Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

Mikataba ya Madini na Serikali ya Tanzania

...they were not being audited before 2003, such cheating could not be detected. However, the first audit of gold mining companies carried out by Washington DC based the Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (ASA) revealed how mining firms were cheating the government. Their 2003 audit of three out of the six big mining companies revealed for the first time discrepancies that have cost Tanzania millions of dollars in tax revenue.
Kwa mtazamo wangu, hapa ndipo wazungu wanapotuona majuha. Kama tuliilipa hii kampuni 'billions of money' kisha waka'reveal' wizi tena wa wazi, imekuwaje tumeshindwa kujenga hoja kusitisha walau hii mikataba mitatu kutokana na wao kuanza kuivunja? Au naota kwa kuwa kuna mambo ya 10%?!

...in one instance showed that Geita Gold Mine (GGM)'s "declared accumulated tax losses of US$193 million up to December 2003 is reduced by an estimated US$158 million, making their allowed accumulated tax losses to be US$35 million only."

What this means is that, instead of the company carrying forward a tax loss of US$35m, which would be offset by profit of the following year, the company carried forward a hugely inflated figure of US$193 million. Thus, by offsetting against the profit of the following year, profit declared in the year 2004/2005 was much less than the actual figure. Which means, the tax paid to the government was much less than what should have been due.
Wizi unafanyika kweupeee! Shame being Tanzanian!
 
Zitto,
Shukran sana kwa mara nyingine umedhihirisha maneno yangu ya mwaka 2001 ambayo niliwambieni kuhusu Mkapa na njama zake ndani ya madini kupitia mabalozi wawili waliomtangulia Kalaghe.. Hawa wote wame oa nyumba moja na Mkapa... mkewe Mkapa na wake za hawa mabalozi ni dada wa tumbo moja sasa pimeni uzito wa hawa balozi kuwepo canada wakati nchi yetu ikiingia madeal ya madini, hakuna haja ya kuzunguka mjomba sema ukweli watu wapate kufahamu unachojaribu kupigania.

Kitu kimoja tu ndugu Zitto ningependa kukuuliza, Reality ya nchi yetu inatupa picha wazi kuwa mara nyingi sheria haifuatwi hata kama ipo na wanaotumaliza ni kati ya hawa viongozi wetu wa kudumu! - Problem kubwa ya Tanzania na hasa Africa ni WATU wasoshiba wala sio sheria.
Je, kuna uwezekano gani wa kuondoa pungufu hili la viongozi wa kudumu. Tunaona mawaziri waliovurunda wakadilishwa wizara lakini bado wamekalia viti vyao vya Uongozi!..
Haya, pamoja na kufahamu kuwa hawa mabalozi wameshiriki kutufunga kamba za shingo leo hii bado ni balozi wetu nchi nyinginezo.. kilichopungua hapo na kiwango cha shibe, lakini ulaji bado upo palepale!...
 
Zitto,

Wajumbe wote wa Kamati, mpaka sasa, wapo so serious. Mwenyekiti yupo so serious. Kumbukeni mtu kama Bomani na Simba ni watu ambao hawataki kitu in public isipokuwa historia kuwajudge positively. Hawa wazee ni serious huwezi amini.



Mkuu Zitto,

Heshima mbele na elimu saafi sana, lakini I have a problem na Bomani, toka arudi kugombea urais 1995, na kuukosa akaishia kujiiingiza kwenye siasa za CCM ametoa kauli nyingi ambazo si za kimabadiliko ambayo taifa tunayahitaji na hasa unayojaribu kuyasimamia, naamini kuwa huenda you know something I do not, lakini yeye na Warioba ni Viongozi pekeee waliotoa kauli za kushangaza tena against the respect of the rule of law, wakiwa na hoja ya ku-sucrifice tuhuma za ufisadi in the name of national peace, wakishindwa kuelewa kuwa ili kuimarisha hiyo national peace yetu, ni muhimu kusimamia sheria iapasavyo,

Halafu huyu ndiye mkuu wa maelezo kama sikosei, amewahi kutoa kauli yningi sana kupinga hata kauli zako za msingi kwa taifa, kwa kisingizio cha maadili na always umoja wetu, sasa what makes you believe in him, kwamba yuko serious this time kwenye hii ishu ya madini, baada ya kauli zake za kupinga the way Chadema went about the business za kuwafichua wafisadi? Mkuu huyu mimi simuamini namuona kuwa anataka ukurugenzi wa bodi za serikali za CCM, au? Maana tunajua kuwa kuna viongozi wengi walioombwa na Mtandao wawatetee kuhusiana na tuhuma za ufisadi, wakakataa, lakini huyu na Warioba wakakubali, sasa tumuamini vipi kwenye hili la mdaini? Simba huyo ninamuamini 100%, lakini huyu mkuu simuamini labda utuweke sawa kidogo mkuu, maana ninaamaini you something we do not!
 
Zitto,
Shukran sana kwa mara nyingine umedhihirisha maneno yangu ya mwaka 2001 ambayo niliwambieni kuhusu Mkapa na njama zake ndani ya madini kupitia mabalozi wawili waliomtangulia Kalaghe.. Hawa wote wame oa nyumba moja na Mkapa... mkewe Mkapa na wake za hawa mabalozi ni dada wa tumbo moja sasa pimeni uzito wa hawa balozi kuwepo canada wakati nchi yetu ikiingia madeal ya madini, hakuna haja ya kuzunguka mjomba sema ukweli watu wapate kufahamu unachojaribu kupigania.

Hebu tutajie ndugu yangu ni kina nani hao?
 
Hebu tutajie ndugu yangu ni kina nani hao?

Mheshimiwa Nurujamii,Mabalozi alowataja Ndg Mkandara hapo awali ni;
1; Ben Moses - Ambaye sasa yupo Sweden. na
2; Ombeni Sefue - Ambaye sasa ni Balozi wetu US.

Wakuu hawa kwa wakati tofauti wamewahi kuwa Mabalozi Canada na wameoa nyumba Moja na Mzee Mkapa.
 
Jaji Bomani atetea hoja ya Zitto

MWENYEKITI wa Kamati ya Rais ya Ushauri kuhusu Sekta ya Madini, Jaji Mark Bomani, amesema hoja aliyoitoa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe ilikuwa ni muhimu baada ya kuona kwamba mambo hayakwenda sawa katika mkataba wa Kampuni ya Barrick kuhusu mgodi wa Buzwagi.

Akizungumza katika mahojiano na kituo cha Watanzania cha matangazo ya kiintaneti cha Kijijini Leo Hii News Network, Jaji Bomani alisema Zitto alitaka iundwe kamati ya Bunge kwa hoja tofauti.

“Hoja ya Mhe. Zitto ilikuwa ni muhimu baada ya kuona kwamba mambo hayakwenda sawa katika mkataba wa Kampuni ya Barrick kuhusu mgodi wa Buzwagi.

Yeye alitaka iundwe kamati ya Bunge kwa hoja tofauti. Hivyo ingawa kuna uhusiano wa namna fulani kuundwa kwa kamati yetu hakuhusiani moja kwa moja na hoja ya Zitto,” alisema Jaji Bomani.

Zitto aliwasilisha bungeni hoja akitaka kuundwa kwa Kamati Teule ya Bunge, kuchunguza Mkataba wa Buzwagi pamoja na mikataba mingine hya madini sambamba na kuangalia sheria za madini na sheria za kodi zinazogusa sekta hiyo, mambo ambayo yameguswa katika kamati ya Rais.

“Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi yatatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu,” alisema Zitto alipowasilisha hoja yake iliyopingwa na wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mbali ya kukataliwa kwa hoja hiyo, Zitto alijikuta ‘akigeuziwa kibao’ na kusimamishwa bunge hadi alipoteuliwa na Rais Kikwete katika kamati mpya ya madini siku chache kabla ya kumaliza kifungo chake Novemba 17 mwaka huu.

Jaji Bomani katika mahojiano hayo, anabainisha umuhimu wa kama ingeundwa Kamati Teule ya Bunge kama alivyopendekeza Zitto kwa maelezo kwamba kamati yake haina nguvu za kisheria na kibunge kama ambavyo ingekua Kamati ya Bunge.

“Kamati ya Bunge inapoundwa inakuwa na nguvu za kisheria za kuita watu, kuhoji watu na nguvu nyingine za kimahakama na hata za kuadhibu, kitu ambacho kamati yetu haina.

“Hata hivyo kamati yetu imeundwa na Rais na ndiye atakayepelekewa mapendekezo hayo. Yeye ana uwezo wa kukubaliana na mapendekezo hayo na kupendekeza sheria kwa hiyo pamoja na kuwa kamati yetu haina nguvu za kibunge ina ushawishi mkubwa.

Tutapendekeza na Rais akiyakubali basi anaweza kutumia vyombo vinavyohusika ili kutekeleza mapendekezo hayo,” anasema Jaji Bomani.

Hata hivyo, Jaji Bomani anabainisha kwamba kamati hiyo haikuundwa kwa msukumo wa hoja ya Zitto kwa maelezo kwamba Rais Kikwete, alikwishakuonyesha nia ya dhati ya kupitia mikataba na sheria za madini wakati alipohutubia Bunge kwa mara ya kwanza baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2005.

“Rais alipokuwa anazindua Bunge jipya baada ya uchaguzi wa 2005 katika hotuba yake ya ufunguzi aligusia suala la mikataba na wakati ule Zitto alikuwa hajazungumzia suala hilo. Hivyo si sahihi kusema Kamati hii inatokana na hoja ya Zitto,” alisema Jaji Bomani.

Jaji Bomani alisema Bunge lina uwezo wa kuunda kamati yoyote, juu ya jambo lolote, na wakati wowote ule na hivyo kuundwa kwa kamati ya Rais hakuzuii Bunge kuunda Kamati teule kuangalia suala hili au suala jingine lolote kuhusu madini.

“Kwa kweli hakuna mgongono wowote ule, kwani hata kama ingekuwa ni kamati ya Bunge inayochunguza jambo hilo na yenyewe ingetoa mapendekezo bungeni, na Bunge lingeweza kutunga sheria ambayo utekelezaji wake bado unategemea vyombo vya serikali, hivyo hakuna tatizo lolote kama Bunge litaunda kamati teule baadaye,” alisema.

Jaji Bomani anasema sekta ya madini hasa madini ya dhahabu, haijatoa mafanikio yaliyokuwa yametarajiwa na watu wengi, hivyo kumekuwako na haja ya kuyaangalia ni jinsi gani inaweza kuwa na manufaa kwa wananchi.

“Lolote ambalo lingefanyika lingekuwa ni jambo zuri kwa Tanzania. Hivyo niliona kuwa pamoja na ukubwa wa kazi yenyewe, kuteuliwa kuongoza kamati hii ni kitu cha heshima kuombwa kwa kukifanya. Huo ndio ulikuwa mtazamo wangu,” anasema Jaji Bomani.

Alisema majukumu ya kamati hiyo ni pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali ambayo imetiwa sahihi kati ya serikali na makapuni ya madini hasa makampuni makubwa yaliyowekeza nchini.

“Lengo ni kuona kama mikataba hiyo ina dosari yoyote ile na kama ipo basi tunaishauri serikali ni wapi parekebishwe. Pia tunaangalia ni jinsi gani sekta hii ya madini inaweza kusaidia nchi,” alisema.

Alisema kamati yake itatoa mapendekezo kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na suala zima la kuchimba madini na kutoa mfano wa wananchi wanaoishi maeneo yenye dhahabu na baadaye kuhamishwa kupisha wawekezaji wakubwa.

“Tutatoa mapendekezo ni jinsi gani uhamisho ufanyike kwani kumewahi kuwa malalamiko huko nyuma kuhusu wananchi kuhamishwa katika maeneo ambayo yana madini haya.

Zaidi ya yote tutatoa ushauri juu ya mambo mengine yoyote yale ambayo yatasaidia katika kuifanya sekta hii iwanufaishe Watanzania zaidi,” alisema. Alisema kamati hiyo siyo kamati ya uchunguzi bali ni kamati ya kuangalia upya mambo mbalimbali kama kuhusu sekta ya madini na kuongeza:

“Hatutashughulika kuangalia nani alikosea, wapi alikosea na afanywe nini. Sisi tunaangalia kuanzia hali tuliyo nayo sasa; mikataba tuliyonayo ni hii na inasema hivi, je inafaa iendelee hivyo hivyo, au ifanyiwe marekebisho?

Na kama marekebisho basi ni marekebisho ya namna gani. Hatuingii kwenye kutafuta mchawi. Mambo ya kutafuta nani alifanya nini, sisi hatuendi namna hiyo,” alisema.

Jaji Bomani alisema yeye na wajumbe wa kamati hiyo hawakula kiapo chochote kwa kuwa ni kamati ya ushauri na kwamba kamati hiyo haina nguvu za kisheria ya kumlazimisha mtu yeyote kutoa ushahidi.

“Hatuna nguvu za kuwashurutisha watu. Lakini nakuhakikishia kwamba hilo siyo tatizo. Tatizo tunalokumbana nalo ni kuwa wapo watu wengi ambao wanapenda kuja kutoa ushauri wao. Hivyo hatuhitaji nguvu yoyote kuwalazimisha watu waje kwetu,” alisema.

Kuhusu uwezekano wa watu kutoa taarifa za uongo ama za kupotosha, Jaji Bomani alisema kamati itatumia busara kuyazingatia au kuyapuuza maelezo ama maoni ya mtu wa aina hiyo kazi ambayo alisema haihitaji nguvu ya kisheria.


Source: Raia Mwema
 
Jaji Bomani atetea hoja ya Zitto


I mean, yale yale ya wanasiasa vinyonga, mbona hakusema the next day Zitto aliposimamishwa bungeni? WHY now? Baada ya kuona ishu imepoa hakuna noma, na serikali imekubali kukabwa koo ndio anasema sasa?

Mkuu Zitto, unapaswa kuwa very careful na hawa vinyonga, na hasa this man I just do not trust him, and that is me!
 
Rais alipokuwa anazindua Bunge jipya baada ya uchaguzi wa 2005 katika hotuba yake ya ufunguzi aligusia suala la mikataba na wakati ule Zitto alikuwa hajazungumzia suala hilo. Hivyo si sahihi kusema Kamati hii inatokana na hoja ya Zitto," alisema Jaji Bomani.
Jaji Bomani alisema Bunge lina uwezo wa kuunda kamati yoyote, juu ya jambo lolote, na wakati wowote ule na hivyo kuundwa kwa kamati ya Rais hakuzuii Bunge kuunda Kamati teule kuangalia suala hili au suala jingine lolote kuhusu madini.
Kwa maana nyingine Karamagi alilidanganya Bunge. Bunge likatoa uamuzi wake dhidi ya Zitto lakini rais na wanasheria wetu wote walikaa kimya kupinga uamuzi huo, hata ktk maandamano walionekana walalahoi tu.... siasa za Bongo kali!
 
Mining sector under the microscope: Kiwira coal deal also up for review

-As Bomani committee seeks to make full use of terms of reference

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


THERE are strong indications that the latest government mining sector review committee will also probe the controversial privatisation of the previously state-owned Kiwira coal mine, whose majority shares are now owned by a private company set up by former president Benjamin Mkapa and senior minister Daniel Yona while both were still in public office.

The committee’s chairman, Judge Mark Bomani, made it clear in Dar es Salaam yesterday that the team may look into the Kiwira coal mine issue after concluding its ongoing review of major gold mining contracts in the country.

Responding to a direct query by THISDAY if the committee intended to review the Kiwira coal mine privatisation contract, Bomani said: ’’Right now, we are mainly focused on gold mines. After we conclude this process, our terms of reference give us the liberty to review any other mining contract.’’

He added: ’’We will reach that stage later. And when we do reach that stage, we may summon anyone relevant to our work.’’

The committee’s terms of reference include to review mining contracts and other key documents related to the sector; to evaluate the mining taxation system; and to review the government’s present regulatory system on mining.

The committee will also look into the rights and duties of the government and private investors respectively in mining sector issues; hold talks with the Chamber of Mines and other stakeholders; and make relevant recommendations to the government.

President Jakaya Kikwete has given the Bomani committee three months to conclude its work and submit its much-anticipated report and recommendations for action.

Well-placed sources in government say the committee may expand the scope of its probe by reviewing other contracts pertaining to the mining sector as a whole, apart from the existing Mineral Development Agreements (MDAs) between the state and foreign-owned gold mining companies operating in the country.

Located in Mbeya Region, Kiwira is the country’s only bona fide coal mine, with an average annual output in excess of 35,000 tonnes of the key mineral - most of which is consumed locally for power generation.

Investigations by THISDAY have established that in December 2004, Mkapa and Yona ? while still serving as president and minister for energy and minerals, respectively - jointly registered a private company called Tanpower Resources Company Limited, with various close relatives including wives, children and in-laws in tandem.

At the time of its registration, the first listed directors of Tanpower Resources were the then first lady Mrs Anna Mkapa; Yona himself; Nicholas Mkapa (the then president and first lady’s son); Joseph Mbuna (Nicholas Mkapa’s father-in-law); and one Evans Mapundi.

Among other things, the company was licensed to ’’deal with coal mining in order to generate electricity for consumption and sale; to generate power generators, transmitters and general distributors; and to provide power and general projects management, project appraisers and consultants.’’

It has further been established that Mkapa and Yona - through their positions in government - were also directly involved in the privatisation of the then state-owned Kiwira coal mine. And in mid-2005 - just a few months after its incorporation - Tanpower Resources entered into a joint venture with the government to acquire 70 per cent of the Kiwira coal mine shares. The private company later increased its shareholding in the coal mine to 85 per cent, leaving the government with just 15 per cent.

Nicholas Mkapa - the president’s son - was then appointed to the board of directors of the renamed Kiwira Coal and Power Limited Company, while his father-in-law (Mbuna) became board chairman.

It has also been verified that the privatised Kiwira Coal and Power Ltd was also given control of the Kabulo coal prospect, a nearby but separate area formerly owned by the government, with proven reserves of up to 14 million tonnes of coal. The Kabulo coal deposits were previously under control of the State Mining Corporation (STAMICO), a government-owned agency.

When tabling his ministry’s 2006/07 budget estimates mid-last year, the then Minister for Energy and Minerals, Dr Ibrahim Msabaha, told parliament that the government had concluded negotiations with owners of the Kiwira Coal and Power Ltd company to expand power generation capacity to 200 megawatts by ’’using coal reserves at Kiwira and Kabulo.’’

Dr Msabaha, who has since been moved to the East African Community ministerial portfolio, disclosed in the House that the government, Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) and Kiwira Coal and Power Ltd had in March 2006 signed an agreement of intent for development of the $271.8m (approx. 326bn/-) Kiwira coal-fired power project.


Source: ThisDay
 
Investigations by THISDAY have established that in December 2004, Mkapa and Yona ? while still serving as president and minister for energy and minerals, respectively - jointly registered a private company called Tanpower Resources Company Limited, with various close relatives including wives, children and in-laws in tandem.

At the time of its registration, the first listed directors of Tanpower Resources were the then first lady Mrs Anna Mkapa; Yona himself; Nicholas Mkapa (the then president and first lady's son); Joseph Mbuna (Nicholas Mkapa's father-in-law);


Yaani in bongo jamaa hitwa Mr. Clean, tena na the greatest ever, yaani Mwalimu!
 
Hata tukipitia sheria ya madini kwa sasa,tunachofanya ni kurekebisha yaliyopita na kuganga yajayo. Kwa mujibu wa sheria ya mikataba kwa Tanzania THE LAW OF CONTRACT ACT,1961 mkataba huingiwa kwa hiyari kati ya pande mbili, na ukishahitimishwa(concluded) WENYEWE wanasema it becomes sacrosant yaani ni mtakatifu kwa maana hiyo neither court or any part to it may terminate.si mahakama wala mtu yeyote aweza kuuvunja na kama ukiuvunja unapaswa kulipa fidia upande ulioathirika.Tanzania tutakuwa tu na nguvu ya kubadili mikataba hiyo endapo kwa kuchunguza mikataba hiyo kuna sehemu tunaona kipengele cha Revision yaani kinachoruhusu kupitiwa upya mkataba huo au kufanyiwa ammendment na kama hakuna tumeliwa labda tutume nguvu na tukitumia nguvu hawa bwana serikali zao ndio zinazotufadhili sasa sijui tutafanyeje na ndio maana pamoja na mapepe yote ya JK kwenye vyombo vya habari aliishia tu kuwaomba Barrick watuongezee pesa
Kwa lugha nyingine ni kuwapigia magoti na kusema look tuliingia huu mkataba kwa makosa lakini jamani tumieni ubinadamu tufikirieni kidogo basi.Tulitumia nguvu tunarudi IPTL ambako tulitumia nguvu tukaangukia pua.Kamati itasaidia kuwapata waliosaini hiyo mikataba kuwawajibisha na kutengeneza sheria mpya ili tusirudie kosa hilo hasa ndio tunalofanya.

Ndimi
Augustoons(Augustus)
Student
LLM in International Trade Law
University of Essex
Colchester, Uk
 
Lini mkapa atazungumza? Kwa nini gazeti moja lisijitoe muhanga waandike arrticle ya kumchafua yenye kichwa cha habari "Kumbe Mkapa ni jambazi la kutisha" Tuone kama ataenda mahakamani ili azungumze.
 
Augustoons,
Chavez hakuhitaji mahakama wala sheria... kafanyiza baada ya makampuni hayo kukataa serikali yake kumiliki hisa. Tutaweka mapendekezo yetu mbele walikataa basi inabidi tumtafute Chavez uchaguzi ujao!
Kwa mchango wa 1.9 ktk mfuko wetu nadhani ipo haja kubwa ya kuchukua risk hasa baada ya kuwahukumu Watanzania waliotuingiza ktk mikataba hiyo!..
Usafi tunaanza ndani.
 
Kikwete, Sinclair na Barrick: Pembetatu ya machozi?

Makala ya Lula wa Ndali-Mwananzela

KWA mwaka mzima sasa hakuna kitu ambacho kimegusa hisia za umma wa Watanzania kama suala la madini.

Na kwa namna ya pekee suala hilo la madini lilifikia kilele chake pale mbunge kijana toka Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alipojikuta anapigwa "stop" kwenye Bunge baada ya kudai uundwaji wa Kamati teule ambayo ingechunguza mikataba ya madini na kuona kama "kuna sheria zilizovunjwa" na kuwatambua ni kina nani waliohusika.

Kitendo cha Wabunge wa CCM wakiongozwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waziri mkuu mstaafu John Malecela kumfungia kijana huyo kilisababisha si tu hisia ya uonevu, bali pia hisia ya ukandamizaji kwa kutumia nguvu ya Bunge.

Baadhi ya watu walionekana kukerwa na hali hiyo na wengine wakishikwa na madonge kooni ambayo yaliwafanya hata washindwe kusema. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu wananchi walishuhudia jinsi gani wingi wa wabunge wa chama kimoja bungeni unavyoweza kutumika vibaya kuhalalisha na kuficha mapungufu ya Serikali.

Siku zikapita na miezi ikenda; Na wananchi wakiwa wamekata tamaa Rais Jakaya Kikwete akatangaza kuwa ameunda tume ya ushauri juu ya sekta ya madini ambayo itaongozwa na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa Tanzania Jaji Mark Bomani. Kuundwa kwa kamati hiyo kulipokewa kwa shangwe na baadhi ya watu hasa wale ambao ni mashabiki wa chama tawala wakiamini kuwa hatimaye "Rais kafanya kweli". Na kwa watu wa kawaida habari hizo zilikuwa kama mvua iliyokuwa ikusubiliwa jangwani kwa miongo hasa pale kati ya wajumbe wake lilipotajwa jina la Zitto.

Hata hivyo, baada ya muda kupita na habari sahihi kutiririka, wananchi wakaambiwa kuwa Kamati hiyo si majibu ya hoja ya Zitto bungeni na kwa hakika "haihusiani moja kwa moja" na hoja hiyo ya Zitto.

Jaji Bomani mwenyewe akizungumza na mojawapo ya vyombo vya habari vya nje ya nchi alinukuliwa kukiri kuwa kamati hiyo kimsingi ni Kamati ya ushauri na haina nguvu za "kisheria" kama Kamati ya Bunge na hivyo haina uwezo wa kuita mashahidi au kuwalazimisha kisheria kusema ukweli au kutoa taarifa sahihi.

Wananchi wakiwa wanajikuna vichwa kufikiria mambo hayo wakaambiwa kuwa Kamati hiyo imeanza kuangalia kazi zilizofanywa na Kamati nne zilizotangulia kabla yake. Kwa mara ya kwanza (natumaini ni mara ya kwanza) ndani ya wiki chache Serikali ikaunda Kamati kuangalia kamati nyingine bila kuondoa uwezekano kuwa huko mbele kamati nyingine itaundwa kuangalia kazi za kamati iliyoundwa kuangalia kazi za Kamati nyingine! Watanzania waliokuwa wamejawa na matumaini kama walivyotumaini ushindi wa Taifa Stars, wakajikuta wamefungwa goli la kutolewa Challenji!

Kitu kimoja ambacho Watanzania wengi hawajakifahamu au hakijawekwa hadharani inavyopasa ni sababu kubwa kwa nini Rais Kikwete hawezi na hatoweza kamwe kusafisha sekta ya madini nchini. Nia yake ya kutaka tuwe na kile anachokiita "win-win situation" haiwezi kukamilika na haitatokea kwa sababu yeye mwenyewe ni mdau kwa namna moja au nyingine na hali iliyopo sasa (status quo).

Hivyo wale wanaokaa wakiwa wanatumaini kuwa mapendekezo ya Kamati ijayo YOTE yatafanyiwa kazi na yatachangamkiwa, huyo bora ajiandae kukata tamaa na kushika tama. Kwanza kabisa mapendekezo yote hayatawekwa hadharani; kwa sababu ni mapendekezo tu na hiyo tume haitakiwi iyaweke mapendekezo yake hadharani bali kuyawasilisha kwa Rais kwanza na Rais halazimiki kuwaambia ni nini kimependekezwa.

Jambo la pili hata kama ataamua kutekeleza baadhi ya mapendekezo maslahi ya kwanza atakayoangalia na ambayo hadi hivi sasa ameyaangalia ni maslahi ya "wawekezaji" ili tusiwatishe. Hivyo mapendekezo yoyote ambayo kwa namna moja au nyingine yatatashia uwekezaji katika sekta ya madini yanakufa kabla hayajafika kwenye deski la Rais ofisini kwake.

Kwa kadiri Serikali ya Rais Kikwete inavyojaribu kutengeneza mizani ya mafanikio kati ya wawekezaji na wananchi kuwa ni lazima iwiane kwa hakika wanakuwa kama watwangao maji kwenye kinu. Je, ni lazima manufaa ya wawekezaji yalingane na manufaa ya wananchi wa nchi/maeneo ambapo wawekezaji wanafanya biashara zao?

Kwa kadiri ilivyo sasa inaonekana wazi kabisa kuwa wanaonufaika na uwekezaji ni makampuni na wananchi wanapata "viperemende" vya shule, zahanati n.k Je, yawezekana kupindua modeli hiyo na kuhakikisha kuwa mafanikio ya wananchi yanazidi yale ya makampuni?

Hata hivyo, kuna sababu nyingine na kubwa zaidi ambayo inamfanya Rais Kikwete kuwa na kigugumizi na wakati mwingine kusita kuchukua hatua za kijasiri, madhubuti, na zenye lengo kamili kuibadilisha sekta ya madini. Jambo hilo ni lile ambalo naweza kuliita ni pembetatu ya machozi. Pembetatu hii inamhusu Rais Kikwete mwenyewe, rafiki wa miaka 13 sasa James Sinclair, na kampuni kubwa kabisa ya uchimbaji dhahabu duniani ya Barrick Gold (kutoka Canada).

Kuweza kukaa chini na kuielewa pembetatu hii ndiyo mwanzo tu wa kuelewa ni kwa nini Rais Kikwete licha ya ahadi zake kuhusu mabadiliko katika sekta ya madini hawezi, hatoweza na hana sababu ya kuweza kubadilisha sekta hiyo ili iwe na manufaa zaidi kwa wananchi.

James Sinclair aliingia nchini akiwa na kampuni ya Sutton Resources na alianza shughuli zake za utafiti na uchunguzi wa madini. Baada ya kugongana na bodi ya wakurugenzi wa bodi hiyo Sinclair aliachana (alilazimishwa kuacha?) nayo na kuamua kuanzisha kampuni yake ya Tan Range Exploration iliyotokana na kampuni yake nyingine ya Tanzanian American Development.

Kampuni hii ya TRE liingia nchini ikiwa na lengo la kufanya ugunduzi wa madini mbalimbali (hasa dhahabu) na baadaye inapogundua eneo lenye madini hayo basi huliuza kwa makampuni makubwa ya uchimbaji madini na wao huanza kulipwa kiasi cha fedha kutokana na uchimbaji utakaofanywa pale. Kimsingi kampuni hiyo ya Sinclair haifanyi uchimbaji wa biashara bali wa utafiti na baadaye wakigundua madini basi hujitangaza kwa makampuni makubwa. Kampuni hii ina mikataba mbalimbali na baadhi ya makampuni na mkubwa zaidi ni ule kati yake na kampuni ya Barrick Gold ya Canada ambao wanaupendeleo maalum pale ambapo TRE wanagundua madini.

Akiwa na kampuni ya Sutton Resources Sinclair ndiye aliyesimamia utafiti wa eneo la machimbo ya Bulyanhulu ambayo kama wengi wanavyofahamu yanahusisha kuondolewa kwa nguvu kwa wachimbaji wadogo wadogo na madai ya kuwa baadhi yao walifukiwa wakiwa hai. Ni uhusiano huu ndio ulioifanya Sutton Resources kuuza machimbo hayo kwa Barrick Gold. Na kama nilivyosema hapo juu, kampuni yenyewe ya Sutton baadaye ikanunuliwa na Barrick.

Kuingia kwa Sinclair katika Tanzania kulikuwa kumepigiwa mahesabu ya kina na kubwa zaidi ni kujenga uhusiano wa karibu na wanasiasa na wadau wakubwa wa sekta ya madini. Yeye na binti yake, Marlene, wakaingia Tanzania mmoja akijenga uhusiano na wanasiasa na binti akijushughulisha na shughuli za kijamii. Lengo lao, hata hivyo, likiwa moja tu nalo ni kulainisha nyoyo za Watanzania ili hatimaye watakaposema wanachotaka wanapata.

Kuelewa upendeleo huu ni kuelewa kuwa wakati kampuni ya TRE inabadilishwa kutoka Tan Range kampuni ya Barrick Gold ilinunua hisa za mtaji kwenye kampuni hiyo mpya na hivyo kusaidia katika kuanza kwake. Pamoja na ushirikiano wa kibiashara na Barrick kampuni ya TRE ina ushirikiano na makampuni mengine ya uchimbaji ambayo yanafuatilia shughuli kwa uangalifu.

Leo hii TRE ni mojawapo ya makampuni/watu wachache wenye kumiliki eneo kubwa la ardhi. Ikiwa na leseni zaidi ya 120 za uchunguzi kuzunguka eneo la Ukanda wa Ziwa Victoria, kampuni hii kwa wengine inaonekana ndiyo kiini cha matatizo ya madini katika eneo hilo kubwa hasa kutokana uhusiano wake na kampuni ya Barrick Gold.

