihemko...
Labda tu unapata shida kuelewa nilichokiandika na ndio maana unakuja na hiyo tafsiri potofu.

All in all, ninachojaribu kubainisha hapa ni kuwa hakuna mwanadamu asiyefanya kosa (No one is infallible) na kwa mantiki hiyo basi kumfanya mtu anayeshikilia taasisi ya urais aonekane kama isiyeweza kutenda kosa ni sawa na kumkufuru Mungu.
 
Tawala za kijeshi ulimwenguni pote huwa hazijianzii tu bali husukumizwa kwenye majengo ya ikulu na ngazi zote za maamuzi kupitia mifumo ya kiraia iliyoshindwa, kulegalega, kandamizi, dhalimu, kiimla na kikabila. Kwa muhtasari tu wa tabia za tawala hizi ni kwamba;-

1. Wanajeshi wa ngazi za juu wanaposhirikishwa kufanya maamuzi ya kiraia kwa kudhani huko kutaongeza utii wao kwa serikali iliyopo madarakani kama ilivyokuwa enzi za Hosni Mubaraka. Hali hii hufanya wanajeshi wa ngazi za juu kuwatumia wale wa vyeo vya chini kufanya mapinduzi ili wao wasionekane kuwa chanzo cha kutotii.( Field mashall Tantawi na Abdelfatah Al sisi).

2. Wanajeshi ni mjumuiko wa wananchi wenye elimu na mitazamo tofauti isipokuwa wenye falsafa inayofanana sana. Heshimu aliyejuu yako hasa akiwa mwanajeshi mwenzako hiyo ndio falsafa yao. Katika mazingira ya kawaida ambapo katiba huongoza maamuzi yote ya kiutawala na kuheshimiwa jeshi ni chombo cha kusimamia na ulinzi na kulinda mipaka ila pale katiba inapokuwa majaribuni jeshi laweza kuwa chombo cha kuongeza mtanziko wa kiutawala kwa kujiingiza kwenye uongozi wa nchi.

3. Watawala waoga hujikuta wamekabidhi mamlaka ya uongozi jeshini bila kujua. Pale inapotokea mtawala wa kikatiba ni mwoga dhidi ya wapinzani wake kisiasa kwa kushindwa kujibu hoja zao, kuminya democrasia, kuiba mali ya umma na kupora haki za wanahabari hujikuta amekuwa adui wa wa wananchi wenzake hivyo hujitafutia huruma toka vikosi vya majeshi ambavyo navyo hujikuta kuomba malipo ya fadhila kwa kuingilia maamuzi ya utawala na hivyo kujigeuza watawala halisi.

4. Raia wanyonge na makundi muhimu ya kuboresha uchumi katika jamii yakikandamizwa hupelekea taifa kuingia kwenye mtanziko wa kimaendeleo na kukwamisha huduma za kijamii na kiraia ambapo hiyo hupelekea hata wanajeshi kukosa baadhi ya stahili zao huku mafisadi wachache wakijilimbikizia mali. hali hii huishia kuwafanya wanajeshi kuingilia masuala ya maamuzi kama ilivyotokea Zimbabwe ambapo jeshi lilimpumzisha swahiba wao Mugabe na hadi leo Zimbabwe ina unafuu kabisa kuliko enzi za Dictator huyo katili.

5. Kwa ufupi utawala wa kijeshi sio mbaya kutegemea na muundo wa jeshi na malezi ya kiutamaduni yaliyojengeka kati ya wananchi na jeshi lao, uwezo wa kiutawala ambao jeshi linao mfano wasomi wa taaluma mbalimbali, uhusiano wa kimataifa ambao jeshi linao vyote hivyo huchangia utawala bora wa kijeshi.

Kuhusu jeshi letu kwa sasa linahitaji bado kujengewa uwezo wa kuongoza taasisi achilia mbali nchi kutokana na kuwa na wasomi wachache, wasomi wasio na ujuzi wa kivitendo, tamaa ya kuishi kifahari, mitazamo isiyo ya kijeshi mfano wengi wapo jeshini kutokana na kukosa kazi mahali pengine hivyo kuishi kama sio wanajeshi. Ushauri ni kwamba ili Jeshi liweze kuwa na uwezo ni vizuri likafanya recruit toka watumishi wa umma wenye umri, elimu na uzoefu unaohitajika ili kwa mikataba maalumu wachangie huo uwezo wao na kulijengea jeshi letu uwezo wa kiutalawala kwenye nyanja mbalimbali.
Jeshi oyeeeee
 
Back
Top Bottom