Mihimili ya Kenya wanaiga nchi za ulimwengu wa Kwanza sisi tunaiga mfumo wa Burundi. Jaji Mkuu kamkaripia Rais uteuzi wa Majaji

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Jaji Mkuu wa Kenya amemtaka Mhe. Rais wa Kenya kuheshimu sheria na kite majaji sita wanaohitajika kikatiba. Aidha amesisitiza kuteuliwa kwa majaji wawili walimpinga wakati wa BBI. Hii ni mwendelezo wa uwajibikaji wa Jaji Mkuu kama mkuu wa mihimili. Jaji Mkuu aliyemaliza muda wake itakumbukwa alisimamia haki na kupelekea Uchaguzi Mkuu uliogubikwa na makosa mbambali kufutwa wakati Kenyatta akigombea awamu ya pili.

Hapa kwetu Tanzania Jaji Mkuu ni mshiriki wa hafla za Rais na kila anapopewa nafasi usimama kama sehemu ya serikali siyo mahakama. Leo pia tumeshuhudia Tulia ACksoni akiweka taaalum yake pembeni na kutumisha Mkuu wa nchi awezi kukosolewa na Bunge na likitaka kukosoa serikali litakosoa kwa staha. Ukitafuta tafsiri Hii mwenye sheria haipo means Spika naye nisehemu ya serikali kama ilivyo Burundi. Je tutafika HUKO ulimwengu wa Kati?

Kumbuka Tanzania huwezi kumkosoa aliyekuzidi umri hata akikosea kwa sababu utaambiwa iumekosa nidhamu, huwezi mkosoa kiongozi wa kisiasa na ni marufuku kumsema vibaya Mkuu wa Nchi na hiyo kumsema vibaya siyo suala universal Bali yeye na wateule wake ndio wanaoamua ni wakati Amesemwa vibaya na wakati gani amesemwa vizuri.
 
Back
Top Bottom