SI KWELI Naibu Rais Kenya adai kusalitiwa na Rais Ruto baada ya kukutana na Odinga nchini Uganda

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
gachagua.jpg

Video hii kwenye Facebook imeeleza kuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amesema kuwa Rais William Ruto alimsaliti kwa kukutana na kinara wa upinzani Raila Odinga nchini Uganda.

Video hiyo ilikuwa na ujumbe kuwa “Ruto amenisaliti! DP Gachagua anazungumza baada ya Ruto na Raila kukutana Uganda jana,”
 
Tunachokijua
'Ruto amenisaliti', ni kauli inayoweza kutumika kujenga msingi wa taarifa hii iliyosamba kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kutolewa na Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, akimtuhumu Rais wa Kenya William Ruto.

Kauli hii inatoka Februari 27, 2024, siku moja baada ya Ruto kukutana na hasimu wake mkubwa wa Kisiasa, Raila Odinga, kwenye Shamba la Mifugo ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Ukweli wa Madai haya
Kufuatia utafutaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia Googe Image Search, Picha inayofanana na hii ilichapishwa kwa mara ya kwanza Septemba 10, 2023 kwenye mtandao wa Facebook ikiwa na maneno yanayotoa dhihaka kwa Raia Odinga.

Aidha, siku Gachagua anarekodiwa video hii alikuwa pamoja na William Ruto huko Laare, Kauniti ya Meru kwenye ibada moja kanisani. Ushahidi wa video umewekwa hapa, hapa na hapa.

Ikumbukwe kuwa Akaunti rasmi ya Mtandao wa Facebook ya Rais Ruto ilionesha Mbashara ibada hii, na JamiiCheck imefuatilia maneno ya Naibu Gachagua na kubaini kuwa hakutamka kile kinachotajwa kwenye madai kama yalivyowekwa na mtoa hoja.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom