Jimbo la Kaliua: Kituo cha Afya Usinge Chapokea Vifaa Tiba vya Tsh. Milioni 200

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

JIMBO LA KALIUA: KITUO CHA AFYA CHA USINGE CHAPOKEA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA ZAIDI TSH. MILIONI 200

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Amin Vasomana ameshiriki zoezi la kupokea vifaa Tiba vyenye thamani ya Tsh. 214,253,955.11.

Zoezi hilo limeshuhudiwa na viongozi mbali mbali akiwemo diwani wa Kata hiyo Mhe. Taitas Kalomba Kivula, Wananchi kwa jumla, pamoja na Kamati ya fedha ya Kata ya Usinge.

Akizungumzia suala la kuongeza watumishi, Mganga Mkuu Wilaya ya Kaliua, Dkt. Amin Vasomana amesema wanatarajia kupeleka watumishi wawili kwenye kituo hicho cha afya ambapo pia watumishi wawili wamepelekwa kusoma na kwamba wakirudi mmoja wao atapelekwa kwenye kituo hicho cha afya.

Awali akizungumza afisa mauzo msaidizi bohari ya dawa kanda ya Tabora, Dorothea Mkama amesema vifaa tiba hivyo vilivyotolewa ni kwa ajili ya huduma za upasuaji na maabara vifaa vilivyotolewa kupitia mradi wa cemonc unaolenga kuboresha huduma za mama na mtoto.

Vifaa hivyo vinakwenda kuongeza chachu ya utoaji huduma ya upasuaji Kwenye kituo hicho huduma ambayo aikuwepo hapo awali ambapo Kituo hicho kitasaidia kutoa huduma kwa vijiji vya jirani.
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.27.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.30(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.30(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.30.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.29(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.29.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.27(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.28.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.28(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-02 at 11.49.28(2).jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom