Migogoro wa wakulima na wafugaji haijapata ufumbuzi

Wewe Mama umeniboa sana leo, najiuliza kama tungekupa Ikulu hali ingekuwaje? Mkulima eneo lake ni lile lile miaka nenda rudi. Mzee Rajab wa Msowero alirithi shamba kwa baba yake zaidi ya ekari 50 miaka ya sitini, analima hapo miaka yote na amegawia wanaye na wajukuu, lakini shamba hilo hilo limesababisha apoteze wanaye na wajukuu kwa kuuwawa na wafugaji miaka 50 toka arithishwe shamba. Je lile shamba ni laana? Anajiuliza, anasema bora asingekubali lile shamba labda angebakia na wanaye na wajukuu? Lakini angewalisha nini yeye ni mkulima?
umeongea point mkuu
 
Tanzania inapata UHURU tulikuwa na wasomi wa ngapi wa ardhi ?
Kuna sera gani nzuri iliyowahi tokea Ya kudhidi hii Ya siasa na kilimo ?..................
Umeleta maswali mazuri sana...laiti watu wote wangekuwa wanapenda kujadili kwa lengo la kuleta ufumbuzi na siyo kutafuta justifications...

Kwanza kabisa hatukuwahi kuwa na sera yoyote ya maendelo kabla ya miaka ya 1990. Pia wakati huo wataalamu wetu wa ardhi na dunia kwa ujumla zaidi ya kujua kupima ardhi bila kuelewa mifumo inayohusiana na shughuli za maendelo hasa yanayotumia ardhi yanaingiliana vipi na kuhusiana vipi na mifumo ya ki ekolojia. Kutokana na sababu hizo sheria nyingi zilizokuwa zinatumika zilikuwa ni za mkoloni na zingine hadi leo hazijabadilishwa hadi hapo miaka ya mwanzo wa miaka ya 1990. Siasa ni kilimo siyo sera bali azimio ambalo kabla ya sera iliyopo sasa ilitumika kama sera.

Kwa sasa dunia imetambua baadhi ya practices ai anthropogenic activities ni hatari kwa mazingira na hivyo zina implications kwenye sustainability. Ni miaka hiyo hiyo ya mwanzo ambapo nasi tulipoanza kuleta mabadiliko ya kimfumo yaani structural adjustment ambayo ililetwa kutoka nje, ndipo na dunia nzima ilianza kuelewa namna ambavyo shughuli za binadamu zisiporatibiwa vyema zinaweza kusababisha uchumi kuanguka kwa miaka ya baadaye na vizazi vyetu pengine kushindwa kumudu maisha. Ndipo ambapo maazimio mengi yalipoanza sambamba na sisi kama nchi tukiyapokea na kuingiza katika sera zetu huku tukisomesha watu wetu katika fani mbalimbali.

Kwa sababu hiyo kwakua wasomi wameanza kuongezeka na uelewa kuwa mpana katika agenda nzima ya sustainable development ambayo imekaziwa sana na mabadiliko ya tabia nchi, ndipo sasa ambapo sisi kama nchi tunatakiwa kujitathmini na kuangalia ni wapi na sisi tunaweza kurekebisha sera nanpengine mipango yetu ya maendeleo bila kusababisha hasara kubwa kwa kundi fulani la jamii.

Bahati mbaya sana wakulima wetu na wafugaji wanategemea mali asili moja kwa moja yaani primary users. Wote hao wameathirika na mabadiliko hayo ya tabia nchi ambayo pia nykngi zikiwa zimesababishwa na njia zao za uzalishaji. Hii imepelekea wao kuanza kugombea rasilimali kwakua tu kwanza kuna ongezeko la mahitaji huku namna yao yankuongeza uzalishaji ukitegemea kuongeza ukubwa wa ardhi badala ya uzalishaji kutumia rasilimali kidogo iwe ardhi, mifugo au mazao.

Wataalamu nao wanajitahidi kuja na tafiti mbali mbali ambazo nyingi kutokana na changamoto za nchi hazijatumiwa na watendaji wa serikali kuweza kuhimili changamoto zao za kitendaji....

Nitoe rai yangu kuwa, tunahitaji kama taifa kukaa pamoja na kupanga mipango yetu kwakutumia mbinu ya ushirikishaji wa wadau badala ya kutupa lawama kwa kundi hili au lile

Nawasilisha!
 
Umeleta maswali mazuri sana...laiti watu wote wangekuwa wanaoenda kujadili kwa lengo la kuleta ufumbuzi na siyo kutafuta justifications...

Kwanza kabisa hatukuwahi kuwa na sera yoyote ya maendelo kabla ya miaka ya 1990. Pia wakati huo wataalamu wetu wa ardhi na dunia kwa ujumla zaidi ya kujua kupima ardhi bila kuelewa mifumo inayohusiana na shughulinza maendelo hasa yanayotumia ardhi yanaingiliana vipi na kuhusiana vipi na mifumo ya ki ekolojia. Kutokana na sababu hizo sheria nyingi zilizokuwa zinatumika zilikuwa ni za mkoloni na zingine hadi leo hazijabadilishwa hadi hapo miaka ya mwanzo wa miaka ya 1990.

Kwa sasa dunia imetambua baadhi ya practices ai anthropogenic activities ni hatari kwa mazingira na hivyo zina implications kwenye sustainability. Ni miaka hiyo hiyo ya mwanzo ambapo nasi tulipoanza kuleta mabadiliko ya kimfumo yaani structural adjustment ambayo ililetwa kutoka nje, ndipo na dunia nzima ilianza kuelewa namna ambavyo shughuli za binadamu zisiporatibiwa vyema zinaweza kusababisha uchumi kuanguka kwa miaka ya baadaye na vizazi vyetu pengine kushindwa kumudu maisha. Ndipo ambapo maazimio mengi yalipoanza sambamba na sisi kama nchi tukiyapokea na kuingiza katika sera zetu huku tukisomesha watu wetu katika fani mbalimbali.

Kwa sababu hiyo kwakua wasomi wameanza kuongezeka na uelewa kuwa mpana katika agenda nzima ya sustainable development ambayo imekaziwa sana na mabadiliko ya tabia nchi, ndipo sasa ambapo sisi kama nchi tunatakiwa kujitathmini na kuangalia ni wapi na sisi tunaweza kurekebisha sera nanpengine mipango yetu ya maendeleo bila kusababisha hasara kubwa kwa kundi fulani la jamii.

Bahati mbaya sana wakulima wetu na wafugaji wanategemea mali asili moja kwa moja yaani primary users. Wote hao wameathirika na mabadiliko hayo ya tabia nchi ambayo pia nykngi zikiwa zimesababishwa na njia zao za uzalishaji. Hii imepelekea wao kuanza kugombea rasilimali kwakua tu kwanza kuna ongezeko la mahitaji huku namna yao yankuongeza uzalishaji ukitegemea kuongeza ukubwa wa ardhi badala ya uzalishaji kutumia rasilimali kidogo iwe ardhi, mifugo au mazao.

Wataalamu nao wanajitahidi kuja na tafiti mbali mbali ambazo nyingi kutokana na changamoto za nchi hazijatumiwa na watendaji wa serikali kuweza kuhimili changamoto zao za kitendaji....

Nitoe rai yangu kuwa, tunahitaji kama taifa kukaa pamoja na kupanga mipango yetu kwakutumia mbinu ya ushirikishaji wa wadau badala ya kutupa lawama kwa kundi hili au lile

Nawasilisha!
Somo zuri sana mkuu
 
Tujue chanzo kwanza ili tuweze kusuluhisha...Je wajua sheria nyingi zinamhukumu mfugaji na kumpa upendeleo mkulima? Je unafahamu kuwa vijiji vyote vilivyotengwa kwaajili ya ufugaji vilivamiwa na wakulima kwa kisingizio cha kukosa ardhi ya kilimo huku sheria ikiwa haitoi ulinzi kamilibkwanardhi ya mfugaji au kwa mkulima?

Kutambua tatizo ni chanzo cha kupata suluhu tuache hisia tuishi uhalisia nao ni kuwa, wakulima kama walivyo wafugaji wote ni raia wa Tanzania nao wanayo mahitaji yao ya msingi ambayo mengi ynatokana na kukosekana kwa uratibishaji mzuri wa viongozi wa sector husika.
Nadhani nimedokeza wazi kuwa hakuna mipaka ya fulani kuishi kule na mwingine pale. Hakuna dhana oh hawa wametokea mikoa fulani.
Tatizo ni elimu duni, inayosababisha watu kumiliki mifugo mingi huku wakiishi kwenye umasikini wa kutupwa. Hiyo ni kwa wafugaji. Mtu ana miliki ng'ombe elfu moja, kamuulize anazalisha maziwa kiasi gani. Au zinamsaidia nini. Tuwasaidie wafugaji sasa kwa motisha ya kila namna kwa wale ambao wanataka ufugaji wa kibiashara na si wa kuhesabu ng'ombe.
 
ungejibu kwa hoja kuliko kutoa povu...
subiria makala siwezi kuandika kifupi jambo hili ni kubwa sio kama mama anna alivyoandika ndio maana nimeishia kumkosoa....nakuombea maisha marefu ushuhudie makala yangu ninayoandaa kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji nchini
 
Kwanza kwa kuwa umeanzisha uzi hapa, inabidi uujibu maana wanasiasa mnatabia ya kuanzisha threads na kuzikimbia.
Huoni kwamba unaonyesha kuegemea upande mmoja wa wafugaji? Kama mwanasiasa ulitakiwa kuwa on natural ground.

Kifupi ni kwamba unaonyesha huelewi madhira yanayoletwa na jamii za wafugaji, hasa wamasai, maana hawajali mazao ya mkulima, yani wewe upande wao walishe mazao kwa lazima, ushawahi ona wapi huo utaratibu?
Ushawahi ona mkulima kavamia shamba la mfugaji akaanza kulima?
Kwanini ni mfugaji tu kila siku avamie shamba la mkulima?

Wafugaji wamelelewa sana, wanatenda maovu, sheria hazichukuliwa, wamevimba kichwa. Last week mkulima kapigwa mkuki mdomoni ukatokea shingoni, Morogoro tu hapo, sababu mmasai aliingiza ng'ombe kwa lazima katika shamba lake na kuanza kuharibu mazao machanga. kama ni uvumilive, wakulima wamekuwa wavumilive sana, siku wakiamka itakuwa shida.
Mama kawatetea wafugaji labda kwa vile na yeye ni wa huko
Ukweli ni kuwa wafugaji ni tatizo
Ugali ni muhimu kuliko nyama
Anasema tatizo lilianzia kwenye hizo hekta 70k......... Ina maana wafugaji wote tunao waona maeneo mbalimbali wakisababisha migogoro ni hao wa manyara peke yao?
 
Nakubaliana na wewe kabisa...pengine niongezee kwakuuliza hili sheria ipi inalinda ardhi ya kilimo huku tukitambua kuwa landscapes karibu zote kama madini, national parks, game reserves, forests, water bodies zimewekewa ulinzi wa kisheria?

Utaona kuwa watanzania wa kawaida ambao ni wakulima na wafugaji hawajalindwa kisheria, yaani nyenzo kuu zao za uzalishaji hazijalindwa kisheria. Hii inatoa nafasi kwa wawekezaji wakubwa kuwa nyanyasa sana watu wa chini kwakua tu hakuna enough safety nets.

Bado tunayobahati kama nchi ukilinganisha na nchi nyingi duniani kwamba mtanzania mdogo bado anaweza akapata access to land. Ni vyema basi wakati huu hasa kwa Mh. Rais aliyeamua kulinda haki za wanyonge kuweka mifumo ambayo itampa huyu mnyonge fursa za kuweza ku escape from poverty kupitia rasilimali walizo nazo wengi wakiwa na mifugo pamoja na mashamba madogomadogo.
Wewe unachoandika hapa ni usanii Tu, hatuko kwenye ujamaa na kujitegemea saizi. Kila mfugaji anamiliki mifugo yake na akiuza hela ni zake binafsi, lakini kwenye kuchunga mifugo wanachunga eneo linalomilikiwa na kijiji kizima, nini haki ya wasio na mifugo? Kila mkulima ana eneo lake defined na mkulima mwingine akitaka kulitumia anakodisha kwa hela au kuazima, kwa nini mfugaji asiwe na eneo lake?
 
Nadhani nimedokeza wazi kuwa hakuna mipaka ya fulani kuishi kule na mwingine pale. Hakuna dhana oh hawa wametokea mikoa fulani.
Tatizo ni elimu duni, inayosababisha watu kumiliki mifugo mingi huku wakiishi kwenye umasikini wa kutupwa. Hiyo ni kwa wafugaji. Mtu ana miliki ng'ombe elfu moja, kamuulize anazalisha maziwa kiasi gani. Au zinamsaidia nini. Tuwasaidie wafugaji sasa kwa motisha ya kila namna kwa wale ambao wanataka ufugaji wa kibiashara na si wa kuhesabu ng'ombe.

Tatizo langu kubwa ambalo ni tatizo la average Tanzanians ni ego iliyokuwepo....Ukisena wafugaji wapunguze mifugo yao kwanini usiseme wakulima pia wapunguze ukubwa wa mashamba yao? Na wewe upunguze amount of money in your account?

Lakini sasa ebu tuende kitaalamu...kati ya kupunguza mifugo ambayo ina serve multipurpose na kupunguza ukubwa washamba huku ukitumia technology sahihi kuongeza mazao katika eneo dogo lipi ni pragmatic solutions?

Pengine hufahamu...basi acha nikueleze kidogo kwa uchache...kwenye tropical production systems ng'ombe ambao wako ecologically correct na well adapted kwenye ecosystem zetu ni hawa local breeds...tafiti zinaonyesha kuwa wafugaji waasili ndiyo ambao wameweza kuishi na mazingira kwa ubora zaidi kuliko wale ambao wanafuga diery(sp?) ukichukulia ng'ombe kama mlengwa mkubwa katika ufugaji. Hii ni kwa sababu diery farming imeiletea majanga makubwa dunia ambapo mpaka sasa mharibifu mkubwa wa mazingira hasa kwakukata misitu na kuzalisha hewa ya ukaa nyingi kupita inayozalishwa na magari ni huo ufugaji wa diary farming....uki google utapata machapisho lukuki kuhusu hili...Sasa huo ufugaji wa kisasa ni upi?

Hii inanipeleka level 2 ya discussion yangu...kwamba huo ufugaji wa asili japokuwa ni sahihi kwa mazingira changamoto yake kubwa ni kukosekana kwa ardhi ambayo inahitajiwabkwa mambo mengi ikichagizwa na ongezeko la idadi ya watu. Hii basi ni kusema huo ufugaji pia lazimankwa sasa kutokana na changamoto hizo siyo endelevu lakini unatupa majibu ya msingi kwamba siyo kweli kuwa wafugaji ni wajinga bali kuna mambo ya msingi ambayo kwa ujinga wa science ya wakati huo yalionekana kuwa ni ujinga. Wataalamu kwakutambua hilo wameona ipo haja sasa ya kuunganisha elimu zote mbili ile yaasili iliyodumazwa kwakua haikupewa kipaumbele na ile ambao imeratibishwa yaani formal kuja na suluhisho katika changamoto zinazoikabilia dunia hasa katika sector ya ufugaji.

Wakulima wao kinyume na wafugaji elimu yao ipo na dunia imesonga sana mbele katika technology ya kilimo kuliko ilivyo kwa ufugaji hata hivyo pia ipo na ile ya asili kama ambavyo mifumo yetu inajieleza na hiyo ikiwa ndiyo njia sahihi ya kuendeleza kilimo chetu huku kikifuata uasili wa maeneo ya ki geography...Mfano ukijua kwa asili mahindi, mtama na maharagwe yalitokea katika mifumo gani ya ki ecology basi ni sharti mazao hao yalimwe huko...Kamwe usiende kulima mahindi kwenye maeneo ambapo siyo asili yake ili tuweze kupata kilimo endelevu. Hii pia italinda soko la ndani kwani watu watakuwa wakilima vitu tofauti tofauti na hivyo kutengeneza soko pale ambapo zao moja halipatikani.
 
Wewe unachoandika hapa ni usanii Tu, hatuko kwenye ujamaa na kujitegemea saizi. Kila mfugaji anamiliki mifugo yake na akiuza hela ni zake binafsi, lakini kwenye kuchunga mifugo wanachunga eneo linalomilikiwa na kijiji kizima, nini haki ya wasio na mifugo? Kila mkulima ana eneo lake defined na mkulima mwingine akitaka kulitumia anakodisha kwa hela au kuazima, kwa nini mfugaji asiwe na eneo lake?

