Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,391
- 39,484

Wanachuo UCLAS wagoma
2007-02-23 09:29:20
Na Sabato Kasika
Wanafunzi zaidi ya 1000 wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo (UCLAS), jijini Dar es Salaam, wamegoma kuingia darasani wakilalamikia kukatwa fedha zao za mafunzo kwa vitendo yanayotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Mgomo huo ulianza jana asubuhi ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wa tano wanaochukua masomo mbalimbali yakiwemo ya mipango miji, upimaji ardhi, uhandisi mazingira na usanifu majengo, walikuwa wakiushinikiza uongozi wa chuo kuwalipa fedha zao.
Akizungumza na Nipashe, Rais wa chuo hicho, Bw. Ndatwa Ng?evilabuze, alisema awali wanafunzi wa awamu ya mwisho walikuwa wakipewa Sh. 3500 kwa ajili ya malazi na chakula na Sh. 6000 kila siku kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Alisema kwa sasa wamepata taarifa kuwa pesa hizo za mafunzo zimekatwa kwa kila mwanafunzi Sh. 50,000 ambapo wao wanahoji kuwa ukataji huo umeangalia vigezo gani.
(Wanafunzi wa Mlimani walipogoma mapema mwaka huu)
04.10.2007 0847 EAT
Muhimbili wagoma
*Ni kutokana na baadhi yao kukosa makazi
*Mkuu wa Chuo asema hosteli hazijakamilika
*Awaambia hamkufuata mabweni bali masomo
Na Said Mwishehe
WANAFUNZI zaidi ya 1,400 wa Chuo Kikuu cha Sayansi za Afya (MUCHS) Dar es Salaam, wamegoma kuingia darasani kutokana na wenzao mwa mwaka wa kwanza kukosa sehemu za kuishi.
Mgomo huo ulianza jana saa sita mchana, baada ya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho (MUHASSO), Bw. Edwin Chitage, kutangaza rasmi mgomo huo kupitia Baraza la Chuo, ambao kumalizika kwake kutatokana na kutotimizwa kwa madai waliyoyatoa kwa uongozi wa chuo.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Wanafunzi chuoni hapo, Bw. Chigate alisema wamefikia uamuzi wa kugoma ikiwa ni hatua ya kuushinikiza uongozi wa chuo kuwatafutia makazi mapya baada ya kuona wanafunzi wa mwaka wa kwanza 124 hawana makazi ya kuishi na wengine zaidi ya 1,000 wakitangatanga kwa wenzao kutokana na kupanga mbali na chuo.
©2007Business Times Limited .
Wanafunzi IFM wagoma
2007-06-05 10:45:49
Na Godfrey Monyo
Wanafunzi wote wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) cha jijini Dar es Salaam, wamegoma kuingia madarasani kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kuwarudisha wenzao waliofukuzwa.
Nipashe ilifika chuoni hapo jana saa 3:40 asubuhi na kuwakuta wanafunzi hao wakiwa wamekusanyika katika makundi makundi wakijadili hatma ya wanafunzi wenzao waliotimuliwa.
Mbali ya wanafunzi kukusanyika nje ya chuo hicho, pia walikuwa wakipiga kelele na kuimba nyimbo mbalimbali zilizolenga kuushinikiza uongozi wa chuo hicho kusikia kilio chao na kuwarejesha masomoni wenzao watatu waliofukuzwa tangu Mei 29, mwaka huu akiwemo Rais wa Serikali ya Wanafunzi, Bw. Baltazar Boniface.
Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe wagoma
John Nditi, Morogoro
HabariLeo; Friday,October 26, 2007 @00:01
WANAFUNZI wa mwaka wa kwanza na wa pili wapatao 1,800 wa Chuo Kikuu Mzumbe mkoani hapa, wametangaza kuanza mgomo wa kutokuingia darasani kuanzia jana.
Mgomo wao ni kupinga uamuzi uliochukuliwa na chuo hicho wa kutowafanyia udahili wanafunzi watakaoshindwa kulipa ada ya muhula wa kwanza. Wanafunzi hao wamesema watagoma kwa muda usiojulikana.
Wanafunzi hao wameamua kugoma baada uongozi wa chuo hicho kuchapisha waraka Oktoba 19, mwaka huu unaotoa maelekezo mapya ya udahili kwa mwaka 2007/08 kwa wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza na wa pili wanaofadhiliwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Kwa mujibu wa waraka huo uliosainiwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Joseph Kuzilwa, idadi kubwa ya wanafunzi wanaofadhiliwa na Bodi hiyo wamekwisha kulipa ada ya tuisheni kwa mwaka wa masomo 2007/2008.
Hata hivyo, baadhi ya wanafunzi hao ambao wamegoma kulipa kima cha chini cha asilimia 50 ya ada hiyo ambayo ni Sh 400,000 kwa muhula wa kwanza.
Kwa mujibu wa waraka huo, mwanafunzi atakayekubaliwa kupatiwa chumba cha kuishi katika mabweni ya chuo hicho ni yule atakayekuwa ametimiza masharti yaliyotolewa na uongozi wa chuo hicho.
Wanafunzi DUCE wagoma
2007-11-29 10:30:19
Na Eshy Mushi na Anneth Kagenda
Wanafunzi 56 wa mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Ualimu Dar es Salaam (DUCE), wamegoma kuingia madarasani kama njia ya kushinikiza kupewa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Wamedai kuwa, hatua ya uongozi wa DUCE, kukataa kusaini fomu za mikopo walizoziwasilisha, imewafanya washindwe kuhudumiwa na HESLB.
Hayo yalisemwa jana na baadhi ya wanafunzi hao walipokuwa wakizungumza na Nipashe chuoni hapo.
SWALI:
Hivi mwaka ujao 2008 tunaweza kwenda bila kuwa na mgomo kwenye chuo chochote kikuu? Ninyi wenzetu mlioko ughaibuni mara ya mwisho kuwa na mgomo wa wanafanzi kwenye nchi zenu/vyuo vyenu ilikuwa lini?