Milioni 500 Kumaliza Ujenzi Kituo cha Afya Madilu - Jimbo la Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

MILIONI 500 KUMALIZIA UJENZI KITUO CHA AFYA MADILU

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga amesema nwaka huu serikali inatoa kiasi cha sh. Mil. 500 kwaajili ya umaliziaji ujenzi wa kituo cha afya cha kata ya Madilu ambacho wananchi wamejenga kwa asilimia 80 kwa kuchangishana fedha kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara alipofanya ziara katika kijiji cha Madilu, Ilawa na Ilininda vilivyopo katika kata hiyo mbunge huyo amesema awali alipata taarifa kutoka kwa baadhi ya wananchi waliodai kuwa kuna fedha ambazo wananchi wamechanga lakini zimeingia mifukoni mwa viongozi ambapo alitoa taarifa katika ofisi za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao walituma wakaguzi watatu ili kuja kufanya uchunguzi.

”Haiwezekani wananchi wanakuwa na moyo wa kuchangia halafu wanatokea watu wasiopenda maendeleo wanatumia fedha ambazo wananchi wamejibana ili wapate maendeleo halafu anatokea mtu anakula, hii ni kuwavunja moyo wananchi”. Amesema Kamonga.

Aidha kwa upande wa wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa huduma ya kituo cha afya ni kipaumbele kwao kwani wanapata tabu katika kupata huduma na hasa za uzazi kwani wanalazimika kwenda katika kata ya Lugarawa ama Mundindi kitu ambacho kinawalazimu kutembea umbali mrefu sana.
 

Attachments

  • IMG-20230708-WA0010.jpg
    IMG-20230708-WA0010.jpg
    207.6 KB · Views: 4
  • IMG-20230708-WA0009.jpg
    IMG-20230708-WA0009.jpg
    149.9 KB · Views: 3
  • IMG-20230708-WA0008.jpg
    IMG-20230708-WA0008.jpg
    75.6 KB · Views: 3
  • IMG-20230708-WA0007.jpg
    IMG-20230708-WA0007.jpg
    68.7 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom