Miguna Miguna athibitisha kurejea Kenya baada ya Rais Ruto kumpa kibali

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1663071970183.png

Wakili aliyehamishwa Miguna Miguna ana kila sababu ya kutabasamu baada ya Rais William Ruto kuondoa arifa nyekundu zilizotolewa dhidi yake.

Katika taarifa yake mnamo Jumanne, Septemba 13, wakili huyo alibainisha kuwa alipokea hakikisho kutoka kwa Amiri Jeshi Mkuu kuhusu hali yake ya uhamishoni.

Alifahamishwa kuwa arifa hizo nyekundu zingeondolewa kufikia Jumatano, Septemba 14 - saa 24 baada ya Ruto kuchukua wadhifa wa Rais wa tano wa Kenya.

Miguna zaidi alibainisha kuwa baada ya hakikisho hilo, ameweka mipango ya kurejea katika nchi yake ya asili.

“Nina furaha kutangaza kwamba Rais William Ruto amenihakikishia kwamba arifa hizo nyekundu zitaondolewa Jumatano, Septemba 14, 2022.
"Baadaye, nitafanyiwa upya Pasipoti yangu ya Kenya na nitatangaza tarehe ya kurudi kwangu katika nchi ya mama yangu. Bravo!" alitangaza Miguna.

Masaibu ya wakili huyo yalianza Machi 2018 alipohamishwa hadi Kanada kwa kuendesha hafla ya kuapishwa ya kinara wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Tangu wakati huo, Miguna, ambaye ana Uraia wa Kanada pamoja na ule wa Kenya, aliingia katika mzozo na Serikali ya Kenya katika jaribio lake la kurejea kwa ndege.

Katikati ya Agosti, mkosoaji mkubwa wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta aliapa kwamba angekanyaga Kenya baada ya kuapishwa kwa Rais Ruto.

Pia alitaka arifa hizo nyekundu ziondolewe na hati yake ya kusafiria ya Kenya iongezwe upya - akionyesha kwamba alikuwa amefungasha virago vyake tayari kwa safari ya saa 15.

"Kwa wazalendo wote: Tulieni. Asante kwa mshikamano. Ndiyo, nimefunga virago na niko tayari. Lakini kabla sijaweza kuchukua ndege yangu kurejea nyumbani, William Samoei Ruto lazima kwanza aapishwe kama Rais. nimeinuliwa na pasipoti yangu ya Kenya kufanywa upya. Tutaonana hivi karibuni. Cheers!" alisema wakati huo.
Ahadi ya Ruto

Wakati wa ziara yake nchini Marekani, rais mteule awali alikuwa amethibitisha kwamba utawala wake ungemrejesha wakili aliyehamishwa katika muda mfupi iwezekanavyo.

"Tutamrejesha nchini Miguna Miguna ndani ya muda mfupi iwezekanavyo. Hii ni kwa sababu yeye ni Mkenya na hata kama amefanya uhalifu, tuna sheria ambazo angefunguliwa mashtaka. Sioni haja yoyote kuwa na wakimbizi kutoka mataifa mengine huku sisi wenyewe ni mkimbizi katika nchi nyingine," Ruto alisema wakati wa ziara hiyo.
 
Back
Top Bottom