DC Ludewa azindua Kituo cha Afya na Zahanati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

DC LUDEWA AZINDUA KITUO CHA AFYA NA ZAHANATI

Na. Damian Kunambi, Njombe.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amezindua kituo cha afya Mundindi kilichogharimu kiasi cha zaidi ya sh. Mil. 500 ambapo uzinduzi wa kituo hicho uliambatana na mapokezi ya vifaa tiba vvyenye thamani ya sh. Mil. 150.

Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho iliyowasilishwa kwa mkuu huyo wa wilaya katika hafla ya uzinduzi huo imeeleza kuwa kituo hicho cha afya kinaenda kunufaisha wakazi zaidi ya elfu arobaini wa Tarafa ya Liganga ambao hapo awali walikuwa wakikumbwa na changamoto juu ya upatikanaji wa huduma hiyo.

Akizindua kituo hicho mkuu huyo wa wilaya amesema katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita suala la huduma ya afya imekuwa ikipewa kipaumbele kwani wilaya ya Ludewa tayari imepokea fedha nyingi za kuboresha huduma hiyo ikiwemo kiasi cha sh. Mil 900 kwaajili ya kuboresha miundombinu ya majengo katika Hospitali ya wilya hiyo, Mil. 200 kwaajili ya kukamilisha zahanati ya Kitongoji cha Chimbo, zahanati ya Mkiu, Kimelembe ambazo zote tayari zimekamilika na kuanza kutoa huduma huku zahanati ya kijiji cha Ndowa ujenzi wake ukiendelea.

Kuhusu mapokezi ya vifaa tiba Mwanziva amewaagiza watoa huduma kuvitunza vifaa hivyo ili viweze kutumika kwa muda mrefu huku akiyaomba mashirika mbalimbali pamoja na wadau wa afya kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya kwa kuleta vifaa tiba ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora zaidi na kuwaasa wananchi hao kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili waweze kupata huduma kwa gharama nafuu.

"Tunamshukuru mama yetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mbunge wa jimbo la Ludewa kwa ushiririkiano wao uliowezesha kupatikana kwa fedha hizo za miradi kwani Rais huyo amekuwa akifika kusiko fikika kwa kuleta Fedha za kuboresha miundombinu hii ya afya na si hizo tuu bali hata katika miradi mingine kama ya elimu na barabara ", Amesema Bi. Mwanziva.

Katika hatua nyingine pia mkuu huyo wa wilayani amezindua zahanati ya kitongoji cha Chimbo ambayo imegharimu kiasi cha zaidi ya Sh. Mil. 74 ambapo miongoni mwa fedha hizo Mil. 50 imetolewa na serikali na nyinginezo ni michango ya wananchi na wadau mbalimbali wa afya.

Sunday Deogratius ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo amesema amepokea maelekezo hayo huku akiwapongeza wananchi kwa kujitoa kuanzisha ujenzi miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo zahanati na vituo vya afya ambapo amewataka kuendeleza jitihada hizo za kujitoa katika maendeleo ambapo serikali itawaunga mkono badala ya kukaa na kusubiri serikali ianzishe miradi hiyo.

Ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua juhudi za wananchi kupitia mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga huku akiwataarifu kuhusu ujio wa fedha za Ruzuku ya maendeleo ya halmashauri ya Wilaya hiyo kiasi cha zaidi ya sh. Bil. 1.5 hivyo ameahidi kutenga kiasi cha Sh. Mil. 150 kwaajili ya ununuzi wa vifaa vingine zaidi katika kituo cha afya Mundindi.

"Ndugu zangu ujio wa fedha hizi za maendeleo, upatikanaji wa vifaa tiba na fedha za umaliziaji miradi ya ujenzi zinakuja kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge wetu Joseph Kamonga ambaye tumekuwa tukifanya nae kazi bega kwa bega na amekuwa akizunguka katika wizara mbalimbali ili kuona namna ya kupata fedha za maendeleo ya jimboni kwake lakini tunashukuru Rais wetu Dkt. Samia amekuwa akiona jitihada zetu na mbunge huyo matokeo yake amekuwa akiidhinisha fedha kwa kipindi kifupi tuu baada ya kuombwa". Amesema Mkurugenzi Ludewa.

#LudewaYetu #Ludewa
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56.jpeg
    85.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56(1).jpeg
    82.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.56(2).jpeg
    58.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57.jpeg
    75.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57(1).jpeg
    67.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.57(2).jpeg
    80.6 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58.jpeg
    69.5 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58(1).jpeg
    55.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.58(2).jpeg
    71.7 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.59.jpeg
    WhatsApp Image 2023-09-15 at 02.26.59.jpeg
    92.2 KB · Views: 2
Ni habari njema sana hii, pokeeni maua yenu wana Ludewa. Hongera sana.

Hapa wale wachukia maendeleo hutawaona. Lakini ni vyema sana wajionee wenyewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom