Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Mkuu Masanja chukua tano kwanza.
Ukikaa karibu na wanafunzi wa UDSM ndipo utrakapobaini kuwa wengi wao mawazo yao hayaendi mbali sana. Ukiwasikiliza kwa makini, wanatoa hoja ambazo hazina mashiko. Madai yao yanaweza kuwa ya halali lakini wanashindwa kuangalia upande wa pili wa shilingi. Wanachoomba ni mikopo na inashangaza sana unakwenda kumkopa mtu, anakuamba hana uwezo wa kukukopesha chote unachotaka kukopa, halafu unamjia juu ukimlazimisha akukopeshe kwa kiwango unachotaka wewe na si kulingana na uwezo wake.
Bodi ya mikopo imetengenezwa kama namna fulani ya revolving fund. Wapo wanafunzi ambao walipaswa kuwa wanalipa madeni yao hivi sasa na fedha hizo zingetumika kuwakopesha wanafunzi wengine, lakini nenda ukaulize kiasi gani cha fedha ambacho kilipaswa kuwa kimerejeshwa lakini hakijarudi, utashaa.
Katika madai yao ya sasa wanataka kubadilishwa kwa sera-hivi sera inabadilishwa ghaflaghalfa tu? Walishaambiwa na Maghembe kuwa hicho si kitu cha kukaa na kuamua tu, inahitaji mashauriano ya madau wote, hawataki kusikia. ndio wanaweza kusema kuwa madai hayo yamekuwa ya muda mrefu ambao ungetosha kulifanyia mabadiliko jambo hilo, lakini kweli lazima imesaidia kutatua matatizo yao?
 
MN,, heshima mbele,, suala la sera.....kwani kuanzishwa kwa sera mpya au kubadili iliyopo inakuwaje?

Mi naliona hili vuguvugu kama mchakato katika kubadili sera iliyopo.

Hoja hapa sio uwezo wa bodi ya mikopo bali ni uwezo wa serikali au vinginevyo uwezo ambao serikali ingekuwa nao kama ingelipa suala la elimu ya juu kipaumbele kinachostahili. Tusiiangalia bodi kama chombo kinachosimama peke yake...kimewekwa na serikali!
 
Cönfirmed now. Jamani madai yao ya msingi. Kwani kodi zetu na makato yetu ya madeni ya chuo yanaenda wapi

Inashangaza sana nchi yetu ina rasilimali nyingi tena adimu duniani sidhani kama wawakilishi wetu wanafikiria vyema au labda ni kukandamizwa na mashirika ya umoja wa mataifa. As Nyerere said "You can not say NO?" Kila kipengele wanakipokea na kusaini YES!

Problem here is some of our leaders not able to think outside the box.

University education in Tanzania is very basic finacially as no where in the world one can study at that very small amount of money say US$ 2000 per year incl. tuition, medical fees, etc. That amount a Government such as Tanzania can afford with high paying number of tax payers. Its ridiculous if at all there is a lot of money being taken fraudulently and dubious contracts are being made across this very country to them poor citizens.

I am crying so I can not type anymore.
Till then TKS
 
I really feel these students. Maisha ya mlimani ni magumu, bila bumu hali ni ngumu.

Lakini napenda kuangalia upande wa pili wa shilling. Leo hii 80% ya watanzania wanaishi vijijini wakitegemea jembe la mkono. zaidi ya raia million kumi na tano wako kwenye UMASIKINI WAKUTUPWA. Walio na nafuu wengi wao wanabangaiza mno. Kwa hiyo swala kwamba watoto wengi wanaosoma mlimani ni watoto wa wakulima ni kweli lakini hilo inabidi tufike point tulitafutie muafaka. Nchi yetu ina matatizo mengi mno. Wewe atleast unalalamika lakini kuna millions ambao hata hiyo chuo kikuu ni ndoto ya mchana. wanataka tuu wapate ugali wa mchana. Kuna akina mama wanakufa kwa sababu hawana aspirini, kuna sehemu umeme ni anasa, maji ya bomba ni ndoto..and on and on...Sasa jamani haya ni matatizo ambayo yanaiangalia hiyo hiyo bajeti na kodi zetu.....Think about it..matatizo ni mengi mno....Ingawa watu ni mafisadi wanaiba..lakini hatuwezi kuendelea kutumia kigezo cha umasikini forever...

Tanzania haiwezi KUWAKOPESHA wanafunzi WOTE wa elimu ya juu. Huo uwezo hata kama upo....itatuchukua miaka mingi kuwa na vigezo halali vya kujua nani anastahili...especially kipindi hiki ambacho kila mtu ni fisadi anadanganya... Mimi naamini ile ya kukopesha (60% not sure) was the best way kuwasaidia watoto wa wakulima.... Wazee elimu ya siku hizi ni aghali mno......

Swala kwamba tuna raslimali ambazo zinaweza kuwakopesha wanafunzi kama zingetumika vyema..ni kweli I agree..lakini wote tunajua kabisa..nchi haiendeshwi hivyo...Hata mimi ningesema..yale mabillion ya EPA yangerudishwa..hali za watanzania zingekuwa bora zaidi..lakini we all know what is happening.

Ushauri wangu kwa wanafunzi wa mlimani na kwingineko..inabidi wajue kwamba maisha na zama zimebadilika. huwezi kuishi kwa zile slogans zetu eti..mbona "serikali zamani ilikuwa ikiwasomesha watu wake bure". Hizo slogans hazisaidii tena. Lazima wanafunzi wakae chini waangalie hiyo 40% inapatikana vipi. Mgomo siyo suluhisho....Serikali haina wajibu wa kukusomesha! na wala haina wajibu wa kuwapa mikopo! ni swala la sera tuu.

Kifupi wanafunzi wa elimu ya juu...inabidi waanze kusolve matatizo yao kiutu uzima..sana sana leo wamegoma...watoto wa wenye uwezo..wataenda zao nje..mtoto wa mkulima utarudi Kigoma (kama bado una nauli)..after two moths utaambiwa uandike barua uitume kwa registered mail ya kuomba kurudishwa chuo na masharti yale yale au zaidi! upo hapo?

hivi kweli na hizi shule za Yebo yebo za Lowassa...in ten years kutakuwa na thousands wanaingia chuo kikuu..do you expect serikali iwakopeshe wote? you are kidding! Tujiulize tunaoandika hapa kwenye forum..ni wangapi tumeshalipa mikopo yetu kuwasaidia wenzetu wa nyuma?

Hili swala ni gumu halihitaji mgomo wala papara...

Kindly we need to think outside the box and not the way our logic and thinking and intelliegence so determines sometimes.

What students did is the right approach because inside the box is politics and outside the box country interests. Think and think not just sitting on comfortable sits and pc infront of us and say this is not the way the govt is run to give them citizens what belongs to them?

I was wondering if you though studied under the same system you would otherwise be negative to these students especially when summing it up with the present country's financial turmoil and ufisadi and dubious contracts. One that sees this can cry 24/7 or shout for them students!!!
 
Date::11/12/2008
Wanafunzi sasa wamtaka Kikwete

Na Waandishi Wetu
Mwandishi

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu, eneo la Mlimani, sasa wanamtaka Rais Jakaya Kikwete aende chuoni kuzungumzia mpango wa serikali yake kutatua tatizo la sera ya uchangiaji elimu ambayo wanaipinga kwa kutoingia madarasani.

Hatua hiyo ilifikiwa baada ya mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kushindwa kutokea kwenye Ukumbi wa Nkrumah, ambako wanafunzi hao walikuwa wamekusanyika kuzungumzia mgomo wao.

Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Anthony Machibya, alikuwa amewataarifu wanafunzi hao jana kuwa, baada ya Waziri Jumanne Maghembe kukutana na viongozi wa vyuo saba vya serikali, aliahidi kutuma mwakilishi wa wizara chuoni hapo ili awaeleze wanafunzi hatua ambazo serikali itachukua kumaliza mgomo ulioanza juzi kupinga sera hiyo ya uchangiaji.

Baada ya wanafunzi hao kumsubiri kwa muda mrefu mwakilishi huyo, rais huyo aliingia tena kwenye ukumbi huo wa Nkrumah na kuwataarifu wanafunzi kuwa, mwakilishi huyo asingeweza kufika kwa kuwa amekwenda kukutana na Rais Jakaya Kikwete kujadili suala hilo.

"Baada ya kwenda kwa makamu mkuu wa chuo, Profesa Rwekaza Mukandala, nilitaarifiwa kuwa makamu huyo akiwa na baadhi ya wasaidizi wake wameitwa Ikulu na Rais Kikwete kuzungumzia madai yetu pamoja na Waziri wa Elimu, Profesa Jamanne Maghembe," alisema Machibya.

Taarifa hiyo iliwafanya wanafunzi kulipuka kwa furaha za shangwe.

Baadaye mmoja wa wanafunzi hao alipewa kipaza sauti na kupendekeza kuwa, kwa kuwa viongozi wengine wamekuwa wakitoa majibu ambayo yanaonekana kuwa ni ya kusumbua, ni afadhali wakutane na rais, pendekezo ambalo lilipitishwa na wanafunzi wote, waliokuwa wakipiga kelele wakidai kuwa wamechoka kuzungushwa kwa hadi zisizotekelezeka.

Wanafunzi hao wanapinga sera ya uchangiaji gharama za elimu ambayo inataka wazazi walipie sehemu ya gharama hizo na walianza mgomo wao juzi bila ya vurugu kubwa.

Chini ya utaratibu huo, wanafunzi hutakiwa kujaza fomu zinazoeleza mintaarafu ya maisha yao na wazazi wao, ikiwa ni pamoja maelezo ya shule walizopitia na baadaye taarifa hizo huingizwa kwenye kompyuta ambayo hufanya mchanganuo na kuamua muombaji mkopo wa elimu apewe fedha kwa kiwango gani.

Kwa mujibu wa takwimu za Bodi ya Mikopo, asilimia kubwa ya wanafunzi huangukia kwenye kuchangia asilimia 20 ya gharama za masomo ya vyuo vya elimu ya juu, wakati ni wachache sana ambao hupata asilimia 100.

Wakati wanafunzi wakikubaliana kuwa Rais Kikwete ndiye suluhisho la matatizo yao, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof Jumanne Maghembe aliwaambia waandishi wa habari kuwa, wanafunzi wote hawana budi kuingia madarasani leo, kusubiri suala lao kushughulikiwa na serikali.

Profesa Maghembe alisema kutokana na wanafunzi kutaka sera hiyo ifutwe, serikali ilikutana na viongozi wa wanafunzi juzi na kukubaliana na viongozi wa wanavyuo hao kuwa leo waingie darasani huku mchakato wa kuiangalia sera hiyo ukifanywa na serikali.

"Kama waziri mwenye dhamana, niliwasisitiza viongozi kuwa matatizo yaliyojitokeza katika utekelezaji wa sera hiyo, yatatafutiwa ufumbuzi na tukakubaliana katika kikao hicho cha pamoja cha Oktoba 23, 2008," alisema Maghembe.

Prof Maghembe aliongeza kutokana na hali ya uchangiaji elimu kuanzia mwaka 2005/06 hadi Juni 2008 wanafunzi 145,970 wamenufaika na mikopo hiyo na kiasi cha Sh254 bilioni kimetumika na kwa mwaka 2008/09 mpango huo unatarajiwa kunufaisha wanafunzi 60,000.

Pia tamko hilo la Serikali limewataka wanafunzi wote waliogoma kurejea madarasani leo saa 1.00 asubuhi na wawe wamesitisha mgomo wao wakati serikali ikiendelea kushughulikia matatizo ya sera hiyo.

Hali ilikuwa mbaya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, eneo la Mlimani, ambako wanafunzi waliogoma walifanikiwa kukwamisha takriban mitihani mitatu, ukiwemo wa Historia uliokuwa ufanywe jana asubuhi na mwingine wa 264 CO, uliokuwa ufanyike kwenye kafteria ya Yombo chuoni hapo jana saa 8:00 mchana.

Wanafunzi hao waliunda kikundi walichokiita cha 'task force' ambacho kilizunguka kwenye madarasa na maktaba ya chuo hicho na kuwatoa nje wanafunzi waliokuwa wakijisomea, kitendo ambacho kilisababisha mgogoro kati yao na kulazimu maktaba hiyo kufungwa.

"Tunachotaka ni ninyi kuondoka hapa darasani mkasomee huko mabwenini kwenu kwa sababu mnapofanya hivyo mna maana hiki tunachokifanya sisi hakina maana na ninyi ndiyo mnaopenda kusoma sana," alisema mwanafunzi mmoja wa kikosi hicho.

Kitendo hicho kililalamikiwa na baadhi ya wanafunzi hasa walio mwaka wa mwisho, wakidai kuwa kinawanyima haki ya kujisomea wanafunzi wasiotaka kujihusisha na mgomo huo.

"Kwa kawaida wanafunzi wanaomaliza siku zote kunapotokea mgomo hawataki kujihusisha. Hii ni kwa sababu wengi wanakuwa wako makini sana na kusoma na wanaogopa wakigoma wanaweza wakaathirika na kupoteza miaka yote waliyokaa chuoni," alisema Fakih Othman, ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu.

"Suala la kuwazuia wengine wasisome halipendezi kwa sababu linawanyima uhuru wao wa kusoma."

Fakih aliongeza kusema: "Ninaunga mkono mgomo huu kwa kuwa umesababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kuendelea na masomo na wengine kuishi maisha ya tabu, lakini njia zinazotumika kufanya mgomo huo haziwashirikishi wanafunzi wote ndiyo maana baadhi ya wabunge waliupinga katika vikao vya Bunge vilivyopita."

Afisa Uhusiano wa UDSM, Isdory Jackson alikataa kuzungumzia kitendo hicho akisema si msemaji wa chuo.

Habari hii imeandikwa na Hussein Kauli, Mussa Mkama na Festo Polea.
 
hivi ni kweli serikali inashindwa kuwalipia mkopo 100% au ndo hivyo wanazungushia kwenye mabussiness yao?

Katiba ya Tanzania inamtambua raia kuwa mtu mzima mwenye uwezo wa kujitegemea anapotimiza miaka 18. Kwa mujibu wa sheria za kazi, mafao apatayo mfanyakazi, inaweza kuwa ni pamoja na matibabu, usafiri n.k kwake ni watoto ambao kisheria ni wa umri wa chini ya miaka 18.

Kwa maana hiyo, kumbebesha mzigo mzazi kumsomesha hawa watu wazima ambao kisheria wanatakiwa wajitegemee ni kosa. Hili linabaki kuwa jukumu la serikali, na njia ya kulifikia hili ni kuwapatia mikopo kwa silimia 100.

Kifungu cha 9(a) cha katiba kinasema hivi "kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa
waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;"

na kifungu cha 11 (3) "Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu
wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata
elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo
vinginevyo vya mafunzo."

Kifungu cha 11(1) kinasema hivi ".... . Na bila kuathiri haki hizo, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake"

1. SASA FURSA SAWA INAPATIKANA JE? (WENGINE KUPATA 20% NA WENGINE 80% ???)

2. Kila mtu anaishi kwa jasho lake. Ni sahihi mtu mwenye umri unazidi miaka 18 kuishi kwa jasho la mzazi wake kikatiba? Je, serikali ili weka utaratibu na kuingia mkataba na wazazi ili waweze kuwakopesha hao kina baba na kina mama wanaosoma kwenye vyuo vyetu?
 
MN,, heshima mbele,, suala la sera.....kwani kuanzishwa kwa sera mpya au kubadili iliyopo inakuwaje?

Mi naliona hili vuguvugu kama mchakato katika kubadili sera iliyopo.

Hoja hapa sio uwezo wa bodi ya mikopo bali ni uwezo wa serikali au vinginevyo uwezo ambao serikali ingekuwa nao kama ingelipa suala la elimu ya juu kipaumbele kinachostahili. Tusiiangalia bodi kama chombo kinachosimama peke yake...kimewekwa na serikali!

Kuhusu suala la uwezo wa serikali, ukisoma bandiko la masanja hapo juu ameleza kinaganaga. Ni kweli kuwa serikali ina fedha lakini tukumbuke pia kuwa kuna matatizo mengi ambayo utatuzi wake unahitaji zaidi ya hizo fedha ambazo serikali inazo. tatizo ni kuwa wanafunzi wengi wanachukulia mikopo hii kama misaada-wana malengo ya kutorudisha fedha hizo. ndio maana utawaona wanahusisha masuala ya ufisadi na wao kuomba mikopo. Hoja kwamba "mbona mafisadi wanaiba fedha" unapoiingiza kwenye madai kama haya, unajionyesha kuwa na wewe una lengo la kufisadi pia.
Kuhusu suala la kubadili sera; linahusisha mchakato ambao unawahusisha watu na taasisi kadhaa zinazohusika na sera hiyo. katika hili, si suala la Maghembe au hata Pinda kukaa na kuamua kuwa kuanzia sasa tunaondoa means testing kwenye sera ya mikopo ya elimu ya juu. Inabidi wadau wakae, kukiwa na hoja za msingi kuhusiana na ubaya wa hicho kinachopingwa na wanafunzi na hoja hizo zitapimwa na iwapo itakubaliwa kwua hoja zao ni za msingi, hapo ndipo mchakato wa kuibadili sera hiyo utakapoanza, si waziri kukaa peke yake na kuamua kwa sababu si yeye aliyeiweka sera hiyo peke yake
 
Lakini hii tabia ya kuwafukuza wanafunzi chuoni wakigoma itaisha lini?inakera sana kwa kweli
yaani watu wanafukuzwa hadi vyumbani!Sasa kufunga chuo ndo kutasababisha tatizo kutatuliwa au?Serikali iwasikilize wanafunzi!
 
Kuwafukuza Wanafunzi chuoni ni sera iliyopitwa na wakati; inatimiza ile sera ya "wagawanye then uwatawale". Serikali ikiishiwa sera madhubuti ya kukabiliana na tatizo wanatumia vitisho na kutegemea ushirikiano kutoka kwa raia ambao hawana elimu.

Maoni yangu ni kuwa sioni kama ni sahihi kwa serikali kulipia kila mwanafunzi 100% ya ada yake. Kuna wanafunzi wengi ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwalipia ada yote, na kuna wale ambao hawana hata uwezo wa kupata hela ya kula. Serikali ilipaswa kutafuta utaraibu uliosimama wa kuwachuja hawa ambao wazazi wao wana uwezo na kuwaachi mzigo huo wazazi wao.

Inachofanya serikali sasa hivi ni kuwaweka wanafunzi wote kwenye kapu moja na kuwaamuru wote walipe 60%. Huku ni kufilisika ni kisera na ukiukwaji mkubwa wa jukumu la serikali kulinda na kusaidia maendeleo ya nchi kupitia elimu kwa raia wake.
 
Lakini hii tabia ya kuwafukuza wanafunzi chuoni wakigoma itaisha lini?inakera sana kwa kweli
yaani watu wanafukuzwa hadi vyumbani!Sasa kufunga chuo ndo kutasababisha tatizo kutatuliwa au?Serikali iwasikilize wanafunzi!

First lady, mimi naamini hata mgomo nao usingesaidia kutatua matatizo haya
 
Kuhusu suala la uwezo wa serikali, ukisoma bandiko la masanja hapo juu ameleza kinaganaga. Ni kweli kuwa serikali ina fedha lakini tukumbuke pia kuwa kuna matatizo mengi ambayo utatuzi wake unahitaji zaidi ya hizo fedha ambazo serikali inazo. tatizo ni kuwa wanafunzi wengi wanachukulia mikopo hii kama misaada-wana malengo ya kutorudisha fedha hizo. ndio maana utawaona wanahusisha masuala ya ufisadi na wao kuomba mikopo. Hoja kwamba "mbona mafisadi wanaiba fedha" unapoiingiza kwenye madai kama haya, unajionyesha kuwa na wewe una lengo la kufisadi pia.
Kuhusu suala la kubadili sera; linahusisha mchakato ambao unawahusisha watu na taasisi kadhaa zinazohusika na sera hiyo. katika hili, si suala la Maghembe au hata Pinda kukaa na kuamua kuwa kuanzia sasa tunaondoa means testing kwenye sera ya mikopo ya elimu ya juu. Inabidi wadau wakae, kukiwa na hoja za msingi kuhusiana na ubaya wa hicho kinachopingwa na wanafunzi na hoja hizo zitapimwa na iwapo itakubaliwa kwua hoja zao ni za msingi, hapo ndipo mchakato wa kuibadili sera hiyo utakapoanza, si waziri kukaa peke yake na kuamua kwa sababu si yeye aliyeiweka sera hiyo peke yake

Mkuu labda useme wewe

Wengine tunaonekana tunaihurumia serikali. Hapana! No body is symphathetic to JK and his group...lakini wanafunzi nao inabidi wawe serious bana...

Sana sana wanafunzi wangegomea hiyo means testing method inayowafanya wengine wapate na wengine wasipate mkopo. Kifupi lazima wawe na hoja waonyeshe kwamba hiyo method ina descrepancy zinazoweza kurekebishika. Hivi Tanzania kuna vyuo vikuu vingapi? Na wote wanaitegemea hiyo hiyo serikali?.

Jee UD wamegoma..is it all higher learning institutions in the country au ni mlimani tuu ndo wamegoma?

My friend kugoma eti lazima serikali ikukopeshe mtoto wa mkulima..duh..who cares with mtoto wa mkulima nowadays? Kibaya zaidi sidhani kama wanafunzi walishirikishwa wakati wa kutunga hizi sera za mikopo...

Mama wa kwanza;

Kufukuzwa ni wajibu..kama una siku mbili umegomea darasa..ni kwamba huna haja ya kuendelea kutumia facilities za chuo..kwa nini waendelee kulipia umeme, maji nk wakati wewe hausomi? na hii ni issue ya bodi/serikali vs wanafunzi..Mkandara na chuo wao wako pembeni..

Serikali yetu ni incompetent, but lets do better than the government.
 
Mkuu MN,

Apo juu napata tabu kukubaliana na wewe kwenye hilo..inawezekana wanarejea mafisadi wanaoiba fedha kuonyesha kuwa fedha hizo zingetumika kuwakopesha!

Mimi ningependa kujua kuwa serikali inahitaji kiasi gani cha fedha kuwakopesha wote kwa 100%, halafu tuone pia hivyo vipaumbele vingine/au matatizo mengine yanaopewa kipaumbele ni yapi zaidi ya elimu

Kama kuna chi inacheza na elimu sasa hivi katika dunia hii, tusitegemee kwenda mbele hata siku moja!

Nakubaliana na wewe kuwakuhusu sera, Maghembe hawezi kuibuka mwenyewe na kusema kuwa anabadili sera...lakini nirudie pia kuwa kubadili sera ni mchakato na huo mgomo ni sehemu ya mchakato huo!
 
First lady, mimi naamini hata mgomo nao usingesaidia kutatua matatizo haya

LOL siku hizi ndo imeshakuwa utaratibu wetu...fikiria mambo ya TRL utapata jibu ni kwa nini mgomo unaweza kutatua hali kama hii

nakumbuka enzi nasoma chuo kikuu, mambo yalikuwa hayaeleweki hadi mgomo..cha ajabu mkishagoma mnatatuliwa shida zenu ambazo zilionekana hazitatuliki wakati wa mazungumzo!
 
First lady, mimi naamini hata mgomo nao usingesaidia kutatua matatizo haya
Mgomo unasaidia sasa kama serikali inashindwa kutatua matatizo bora kugoma!hata manchi ya watu huko huwa wanagoma then mambo yanakuwa mswano!ila kufunga chuo!hii kali
 
Mkuu labda useme wewe

Wengine tunaonekana tunaihurumia serikali. Hapana! No body is symphathetic to JK and his group...lakini wanafunzi nao inabidi wawe serious bana...

Sana sana wanafunzi wangegomea hiyo means testing method inayowafanya wengine wapate na wengine wasipate mkopo. Kifupi lazima wawe na hoja waonyeshe kwamba hiyo method ina descrepancy zinazoweza kurekebishika. Hivi Tanzania kuna vyuo vikuu vingapi? Na wote wanaitegemea hiyo hiyo serikali?.

Jee UD wamegoma..is it all higher learning institutions in the country au ni mlimani tuu ndo wamegoma?

My friend kugoma eti lazima serikali ikukopeshe mtoto wa mkulima..duh..who cares with mtoto wa mkulima nowadays? Kibaya zaidi sidhani kama wanafunzi walishirikishwa wakati wa kutunga hizi sera za mikopo...

Mama wa kwanza;

Kufukuzwa ni wajibu..kama una siku mbili umegomea darasa..ni kwamba huna haja ya kuendelea kutumia facilities za chuo..kwa nini waendelee kulipia umeme, maji nk wakati wewe hausomi? na hii ni issue ya bodi/serikali vs wanafunzi..Mkandara na chuo wao wako pembeni..

Serikali yetu ni incompetent, but lets do better than the government.
Kama nimekosea mnisahihishe by law si inasema mkigomea darasa siku tatu mfululizo ndo mnatimuliwa au?siku hizi hata mkigoma siku moja tu mnashtukia press release kila mtu kwa yaani wanahangaika sana fikiria huna jamaa Dar yaani maisha yanakuwa magumu kweli!
 
Ndugu zangu nchi hii imeoza na "material condition" inaita kwa mapinduzi makubwa, JK ameelemewa kabisa na hali hii. Sasa kuna wale wenye mawazo finyu wanaosema kuwa kuna chama cha siasa kiko nyuma ya hili, mimi nakataa, tuangalie hoja je ni ya msingi? Siku za ccm sasa zinahesabika na wantapa tapa.

Hata hivyo kufungwa kwa UDSM si jambo la ajabu na nawapongeza mbwana wadogo uzi ni ule ule mpaka kieleweke, kufukuzwa kwenu ni msingi mzuri kwa elimu ya Tanzania baadaye.

Msife moyo kwani Mungu yupo upande wenu.
 
Viongozi wetu wanashangaza sana kwa kweli!Mtu unamwambia alipe asilimia 40!yaani ni hohehahe wa kutupwa nauli yenyewe yakuja Dar kachangiwa na kijiji!Ingekuwa ni nchi inayotoa fursa kwa mfano kungekuwa na student jobs yaani mtu unaweza ukafanya kazi na kujikakamua kulipa hiyo asilimia 40 hapo ningesema wanafunzi hawana sababu ya kugoma!Ila kwa hali hii ya sasa viongozi wanachemsha sana sasa tutawekezaje kwenye elimu kama mambo yenyewe ndo haya?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom