Mikoa maskini zaidi yatajwa

Mikoa maskini zaidi yatajwa

Umeshafika hizo wilaya nilizotaja lakini,Karagwe hakuna nyumba ya nyasi wala udongo,vyakula vingi,kahawa na mahindi na maharage yanawapa hela sana
Karagwe nyumba za udongo nyingi tu
Ngara,biharamulo ndo hoi
Muleba nyumba za nyasi nyingi mno hasa kata za ngenge,kimwani,nyakabango,mushabago,kasharunga NK
 
Mkuu,

Lindi siku hizi tumeamka Sana.

Tuna misimu ya mazao Kama Sita kwa mwaka inayotufanya tutoke kwenye umasikini wa kutupwa.

Tuna msimu wa mahindi,
Msimu wa kunde,
Msimu wa ufuta,
Msimu wa mbaazi,
Msimu wa korosho,
Na mwisho kabisa msimu wa maembe ambayo kuanzia mwezi wa kumi Hadi wa 12 tunalisha miji mikubwa Kama Dar na Sasa hivi Bahresa ananumua Sana. Si umewahi kusikia "haya ni maembe ya kusini?" Basi ndiyo sisi.

Pia kwa. Maeneo yenye maji ya kutosha tunalima Sana nyanya na vitunguu ambavyo tunalisha mtwara,masasi na Dar es salaam.

Alafu Kuna mgodi wa Namungo ambao upo Ruangwa,unawanufaisha wananchi na kuongeza mzunguko wa hela maana **** wageni wengi Sana Sasa hivi. Rungwa inafikika kwa barababrayya lami na Kuna mahoteli kadhaa ya ghorofa yanayoupendezesha mji.

2025 nikigombea ubunge nikapita ndiyo naenda kuibadilisha moja kwa moja Lindi.

Kwa hiyo Lindi haiwezi kuwa katika hiyo list ya Kigoma,Kagera na Tabora.
Hongereni Lindi, Sisi Wana Kilimanjaro tuko pamoja nanyi tunashukuru kwa mashirikiano yenu kibiashara na Sisi maeneo ya Kilwa ,Lindi town nk
 
Unavyowaona Wapemba wana mabiashara makubwa mikoa mbalimbali hasa Kariakoo huwezi dhani Pemba wengine hawana hata vyoo. Kuna Mhindi maskini bongo? Ila kwao India kuna maskini chungu nzima.

Umaskini wa eneo unaweza tokana na fursa ndogo zilizopo ila watu wake walewale wanaweza enda sehemu nyingine wakatajirika. Ndio maana Hyundai ilianzishwa na jamaa aliyetoroka North Korea na Hyundai kwa mwaka inatengeneza hela nyingi zaidi kuliko bajeti ya North Korea nzima.

Elon Musk alitoka South Africa kaenda Marekani sasa ni tajiri, Sergei Brin wazazi waliondoka Urusi wakaenda Marekani na sasa ni billionaire.
Wayahudi wana umiliki wa biashara kubwa na institutions duniani ila nchi yao inasaidiwa security package na Marekani.
Watu pekee walioweza kuwa matajiri nyumbani na ugenini ni Wachagga. Kuna la kujifunza kutoka kwa miamba hii.
 
Jibu lako la kisomi lakini mbona wandegereko wazalamo wakwele ni masikini wengi wao tena kuliko wakaazi wa kagera?
Wanabebwa na makabila mengine yaliyo Ktk jamii zao
Mfano wachaga dar wameinunua tangu zamani,hâta ukija kisarawe , bagamoyo,kibaha NK Wachaga wamewasogeza hivyo maendleo yaliyo Ktk jamii hizo yanawabeba ijapokuwa wao hawana kitu
 
Yaani ukitoa Kilimanjaro, mikoa mingine ya Tanzania ni majanga matupu kwa sehemu kubwa. Kiujumla kwa sehemu kubwa ya nchi kuna harufu kali ya umaskini. Bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Serikali izidi kupambana sana kwenye miundombinu, kilimo na elimu. Watu wengi wakipata elimu bora watapambana kujikwamua. Hata Kilimanjaro walitanguliza elimu ndo maana wako hapo walipo.
Tuma salamu kwa watu wawili
 
Huko Kilimanjaro kuna nini, tutolee utapiamlo hapa.
Utapiamlo ni hawa
Tofautisha vitambi n'a utapiamlo
Kilimanjaro inaongza kwa vitambi manake Watu Wana over feed
1676389990311.jpg
 
Hata huko Kilimanjaro watu wamechoka sana,hakuna unafuu labda useme tunazidiana kwenye umaskini, hii nchi watu waliojikomboa toka kwenye umaskini ni asilimia ndogo sana.

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Naam Kilimanjaro umaskini upo Ila ni kwa 10% tu hakuna anaebisha,hâta uchina,usa,ujerumani maskini wapo
 
Back
Top Bottom