Kituo cha Afya Mundindi Tarafa ya Liganga Kinachokwenda Kuhudumia Wakazi Zaidi ya 40,000 Wilaya ya Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
946

TIZAMA PICHA ZA KITUO CHA AFYA MUNDINDI AMBACHO KINAENDA KUHUDUMIA WAKAZI ZAIDI YA 40,000 TARAFA YA LIGANGA- KATA YA MUNDINDI, WILAYA YA LUDEWA

Wakazi zaidi ya 40,000 wa Tarafa ya Liganga wilayani Ludewa mkoani Njombe wameondokana na adha ya kutembea umbali wa zaidi ya Km. 50 kufuata huduma ya afya baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha sh. Mil 500 ambazo zimewezesha kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kwa asilimia 100 ulio ambatana na unujuzi wa vifaa Tiba vyenye thamani ya sh. Mil 150.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa; Victoria Mwanziva amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwekeza katika sekta ya Afya Wilayani Ludewa- zaidi ya Bil. 1.5.

Kituo hicho kinaenda kutoa huduma ya wagonjwa wa nje, chanjo, uzazi, vipimo vya maabara,uteketezaji wa taka, huduma ya upasuaji kwa akina mama wajawazito na wagonjwa wengineo.

Akizindua kituo hicho mkuu wa wilaya amesema katika kipindi hiki cha uongozi wa serikali ya awamu ya Sita suala la huduma ya afya imekuwa likipewa kipaumbele kwani wilaya ya Ludewa tayari imepokea fedha za kuboresha huduma ya Afya na ni mojawapo ya vipaumbele katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi wote.

Kuhusu mapokezi ya vifaa tiba Mwanziva amewaagiza watoa huduma kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu huku akiyaomba mashirika mbalimbali pamoja na wadau wa afya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya kwa kuleta vifaa tiba ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora zaidi na kuwaasa wananchi hao kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili waweze kupata huduma kwa gharama nafuu.

"Tunamshukuru mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa kwa ushiririkiano wao uliowezesha kupatikana kwa fedha hizo za miradi kwani Rais huyo amekuwa akifika kusiko fikika kwa kuleta Fedha za kuboresha miundombinu hii ya afya na si hizo tuu bali hata katika miradi mingine kama ya elimu na barabara ", Amesema Bi. Mwanziva.

#LudewaYetu #Ludewa
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.28.jpeg
    67.3 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27(2).jpeg
    85.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27(1).jpeg
    91.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.27.jpeg
    75.3 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.26.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 09.15.26.jpeg
    73 KB · Views: 3
Back
Top Bottom