Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Mgomo kesho unafanyika chuoni hapo kutokana na ukandamizaji unaofanywa na menejimenti ya chuo kwa wanafunzi chuoni hapa. Prof mmoja anaitwa Mlacha ndo chanzo cha matatizo yote, hana utu, yeye kwake pesa ndo utu. Wanafunzi wamechoshwa na ukandamizaji wake. Hashauliki huyu bwana. Sasa kazi inaanza kesho na ole wake watoto wa maskini wana hasira sana nae.

- ukandamizaji wa aina gani unaofanywa na menejiment ya hicho chuo?
- Na je menejiment ya hicho chuo nina mtu mmoja tu (Prof uliyemtaja?)
- je kutokushaurika ndio ukandamizaji wenyewe?
- kabla ya kuamua kufanya mgomo hatua gani za awali mmeshachukua juu ya huo "ukandamizaji"?
- so kwa vile hao watoto wa masikini wana hasira na huyo mlengwa uliyemtaja hapo juu kunajustify kufanya mgomo?
 
.....utakuta ni njaa tuu na ubabe wa kishenzi,wanafunzi njaa walimu njaa utawala njaa..basi wakiletewa vipesa kutoka serikalini ni kukandamizana tuu...wanafunzi wajifunze kutumia mahakama labda kutaleta kuheshimiana kidogo kuliko migomo!
 
Matatizo ya Udom na Mlacha ni: 1. Chuo kimegoma kusajili mwaka wa kwanza hadi walipe % wanazotakiwa kuchangia wakati mikopo haijaja na wengine hawajui hata wamepata % ngapi kutoka loan board. Wakati huo uongozi hautaki hata wanafunzi walipe kwa awamu licha ya serikali ya wanafunzi kuomba fursa hio. Pili, pesa ya mkopo imekuja kwa baadhi ya wanafunzi lakini hadi leo hii kuwalipa imekuwa taratibu mno wakati njaa inataka kuua watu. Wakati wa kukusanya direct costs za chuo kutoka kwa wanafunzi, zoezi hilo lilifanyika hadi usiku, lakini kulipa wanafunzi hela zao inatumika saa moja au mawili kwa siku, then mhasibu anaondoka. Wiki ya 3 sasa hela zipo kulipa shughuli. Tatu, waziri kabaka alitangaza kuwa wote wenye bima ya afya wasilipishwe pesa ya matibabu sh laki moja, uongozi wa chuo umeamua kupuuza bima za afya za wanafunzi. Nne, haupewi funguo ya chumba Udom hadi ulipn laki 3 na 25 elfu au laki 2 na 44 elfu kama direct costs ikiwemo pesa ya accomodation shs 751 ya chumba kwa siku. Chuo hakitaki hata kupunguza bei hio kubwa wakati hata Udsm ni nafuu. Kuna kitu gani special kwenye vyumba vya Udom ambacho hakipo vyuo vingine hadi bei iwe kubwa kiasi hicho? Sasa serikali kwa mda wa wiki 2 imefanya chini juu kuongea na uongozi lakini imekwama. MlACHA yeye ni deputy vice chancellor, xeye ndo kila kitu hapa, fedha, utawala usajili yeye. Na tunasikia kwamba yeye anawatisha hata walimu wenzake kuwa yeye hakuomba kazi hapa udom ila aliteuliwa na Kikwete. Kwa hio anafanya anavyotaka. Sasa maisha ni magum sana hata kusoma hakuna tena, hata walim wengi hawafundishi kwa sababu ya Mlacha.
 
Sasa kwa nini msiibane bodi ya mikopo.

Kumbe Mlacha hapokei pesa, basi mgewagomea hao wahasibu wanaojali sana kupokea

Habari ya vyumba inahusikaje direct na Mlacha? je hakuna mgawanyo wa madaraka hapo Udom kiasi ambacho VC anaingia direct katika sakata la vyumba? Nilidhani mngeenda kushtaki kwake kwa vyumba ni soo! Kwani ni lazima mlipie chumba malipo sawa na malipo ya udsm?

Kuhusu Malipo ya ada, ingekuwa vizuri kama chuo kingekubali malipo ya awamu, lakini na Mlacha anaingiaje kwenye hili hadi mumkomeshe?

Watoto jaribuni kujua sheria na kuzifuata, hii migomo migomo hii itawapeleka pabaya....... sio lazima mgomo ili muonekane na nyie ni wanafunzi wa chuo!!!
 
Kweli mgomo siyo suluhu ya matatizo mengi lakini pia huweza kutumika kama last resort kama njia nyingine zote za majadiliano zimeshindwa. Ushauri wangu kwa wanachuo wa Dom University ni kushinikiza kukaa na uongozi wa chuo ili muweke wazi matatizo yenu.... Orozesheni matatizo yenu na jinsi mnavyopenda yatatuliwe... then sikieni upande wa pili utasemaje.

Ikishindikana njia ya mazungumzo ndipo mwaweza anza kunji lenu. Katika maelezo yake yote mawili ya motoyambongo, thread na post, hakuna sehemu yeyote inayoonyesha kulikuwa na jitihada za mazungumzo! Sema nao.
 
Chuo cha JK nako wanagoma, au ndio mzimu wa Mwankupili?

Walizoea kusema UDSM ndo wakorofi na wahuni wasiojua kutumia diplomasia kutatua matatizo yao.Leo Chuo cha JK Chancellor Mkapa na wabunge wanakitambua ndo wanagoma.Makubwa.
 
Sasa kwa nini msiibane bodi ya mikopo.

Kumbe Mlacha hapokei pesa, basi mgewagomea hao wahasibu wanaojali sana kupokea

Habari ya vyumba inahusikaje direct na Mlacha? je hakuna mgawanyo wa madaraka hapo Udom kiasi ambacho VC anaingia direct katika sakata la vyumba? Nilidhani mngeenda kushtaki kwake kwa vyumba ni soo! Kwani ni lazima mlipie chumba malipo sawa na malipo ya udsm?

Kuhusu Malipo ya ada, ingekuwa vizuri kama chuo kingekubali malipo ya awamu, lakini na Mlacha anaingiaje kwenye hili hadi mumkomeshe?

Watoto jaribuni kujua sheria na kuzifuata, hii migomo migomo hii itawapeleka pabaya....... sio lazima mgomo ili muonekane na nyie ni wanafunzi wa chuo!!!

Kwanza shikamoo!
Nakuunga mkono kwa kweli maana hiyo menejimenti ya hiko chuo pamoja na sifa zote walizopewa na Jk kwenye hotuba yake hiko chuo kinachukuaje wanafunzi wengi kiasi cha kwamba hamna hata rooms za accomodation.

I think hawa wanafunzi hawajui who they are against maana they are supposed to fight the menejimenti maana menejimenti is not about one person na suala la bodi ya mkopo linauhusiano gani na huyo Prof?

Huyu mtu aliyeanzisha hii mada nadhani alipaswa aseme kwamba wanafunzi wanagoma kuhusiana na boom and ohter factors siyo Prof whatever!
 
Kama sikosei mtu huyu anaripoti tu yanayoendelea pale chuoni lakini naona kama kuna direct attack kwake kutoka kwa baadhi ya wachangiaji.
Hapo atakuwa atendewi haki.
Lakufanyika nikuwashauri wanafunzi watumie mgomo kama hatua ya mwisho kabisa baada ya kushindwa kufumbua matatizo kwa njia zingine zote ikiwamo na mahakama.
 
Nyie Wanafunzi wa Ugogoni,
Jaribuni kuwasiliana na viongozi wa UDSM, Mzumbe na vyo vingine. Muulizie uzoefu wao katika matatizo kama haya. Mkiweza kuchangishana na kutafuta mwana sheria pia itakuwa safi sana. Katika hii ya sheria mnaweza hata kutafuta wanafunzi wa sheria wa UDSM kama watakubali basi mmoja mumpelekee tiketi aje Dodoma na kusikia matatizo yenu. Mwisho kama sikosei kuna umoja wa Vyuo vikuu. Viongozi wenu watafute msaada kutoka kwa viongozi wenzenu juu.
Katika yote hayo, la muhimu ni kuwa MIGOMO au MGOMO uwe ni hatua ya mwisho.
Wakati manajadili, wekeni pembeni HASIRA. Mkitumia hasira MMEKWISHA. Jaribuni na au niseme LAZIMA mfanye JUU CHINI kujua ADUI yenu ni nani na Makosa yake ni yapi na Muwajibikaji wa hayo ni nani. Pia mjue HAKI yenu iko wapi. Nafikiri ni heri hata KUANDAMANA siku ya JUMAMOSI au Jumapili ili kutangaza matatizo yenu na kuomba msaada. (Mgomo iwe LAST OPTION x70).
 
Nimessikia wamegoma leo
Namuonea huruma huyu waziri wa hii wizara kwani kuna mgomo mwingine wa TAHLISO unakuja mwezi huu
 
Nimessikia wamegoma leo
Namuonea huruma huyu waziri wa hii wizara kwani kuna mgomo mwingine wa TAHLISO unakuja mwezi huu

Kwani waziri ana shida gani? Tuwaonee huruma watoto wetu wanaokosa elimu na kunyanyasika kutokana na mifumo mibovu. Pamoja na kwamba kamwe siungi mkono mgomo wa aina yoyote, nadhani wakati umefika kwa viongozi katika vyuo vyetu kupewa mafunzo madhubuti kuhusu namna ya kusimamia mifumo ya elimu ya juu, maana hii ndiyo chanzo cha vurugu zote. Kila wakati wanafunzi wanagoma, zinatumika mbinu za "zima moto" kutatua tatizo kwa muda tu, na baadae yaleyele yanarudiwa tena kama si chuo hichohicho, basi chuo kingine!
 
Wana haki kabisa kugoma.
Kama hawatendewi haki zao za msingi wanazo dai njia sahihi ni kugoma tu.
 
Siku hizi watanzania wana hobby ya kugoma
Si hobby Shy hapana ni kuonyesha ni kiasi gani wajieleze kwa kuwa wakijieleza kwa njia ya kawaida hakuna anayesikiliza kwa kuwa viongozi wetu wamejaa dharau na kupandisha mapega juu kwa majivuno.
Hapa Tanzania ukichaguliwa kuwa kiongozi wewe unajiona ni mungu mtu.
 
Mgomo kesho unafanyika chuoni hapo kutokana na ukandamizaji unaofanywa na menejimenti ya chuo kwa wanafunzi chuoni hapa. Prof mmoja anaitwa Mlacha ndo chanzo cha matatizo yote, hana utu, yeye kwake pesa ndo utu. Wanafunzi wamechoshwa na ukandamizaji wake. Hashauliki huyu bwana. Sasa kazi inaanza kesho na ole wake watoto wa maskini wana hasira sana nae.

Enzi zetu huyu alikuwa anafungiwa kwenye gunia na kuchapwa viboko tu bila kumdhuru na kumwachia. kwikwikwikwikwi
 
Kwani waziri ana shida gani? Tuwaonee huruma watoto wetu wanaokosa elimu na kunyanyasika kutokana na mifumo mibovu. Pamoja na kwamba kamwe siungi mkono mgomo wa aina yoyote, nadhani wakati umefika kwa viongozi katika vyuo vyetu kupewa mafunzo madhubuti kuhusu namna ya kusimamia mifumo ya elimu ya juu, maana hii ndiyo chanzo cha vurugu zote. Kila wakati wanafunzi wanagoma, zinatumika mbinu za "zima moto" kutatua tatizo kwa muda tu, na baadae yaleyele yanarudiwa tena kama si chuo hichohicho, basi chuo kingine!

Nakuunga mkono Kithuku, pamoja na hayo pia viongozi wetu (wakiwemo mawaziri, mameneja, maprofesa etc) wanatakiwa wajue kwamba wao sio Mungu na vilevile wanahitaji kugawa madaraka na kusikiliza ushauri wa watu wengine kwa manufaa ya walengwa. Jambo ambalo viongozi wetu wanatakiwa walikumbuke ni kuwa "Kidole kimoja hakiuwi chawa" na "Cheo ni dhamana" basi tusijirundikie madaraka na kujiona 'untouchable' tukubali kurekebishwa, kukosolewa na pia kuongoza kwa busara na sio jazba. Tukumbuek kuwa cheo ni dhamana hata kama hukuomba ni Rais amekupa ( hope amekupa kwa utendaji mzuri na sio vinginevyo) basi kitumie cheo hicho vizuri hizi damu za hawa watu tusiowatendea haki zitakuja kudaiwa mikononi mwetu. Just be a human being and not a monster for the sake of other people! Inauma sana kusikia matatizo wanayopata wanafuzni wa elimu ya juu Tanzania hivi sasa, hakuna mtu aliomba kuwa maskini na kutegemea mikopo ya serikali ila ni watanzania wangapi wanaoweza kuwasomesha watoto wao bila mkopo? basi tusiwanyanyase na kuwafanya hao wanafunzi wajione wanyonge ilhali wanajitahidi kujikomboa kimaisha na kujitegemea siku za usoni.
 
Wana haki kabisa kugoma.
Kama hawatendewi haki zao za msingi wanazo dai njia sahihi ni kugoma tu.

swali ni je wamedai hiyo haki kwa njia inayeeleweka? Sawa viongozi wetu ni vichaa, kwa hiyo kichaa akigombana na wewe kwa kuvua nguo na wewe unavua? la hasha, unafikiri, unajaribu njia mbadala, ila inaposhindikana basi ndio unagoma. ila mwandishi ameshimdwa kulipoti knjia zilizotumika kabla ya kufikia uamuzi wa mgomo, na ndio hapo tunajikuta kutokubali kukubaliana naye.
 
KUNA TAARIFA KUWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM KIMEFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KUTOKANA NA WANAFUNZI KUENDELEA NA MGOMO LICHA YA WAZIRI WA ELIMU PROF MAGHEMBE KUWASISITIZIA WAINGIA MADARASANI IFIKAPO LEO SAA MOJA ASUBUHI, PIA KUNA HABARI KUWA MGOMO HUU UNAMASLAHI YA KIITIKATI ZA KIVYAMA NA INASEMEKENA KUNA NGUVU KUBWA YA CHAMA KIMOJA KIKUBWA CHA SIASA( hayo ni maneno ya wanafunzi wenyewe)
 
Last edited by a moderator:
Kama mgomo wao una sababu za msingi ni sawa wagome lakini isiwe ndio mambo ya kuburuzana kwa hizo sababu za kisiasa wakitimuliwa wataishia kuja kulialia humu kuwa wameonewa....Macho na Masikio yangu yako wazi kusikia mwisho wao!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom