Military Politics: Is Magufuli in danger?

Military Politics: Is Magufuli in danger?

Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Mleta mada kauliza kwamba hao wanajeshi wanaokaa nje ya bureau de change wana elimu au taaluma gani? Isijekua aliefeli form 4 unampa majukumu yaliyo nje ya uwezo wake
 
Wengi wa watanzania mnaojadili hili swala ni ama hamjui majukumu ya jeshi ama mnaongozwa na mihemko.

Jeshi letu kama yalivyo mengine ulimwenguni humu,kazi yake ni ulinzi wa mipaka ya nchi.mbali na jukumu hilo,jeshi lolote la nchi liko tayari kufanya kazi yoyote ambayo ina maslahi ya nchi husika.isiwe kwa maslahi ya mtu/kiongozi binafsi.
Kwa tanzania katiba imeamrisha kwamba jeshi linawajibika(WAJIBIKA)kushirikiana na taasisi za kiraia katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii mfano wakati wa majanga-jeshi litashiriki uokoaji.

Hivyo basi,anachofanya magufuli na jeshi la nchi(jwtz)kina baraka zote kikatiba,wala msije mkadhani ni mwendawazimu.

Nilipotoa mfano wa kusimamia maduka ya Bureau de Change kule Arusha, wote tunajua haikuwahi kutokea. Kabla ya jeshi, kuna Polisi, Takukuru na FIU (Financial Intelligence Unit). Swali ni je! Vyombo vyote hivyo vimeshindwa? Sikatai kwamba jeshi lina wajibu wa kufanya kazi ile, swali ni je! Tumeshafikia wakati wa kutumia jeshi. Kama jibu ni ndio, basi hali ni tete. Kama jibu ni sio, tunarudia kwenye mada yangu, Matumizi ya hovyo ya jeshi letu.
 
Jeshi la Wananchi Tz, (JWTZ) ni chombo adhimu, angalau bado linaheshimika. Kuna sababu nyingi za kuliheshimu jeshi letu, ingawa sababu hizo zinagawanyika katika makundi makuu mawili. Moja, ni sababu zitokanazo na kazi za jeshi lenyewe. Hapo kuna nidhamu ya jeshi na wanajeshi (bila kujali wachache wanaoharibu taswira hiyo), misheni mbalimbali za ndani na nje zilizofanikishwa na jeshi letu, shughuli mbalimbali za kijamii katika kujenga taifa pamoja na kutoa huduma za kijamii (elimu, afya nk)

Pili, ni sababu zinazotokana na wananchi wenyewe. Hakuna namna wananchi wanaweza kufanya zaidi ya kuheshimu na kulienzi jeshi lao. Na kwa bahati nzuri, watanzania wamekuzwa kwa namna hiyo, ya kuliheshimu jeshi.

Natambua kuna baadhi ya watumishi wa jeshi wanaotumia 'sare' na vitambulisho vyao kujinufaisha mitaani, na wakati mwingine kufanya vitendo vya uonevu kwa raia. Hao ni wajinga wachache ambao leo sioni haja kuwajadili.

Pamoja na hayo, kuna jambo la kustua ambalo kama halitadhibitiwa, jeshi hili adhimu litageuka kuwa janga taifa; kutumiwa hovyo na serikali.
Narudia kwa msisitizo; "Kutumiwa hovyo na serikali".

Tulianza kuona jambo hili wakati Rais Magufuli akiwatunuku kamisheni wanajeshi waliohitimu mafunzo kule Arusha, Septemba mwaka 2017. Kwenye shuguli hizo za kijeshi, Rais alionekana kujadili jambo na Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, liloashiria kuwapo kwa mpango wa kufanya tukio la kisiasa.

Mpango unaoatajwa kuwapo ni ule wa kuwaita watu walioandaliwa (miongoni mwa wananchi waliohudhuria) ili wamsifie Rais kwa maneno waliopandikizwa. Baada ya Gambo kushindwa kuandaa mpango huo, Rais alisikika akimtukana mkuu huyo wa mkoa. Ilikuwa ni ishara mbaya kwa matukio hayo kufanyika kwenye shughuli za kijeshi.

Haikuwa bahati mbaya, matukio ya aina hiyo yanaendelea. Inaonekana ni kama hulka ya serikali ya awamu ya tano kulitumia jeshi, hata kwenye mambo yasio ya lazima.

Kutumia jeshi kwenye sakata la korosho, ni muendelezo wa matumizi ya hovyo ya jeshi. Pamoja na mikurupuko mingine, karibuni tutaona mpango huo ulivyoleta matokeo mabaya.

Tunaambiwa pia, jeshi limepewa kazi ya kulinda maduka ya kubadilishia fedha, eti kuna operesheni maalum ya kudhibiti wanaotakatisha fedha, inastua.

Je! Serikali haina mifumo ya kudhibiti utakatishaji fedha badala yake inatuma wanajeshi wakae kwenye milango ya maduka ya kubadilisha fedha? Natamani kujua taaluma za wanajeshi waliosimama kwenye milango ya maduka kama wana ufahamu wa masuala ya utakatishaji fedha.

Rais ana wasiwasi?
Matumizi ya jeshi, au kukimbilia kutumia jeshi katika mambo yanayoweza kufanywa na taasisi zingine, ni ishara ya nini? Wasiwasi? Hofu? Ulimbukeni wa madaraka? Au vitisho?

Ikiwa sababu ni wasiwasi na/au hofu ya kushindwa kuongoza, maana yake tayari umeshinda kuongoza. Hapa nirejee maneno ya Profesa Mkandala, kwamba kiongozi bora ni yule mwenye wafuasi wa hiari. Ikiwa Rais anatumia jeshi kwa kukosa imani na taasisi zingine, maana yake ameshindwa kuongoza taasisi hizo.

Je! Ni vitisho? Kama ni vitisho, Rais anamtishia nani? Haiwezekani kutumia jeshi kuwatisha watu mmoja mmoja ambao wanaonekana kuwa maadui (wa kisiasa). Jeshi linapotumika kwa lengo la vitisho, maana yake wanaotishiwa ni wananchi. Kuwatisha wananchi unaowaongoza ni ishara ya kushindwa kuongoza.

Bado natafuta kujua lengo la matumizi ya jeshi yasiyo ya lazima.

Mwisho, mimkumbushe Rais Magufuli na wafuasi wake, madaraka ni kama mchanga. Kadiri unavyoukumbatia mchanga kiganjani ndivyo unavyokuponyoka, na ukilegeza vidole pia unakuponyoka. Unahitaji kuwa mtu wa kiasi (gentle), mtu wa hekima na maarifa.

Ni vema kujua kwamba hakuna mahala pengine baada ya jeshi. Ikiwa matumizi haya ya jeshi yana lengo la kujitutumua, kutunisha misuli, maana yake umejitutumua hadi mwisho, na umetunisha misuli hadi mwisho, kwa kuwa jeshi ndio mahali pa mwisho. Hakuna pengine pa kukimbilia. Kutumia jeshi badala ya taasisi zingine ndio tafsiri ya kuyakumbatia madaraka (kama mchanga kiganjani) kwa nguvu zote, kifuatacho ni madaraka hayo kukuponyoka.

Ni vema hatua za haraka zikachukuliwa kudhibiti matumizi haya ya jeshi yasio ya lazima.
Nimeandika.
Mimi naomba tumwache azoeane na jeshi hivyo hivyo...kuna siku watamwambia Mzee tumeona utupishe tu hicho kiti hako "tuinyooshe nchi" ....na hapo hapo ataielewa vizuri dhana ya "kuinyosha nchi" maana wataanza naye!
 
Nianze kwa kusema kwamba miaka mitatu inatosha

JPM anatumia Jeshi katika operesheni mbalimbali lakini je anaelewa kwamba The army has no loyalty?Katika siasa za majeshi mwanajeshi hafundishwi siasa ya loyalty anafundishwa survival.

Unapoamua kutumia Jeshi katika operesheni yoyote ila lazima iwe na lengo moja Kutishia,kuogopesha na kushurutisha.Lakini unapolitumia Jeshi kushughulika na mambo ya raia unatakiwa ujue kwamba mahaba kati ya Jeshi na Raia yanaweza kufanya kuibuka kwa mawazo ya kimapinduzi kwa wanajeshi hasa iwapo unawatumia kukandamiza wananchi na wanyonge.

Kumbuka Soldiers have no Loyalty,they train to survive.

Nimshauri tu mheshimiwa raisi hata kama hana imani na watendaji wa serikali yake awe makini na matumizi ya jeshi letu.

Asiwageuze wanajeshi wetu vibarua wakutumwa kushughulikia hata issue zisizo na maslahi ya taifa.

Ha wa watu hawajawa trained kubeba magunia ya korosho na kubangu,Hawajawa trained kujenga kuta na kufanya shughuli za suluba.Wamefundishwa Vita,Kama usipowapa Vita watakuletea Vita.
Ndugu wewe bila shaka ni mjeda, haya madini siyo ya mtu wa kawaida!
 
Mleta mada kauliza kwamba hao wanajeshi wanaokaa nje ya bureau de change wana elimu au taaluma gani? Isijekua aliefeli form 4 unampa majukumu yaliyo nje ya uwezo wake
Kwani kusimama nje ndo anahesabu? Taaluma yake ni ulinzi sasa unasemaje kwamba hana taaluma?
 
Hii pia inastahili kuitwa low IQ post, kwa hiyo wanajeshi wanaojenga Madaraja, kuokoa watu, kusaidia wagonjwa, hata kufundisha Watoto kusoma na kuandika Shuleni ni matumizi mabaya ya jeshi? Hivi unajua kuna wanajeshi walimu na Madaktari na wanatibu watu? Hivyo wanaoenda kutibiwa Lugalo ni matumizi mabaya ya jeshi?
Au unafikiri Jeshi kwako ni kushika mtutu tu wa Bunduki?
Hebu sikiliza vizuri ufafanuzi wa Gavana, anasema wamelazimika kutumia Jeshi la wananchi kwa sababu Polisi walikuwa kwenye mitihani ya form 2. Kwa maana nyingine matumizi ya JW ni dharura ila wapo waliostahili kutumika. Sisi tusioshikiwa akili tunasema waliostahili wapo wa kutosha. Sasa wewe hizi ngonjera zilizo tofauti na maelezo ya Gavana unazitoa wapi?
 
Kuna jambo atakua analitengeneza huyu. Juzi kati hapa aliongea kuhusu timu ya taifa iundwe na wanajeshi.
 
Mnamjibu mleta uzi kwa jazba. Kisa jiwe. Jiulize malori ya jeshi yameleta tani ngapi za korosho hadi leo? Na zikisha letwa Dar , jiulize zisipo nunuliwa hadi mwakani gharama zote zitakuwa juu ya nani? Zisipopanda bei hao wajeda watakula wenyewe na familia zao? Kuna wajanja sana jeshini, wanaoweza kuatathmini risk za operesheni yo yote iwe ya kijeshi au vinginevvyo. Jeshi nalo lifikirie lisije likawa la kulaumiwa baada ya show kuisha bila chembe ya mkwanja!
 
Yaani the way unavyodiscuss tu unaonekana ni kijana mdogo kifikra. Sitakuuliza mahali umeona jeshi likilinda maduka ya fe

Mdogo wangu, chutama kidogo. Nimesoma udaktari na baadhi ya vitabu nilivyotumia library vina nembo ya US Army, US Navy na/au US Marine. Ni kweli jeshi linapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi karibu zote, nimeweka kwenye paragraph ya kwanza. Hata hivyo kisingizio hiko hakitoshi kuwa sababu ya jeshi kufanya kazi za taasisi zingine wakati hakuna dharura. Nchi ina taasisi zake, labda tuseme taasisi hizo zimeshindwa na haiwezekani kuzirekebisha. Zaidi ya hapo, matumizi ya jeshi kwenye kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi zingine kwa muda wote ni ishara ya kushindwa. Nilipoandika kwamba jeshi ndio kitu cha mwisho cha kukumbatia ulielewa nini? Au ni u-Syncophant unakusmbua? Unataka 1 kusema tayari tumefikia wakati kutumia jeshi kufabya kazi za polisi, FIU na Takukuru?
Unaamini kwamba unafikria sawasawa?

Dharula ni nini kwako ndugu???

Maana maelezo yameainisha kwamba jeshi jwtz linatumika badala ya polisi, kuelekeza nguvu katika usimamizi wa mitihani???hivyo kuna upungufu wa polisi.au ni dharula gani ulihisi katiba ikimaanisha!!!

Hayo ndio majukumu ya keshi jwtz wakati huu wa amani,nyinyi mnaotaka kuleta tafsili nyingine za vichwani mwenu ndio mnajichanganya.
 
Hauelewi unachokiongea, Wanajeshi wana kazi nyingi, mimi nimefundishwa Shuleni na walimu Wanajeshi, Je walikuwa wanatumika vibaya? Jeshini kuna watu wamejiriwa kama madereva tu, wengine mafundi mekanika wote hawa ni Wanajeshi, sasa Serikali ikiwatumia ni kuna ubaya gani? Na unafahamu kwamba JKT ni Jeshi pia? Unajua kazi ambazo JKT wanafanya? Wana viwanda, wanazalisha, wanalima, wanafanya mambo kibao tu, hii ni kawaida Dunia nzima, tatizo lenu mmekaririshwa sana kila kitu na hamuwezi kufikiria hata kidogo nje ya kile mlichokaririshwa, mkisikia Jeshi mnafikiria Vita tu!
Wewe ndio mgumu kuelewa mbona kaeleza mwanzo kabisa mwa paragraph ya Kwanza
 
Yaani the way unavyodiscuss tu unaonekana ni kijana mdogo kifikra. Sitakuuliza mahali umeona jeshi likilinda maduka ya fe

Mdogo wangu, chutama kidogo. Nimesoma udaktari na baadhi ya vitabu nilivyotumia library vina nembo ya US Army, US Navy na/au US Marine. Ni kweli jeshi linapaswa kuwa na uwezo wa kufanya kazi karibu zote, nimeweka kwenye paragraph ya kwanza. Hata hivyo kisingizio hiko hakitoshi kuwa sababu ya jeshi kufanya kazi za taasisi zingine wakati hakuna dharura. Nchi ina taasisi zake, labda tuseme taasisi hizo zimeshindwa na haiwezekani kuzirekebisha. Zaidi ya hapo, matumizi ya jeshi kwenye kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi zingine kwa muda wote ni ishara ya kushindwa. Nilipoandika kwamba jeshi ndio kitu cha mwisho cha kukumbatia ulielewa nini? Au ni u-Syncophant unakusmbua? Unataka 1 kusema tayari tumefikia wakati kutumia jeshi kufabya kazi za polisi, FIU na Takukuru?
Unaamini kwamba unafikria sawasawa?
Achana nae mkuu mbona umeweka kila kitu Sawa kwenye paragraph ya Kwanza kbs
 
Nilipotoa mfano wa kusimamia maduka ya Bureau de Change kule Arusha, wote tunajua haikuwahi kutokea. Kabla ya jeshi, kuna Polisi, Takukuru na FIU (Financial Intelligence Unit). Swali ni je! Vyombo vyote hivyo vimeshindwa? Sikatai kwamba jeshi lina wajibu wa kufanya kazi ile, swali ni je! Tumeshafikia wakati wa kutumia jeshi. Kama jibu ni ndio, basi hali ni tete. Kama jibu ni sio, tunarudia kwenye mada yangu, Matumizi ya hovyo ya jeshi letu.

Kwanini bado sio wakati wa kutumia jeshi!!!???

Kwanini udhani kwamba vyombo vyote havifanyi kazi mpaka likatumika jeshi!!!

Wote tunafahamu kwa sababu ya umasikini,taasisi nyingi za serikali zinakabiliwa na upungufu wa watumishi ,utakuwa mtu wa ajabu sana kuamini kwamba watumishi wa taasisi zote hizo TAKUKURU,FIU,POLISI pasipo kuathili majukumu yao ya kila siku,wangeweza kushiriki zoezi hilo kikamilifu na kuacha wanajeshi wakiwa wamepumzika kambini.
 
Mimi naomba tumwache azoeane na jeshi hivyo hivyo...kuna siku watamwambia Mzee tumeona utupishe tu hicho kiti hako "tuinyooshe nchi" ....na hapo hapo ataielewa vizuri dhana ya "kuinyosha nchi" maana wataanza naye!

Au sio.
 
Mnanishangaza sana kwani jeshi limekatazwa kazi yeyote kati ya wanazopangiwa na Magufuli?

Onesha kifungu chochote kinachoonesha kwamba jeshi linakatazwa kufanya kazi gani na kazi gani?

Yeye ndo amiri jeshi mkuu hata akiamua kwamba wao ndo wasafishe jiji msiulize

Hata akisema ndo walinde mabenki yote hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema kwamba wao ndo walinde clubs zote hakuna mtu wa kuuliza

Hata akisema kila headmaster wa shule za serikali awe mjeda hakuna haja ya kuuliza

Hata akisema call centres kwenye mitandao wakae wajeda kaa kimya
Wewe na upupu wako ndo utashindwa kuuliza na itakubidi ufunge mdomo ukae kimya waachie wenye nafasi kubwa kwenye bongo zao waulize wewe kaa kimya ivyoivyo mzee
 
Kwanini bado sio wakati wa kutumia jeshi!!!???

Kwanini udhani kwamba vyombo vyote havifanyi kazi mpaka likatumika jeshi!!!

Wote tunafahamu kwa sababu ya umasikini,taasisi nyingi za serikali zinakabiliwa na upungufu wa watumishi ,utakuwa mtu wa ajabu sana kuamini kwamba watumishi wa taasisi zote hizo TAKUKURU,FIU,POLISI pasipo kuathili majukumu yao ya kila siku,wangeweza kushiriki zoezi hilo kikamilifu na kuacha wanajeshi wakiwa wamepumzika kambini.
Nimejiridhisha kwamba nahitaji kukuacha.
 
Back
Top Bottom