Kampuni ya Barrick Gold imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa sehemu mbalimbali duniani kama Australia, Chile, Argentina, na Peru. Kitu kimoja ambacho hadi hivi sasa ni dhahiri ni kuwa kile ambacho Barrick inataka, Barrick inapata.

Katika kuhakikisha kuwa hilo linafanikiwa Tanzania, James Sinclair alijitahidi kuwa na urafiki wa karibu na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini kati ya miaka ya 1990, Jakaya Kikwete. Kwa mujibu wa mmojawapo wa wasaidizi wa karibu wa Sinclair ukaribu wake na Waziri Kikwete ulijenga uhusiano wa karibu, kuaminiana na uwazi zaidi na matokeo yake ni urafiki ambao yeye mwenyewe Sinclair anauita ni wa "Karibu". Urafiki huo ulidhihirishwa pale Rais Jakaya Kikwete alipomualika Sinclair katika sherehe za kuapishwa kwake!

Pembetatu hii inaendelea kuzunguka kila wakati na hasa hivi karibuni ambapo Rais Kikwete alirejea kutoka katika ziara yake ya "kikazi" ya ki Vasco Da Gama huko Marekani. Ziara hiyo ya Rais Kikwete ilitokana na mwaliko wa Mwenyekiti wa Bodi ya H. Sullivan Summit Balozi Andrew Young. Balozi Andrew Young ni mtu ambaye katika jamii ya watu Weusi wanamuona kama ni shujaa ambaye alishirikiana na marehemu Dk. Martin Luther, siku hizi ameanza kuonekana kwa mwanga mpya na tofauti.

Kuna baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa Balozi Young amekuwa ni "mbeba mifuko ya ubepari wa Marekani" hasa kwenye nchi za Afrika. Imani ambayo imekuwa ikijengeka siku za karibuni kuwa Balozi Young amenunuliwa na anatumika kama kibaraka wa ubepari na hajali mambo mengine yoyote isipokuwa kutengeneza pesa kupitia migongo ya Waafrika.

Leo hii Andrew Young amepigia debe mkutano ujao wa Sullivan ufanyike nchini Tanzania jijini Arusha. Pamoja na sababu nyingi, bila ya shaka, Young atatengeneza ngawira kidogo. Kampuni ya Young inahusika moja kwa moja na umiliki wa hoteli ya Mt. Meru mjini Arusha.

Lakini zaidi ya yote, Young ni mjumbe wa bodi ya Ushauri ya kampuni ya Barrick Gold. Hivyo bila ya shaka uhusiano wake wa karibu na Rais Kikwete, Waziri wa Madini Nazir Karamagi, Sinclair na watu wa Barrick unamsaidia sana katika kuhakikisha kuwa mambo hayaendi vibaya kwa Barrick hasa yanapokuja kwenye maamuzi ya Serikali.

Kwa kuangalia mambo hayo tunaweza kuona pembetatu ambayo ndani yake kuna mambo mengi ambayo kwa hakika yameshikamana na kufuatana kama lila na fila. Tunaweza kuona jambo moja dhahiri kuwa Rais Kikwete, Kamaragi, James Sinclair, na Andrew Young wote wanaunganishwa kwa namna moja au nyingine na kampuni kubwa kabisa ya madini duniani ya Barrick Gold. Na tukiangalia mifano ya nchi mbalimbali ambako Barrick imekuwa ikilalamikiwa na kupata upinzani tunaona kuwa Barrick haiko katika upande wa kushindwa.

Hakuna sheria au taratibu ambazo zinaweza kutengenezwa na nchi yoyote inayoendelea ambazo zinaweza kuweka matatani maslahi ya kampuni hiyo kubwa ya madini. Kile ambacho Barrick inataka, Barrick inapata.

Kwa kuangalia ukweli huo basi ni wazi kuwa kikwazo kikubwa cha mabadiliko katika sekta ya madini itakuwa ni kampuni hiyo kwani wao wakigoma hakuna kitakachofanyika. Ndiyo maana kutokana na pembetatu hiyo ilikuwa ni rahisi kuishawishi kampuni hiyo kubadili baadhi ya vipengele vya mikataba yake kiasi cha kwamba walikuwa ni wa kwanza kutangaza "kukubali" mapendekezo ya Serikali (ambayo wao wana uhusiano wa karibu nao).

Pembetatu hii kwa hakika imesababisha Watanzania walie sana mwaka huu unaoisha na sitashangaa wakawa tena sababu ya machozi zaidi mwaka ujao. Rais Kikwete hana ubavu wa kusimama mbele ya kampuni kubwa kama hii hata kama atapata ushirikiano kutoka kwa wananchi. Barrick imekuwa ikitamalaki sehemu mbalimbali duniani licha ya pingamizi toka kwa watu mbalimbali.

Ndiyo maana watu kama kina Tundu Lissu wanavyojitahidi kupambana na kampuni hii wanakuwa wamejiweka katika kundi la kushindwa. Tundu Lissu hana ubavu wa kupambana na kampuni iliyozungukwa na pembetatu hii. Kamati ya Madini ya Bomani haina ubavu huo pia kwani haina nguvu zozote na Rais Kikwete alijua ni kwa nini hakutaka iundwe kamati Teule ya Bunge isipokuwa kamati ya ushauri tu; ushauri ambao watekelezaji wake wakubwa watakuwa ni Barrick Gold.

Ni kwa sababu hiyo basi yeyote ambaye amekaa kwa moyo wa matumaini kuwa kuna mabadiliko makubwa katika sekta ya madini huko tunakokwenda yuko njozini. Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana hadi leo Serikali imeshindwa kutoa hadharani ripoti za Dk. Kipokola, Mang'enya, Jenerali Robert Mboma na Laurence Masha.

Kwa sababu mapendekezo hayo hayakukubaliwa na "wakubwa". Hata mapendekezo ya kamati ya kina Zitto ambayo ninaamini yatakuwa mazuri sana yatatupwa nje kama takataka chafu kwani Barrick haiwezi kufanya katika Tanzania kile ambacho imekataa kufanya nchi nyingine.
 
Sheria zinatakiwa zituongoze sio zitutawale, kama sheria zetu ndio zinatumika kutunyonga tukikaa na kusema "hatuna nguvu ya Kisheria" tutaendelea kuwa wajinga. Something can be done!
Kama ukweza kuangalia unaweza kuona ni jinsi gani IPTL wanakunywa pesa zetu, sasa hivi wa madini wanaendelea, na sijui hao Dowans na wengineo, watu wanakwapua tu wanaondoka halafu watu tunalalamikia sheria, what the heck!
 
Afu sheria zenyewe ni zetu, si kwamba ni msaafu ama biblia zimeshushwa toka mbinguni!! kwanini tusizerekebishe ili zitunufaishe??
 
Na Zuhura Waziri, Nzega

BAADHI ya viongozi wa Serikali wilayani Nzega mkoani Tabora, wameeleza wasiwasi wao juu ya kuwapo kwa wizi wa rasilimali za Taifa hususan madini, unaofanywa na wawekezaji katika migodi nchini.

Akitoa maoni yake juzi mbele ya Kamati ya Rais ya kupitia Mikataba na Sera ya Madini chini ya uenyekiti wa Jaji mstaafu Mark Bomani, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Dkt. Charles Kizeba, alisema pamoja na udhibiti mkubwa wa matumizi ya anga na taratibu zilizopo, lakini kuna mazingira yanayoashiria kuwa viwanja vya ndege migodini, hutumika kusafirisha madini kimagendo.

"Taratibu na sheria ni kitu kimoja, tuhuma ni kitu kingine, hizi ni tuhuma zinazogusa uhai wa Taifa, zifuatiliwe, haitoshi kusema hakuna kitu kama hicho kwa kuwa tuna sheria ... itakuwa kwa faida ya nani ... wanachukua mali hawa jamaa, wanaohusika wafuatilie," alisema Dkt. Kizeba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Sikonge.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Nijanija wilayani hapa, alisema hakuna shaka juu ya tuhuma hizi kuwa ndege zinaingia na kutoka na madini na mbaya zaidi hata mchanga unachukuliwa unapelekwa kusikojulikana.

"Hii si siri tena, imetokea hapa Nzega watoto wetu wamekamatwa na mchanga kwenye madebe tu wametajirika, je huu ukijaa kwenye makontena si mabilioni ya pesa ... nasema ninyi waandishi andikeni haya tunakuwa maskini kabisa juu ya ardhi ambayo chini imejaa dhahabu, inauma sana hii," alisema huku
akiwanyooshea kidole waandishi waliokuwa wakimsikiliza.

Masuala mengine yaliyoibuka katika mjadala huo ambao ulihudhuriwa pia na Mbunge wa Nzega, Bw. Lucas Selelii na madiwani, viongozi hao walieleza kutoridhishwa na kiwango kidogo cha fidia kinacholipwa kwa wananchi, kama
fidia kwa nyumba na mali zao, kama njia ya kuwaondoa kwenye maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa uchimbaji madini.

Jambo lililochukua muda katika mjadala huo wa ndani wa viongozi na Kamati hiyo ni kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo kutotoza tozo la dola 200,000 kwa mgodi wa dhahabu wa Resolute (T) Limited tangu mwaka 2003 ilipopitishwa
Sheria namba 15 ya fedha ya Bunge inayotoa uwezo kwa halmashauri kutoza kodi migodi dola zisizozidi sh. 200,000 kila mwaka. Hata hivyo hadi mwaka uliopita, halmashauri ya wilaya ya Nzega ilipewa gawio la kodi kwa mara ya
kwanza.

"Wataalamu wanatuambia kuwa hatukudai, hatukupeleka 'invoice' kudai katika mgodi, tungejuaje kuwa sheria inatutaka tudai bila kuelezwa mkataba unasemaje? Serikali na hasa wizara ndio imezembea ... iliamini tutajua tu,
tutajuaje sasa? Na sasa tunajiuliza tutazipataje fedha zetu?," alihoji afisa wa Serikali wilayani humo na kuomba asiandikwe gazetini.

"Ndugu zangu msikate tamaa, fuatilieni mpaka mwisho mpate malimbikizo yenu...ni mali yenu na sisi tutawasaidia kumfikishia Rais Kikwete kuwa kuna tatizo hapa," alisema mmoja wa wanakamati, Bw. John Cheyo na kueleza kukerwa na jambo hilo.
 
Back
Top Bottom