Mikoa 20 yathibitisha kuhudhuria kesi ya Mbowe Kisutu Agosti 5, 2021

UVIKO-19 Regulations hazitumiki katika shughuli za CCM&Serikali yake.Hamkuona nyomi la Mbeya leo katika Uzinduzi wa Mafunzo ya Uanagenzi?Bila barako na zero distance? Wanadiriki hadi kunong'onezana.UVIKO-19 sasa ni zaidi ya siasa ni kampeni towards 2025 General Elections.
 
Hii ndio sababu ya Sirro kukurupuka leo na tamko lake dhidi ya Mbowe.
 
Mpaka Leo saa 5 Asubuhi taarifa kutoka makao makuu ya Chadema zinasema tayari mikoa 20 ya Tanzania imethibitisha kutuma wanachama kwa gharama zao kuhudhuria kesi hiyo.
 
Mimi nimefika Singida, nimetokea Katavi naelekea Dar kuhudhuria kesi ya Mbowe 5/8/2021.
 
Hiyo tarehe 5 watatofautishwaje wanaoenda kwenye kesi zao, na sisi tunaoenda kwa Freeman??!! Au wote tutachakazwa....
 
Zero anaapa kwa Mungu kuwa anaushahidi lakini aliapa pia kwa MO na kutuonyesha picha za gari ya watekaji mpaka leo kimya, huyu mzee nimshauri asitafu tu...
 
Hiyo tarehe 5 watatofautishwaje wanaoenda kwenye kesi zao, na sisi tunaoenda kwa Freeman??!! Au wote tutachakazwa....
Na kuna wengine tumeshauliwa kama kweli Mbowe anamuamini Mungu atuambie ukweli sasa siku nzuri ya kutuambia ukweli ni hiyo tarehe 05.08...watanzania tujitokeze kwa wingi, gaidi asiekuwa na silaha akatuambie ukweli twendeni mahakamani tarehe hiyo..
 
Kijani wenyewe hawapati corona,au tuseme wanawajali Sana Chadema,mawazo yako tasafali ndugu mujumbe.
 
Zero anaapa kwa Mungu kuwa anaushahidi lakini aliapa pia kwa MO na kutuonyesha picha za gari ya watekaji mpaka leo kimya, huyu mzee nimshauri asitafu tu...
Asitafu kwa hiari kulinda heshima ya uzee,kabla haijaharibika yote.
 
Sidhani kama watakutanika chadema ya sasa ni yamatamko kuliko vitendo.
 
Na Dotto Bulembo wa DW

Kati ya Mwaka 1995-2000 kulikuwa Na mvutano mkali sana kati ya dola Na Chama cha CUF,dola ilitumia kila mbinu kuaminisha umma hususani wa Wazanzibar Kuwa CUF ni Chama cha kisultan,chenye viashiria vya vurugu.

Siku chache kabla ya Uchaguzi,CUF walituhumiwa kuingiza silaha za jadi Ili kuharibu Uchaguzi,Hali ilikuwa mbaya visiwani Zanzibar,Wazanzibar walianza kubaguana Kwa misingi ya vyama,CUF alikuwa hashirikiani na CCM Kwa chochote Mpaka misiba.

Mwana CCM hakuruhusiwa kwenda kuchota maji Kwenye kisima cha Mwana CUF Kama ilivyokuwa Mwana CUF hakuruhusiwa kwenda kuchota maji Kwenye kisima cha Mwana CCM.

Baadhi ya wachambuzi wa Siasa waliona siyo mwelekeo mzuri na wakashauri yafanyike maridhiano,bahati mbaya hawakusikilizwa,mbinu ya kuwaita CUF Kuwa Chama cha Kisultan,Kigaidi Na kihaini ndiyo ikachaguliwa.

Uchaguzi wa Mwaka 2000 ukafanyika huku ukiacha kilio kikubwa Kwa CUF,sauti zao hazikusikika badala yake wakaendelea kuitwa majina Mabaya Kuwa wanataka kuirejesha Zanzibar Kwa Sultan.

Januari 2001 ukaweka historia mbaya Kwenye Siasa za nchi hii baada ya CUF kuandaa maandamano Na kusababisha kuumana Na dola na kusababisha Vifo,ulemavu Na Baadhi ya watu kuikimbia nchi.

Baada ya hapo ndipo tukaanza kuona Vikao vya maridhiano kati ya CUF na dola vilivyolenga kutibu madonda ya 1995,2000 Na 2001.

Huu ndiyo Mkasa ambao Rais mstaafu wa awamu ya tatu Hayati Benjamini Mkapa ulimuumiza Mpaka anakwenda kaburini.

Dola ijenge utamaduni wa kukutana Na vyama pale kunapokuwa Na sononeko kubwa juu ya Haki Na demokrasia,dola isisubiri Mpaka watu waumizane ndiyo ianze vikao.

Nimekuwa nafuatilia mijadala inayoendeshwa kupitia mtandao wa "Space" Na "Club house",ukienda huko ukawasikiliza watu wanayoyazungumza basi vifua vya watu vina mengi.

"Space" Na "Club house" zinaendesha mjadala unaowashirikisha watu Mpaka 2500 Kwa wakati mmoja huku wakiweka Mpaka maadhimio ya namna ya kupigania haki zao.

Baada ya watu kuzuiwa kukutana Na kujadili masuala ya kisiasa,Sasa wanakutana huko Kwenye Club house Na Space,wanazungumza Kwa hisia na mijadala mikali ni Haki za binadamu.

Space Na Club house imekuwa mbadala wa vyama vya Siasa,Baada ya vyama vya Siasa kuambiwa hakuna vikao,wakikutana wanakamatwa,Sasa watu wanakutana kidigital tena wakiwa huru.

Ni vizuri kuviachia vyama vya Siasa huru vifanye Siasa Kwani ndipo sehemu ambayo watu hupumua Kwa kuzungumza yaliyo moyoni mwao,ukivibana watasaka majukwaa mengine tena yasiyohitaji ruhusa ya polisi.

Dola isipuuze kilio kuhusu Haki za binadamu Na demokrasia,ni vizuri yakafanyika mazungumzo Kati ya Serikali yenye dola,vyama vya Siasa,wataalam,Asasi za Kiraia Na madhehebu ya dini,kilio cha watu ni kikubwa kuhusu Haki Na demokrasia.

Haina haja ya kuamini Kuwa Kuwa watanzania wenye nchi Na watanzania wanaotumika,wote ni watanzania .

Nawaasa Viongozi wa dini,Wasomi na makundi yenye ushawishi iiteni Serikali Na muiambie ipo haja ya kukaa na mijadili Siasa za Tanzania,tujenge utamaduni wa kukaa pamoja Na kusikilizana.

#Equal rights by Peter Tosh
#One love by Bob Marley
#Together as one by Luck Dube
#Amani by Justine Kalikawe
#Amani by Vijana Makongoro
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…