Kumbe umeshaibadili katiba wewe?

Bahati nzuri mimi nilimpigia kura yangu Rais mjamaa..wewe wako bepari muda wake bado ukifika mtaleta sera zenu za wezi aka upebari uchwara..
 
Mama kawatetea wafugaji labda kwa vile na yeye ni wa huko
Ukweli ni kuwa wafugaji ni tatizo
Ugali ni muhimu kuliko nyama
Anasema tatizo lilianzia kwenye hizo hekta 70k......... Ina maana wafugaji wote tunao waona maeneo mbalimbali wakisababisha migogoro ni hao wa manyara peke yao?
mama kaongea uongo tu pia kaongelea upande mmoja,mtu mwenye ndoto ya urais anashindwa hata kufanya research kujua in and out kuhusu mgogoro wa wakulima na wafugaji countrywide
 
Duuh hapo sasa kazi ya serikali itakuwa ni ipi kama kila mtu ataamua kujishughulisha anavyotaka?

Ukielewa maana ya serikali na majukumu yake wala usingethubutu kusema haya.

Serikali yoyote duniani jukumu lake la kwanza na muhimu ni kuratibu shughuli za raia wake na ulinzi. Serikali isiyoratibu shughuli za raia wake inakosa uhalali wa kukusanya kodi kwa raia wake. Tuache kupotosha viongozi wetu, tuwasaidie ili nao waweze kuongoza kwa furaha na amani.
Sasa kwa mtu mwenye ng'ombe 3,000 serikali imtafutie eneo impimie halafu imgawie chukua hili eneo chungia mifugo yako? Hivi unatumia ubongo wako sawia. Huyu mfugaji hajui hata pasture ni kitu gani, analisha mifugo anarudi nyumbani kulala na mkewe, kesho anaenda kulisha eneo lingine ambalo hajawekeza hata shilingi utaepuka migogoro hapo kweli.

Mimi sio mkurupukaji au mwanasiasa kama wewe, mimi nimesomea mambo haya. Mimi ninafuga ng'ombe wangu kwenye eneo chini ya ekari kumi, sehemu ng'ombe walipokula ninahakikisha panatunzwa vizuri ili nyasi ziote tena lakini pia ninapanda nyasi na legumes zenye value kubwa zaidi. Wafugaji wetu wanategemea kuchunga maeneo ya bure ambayo mengi yana nyasi za hovyo hovyo hazina chakula kingi
 
Kumbuka mfugaji hami kutoka sehemu moja kwa ajili ya ardhi anahama kwa ajili ya malisho ya mifugo yake wafugaji weng wana ardh zao, tatizo ni malisho ya mifugo naukumbuke kwamba mifugo huharibu sana mazingira ambapo hupelekea ukame katika maeneo yao hivyo basi migogoro ya ardh hapa nchi itaisha tu pale ambapo wafugaji watakubar kuelimika ususan kwenye maswala ya ufugaji wa kisasa
 
Migogoro ya aridhi kati ya wafugaji na wakulima tumeyalea wenyewe, wafugaji wanao leta vurugu karibu nchi nzima wanajulikana - kwa nini Serikali inaruhusu group ya watu wachache wazunguke nchi nzima na mifugo yao wana haribu mazingira, kwa nini hawakai mikoani mwao wakafunzwa ufugaji wa kisasa na kuheshimu utunzaji wa mazingira kitu ambacho wao hawajali kabisa mikoa yao umegehuka jangwa kwa kupuuzia kutunza mazingira wanakata miti ovyo na kusababisha ukame, mambo yakiwendea vibaya mikoni mwao wanaswaga kundi la mifungo kwenda kufanya uharibifu kwa mikoa inayo jali utunzaji mazingira wakifika huko waharibu mashamba ya wakulima kuwatwanga risasi wakulima masikini, kutumia nguvu za pesa kuwaonea wakulima wanafanya wapendalo as if they own this country!!

Miaka ya zamani hasa wakati wa enzi za Kambarage sikuwahi kusikia Serikali ikishinikizwa eti itenge maeneo ya Wakulima na wafugaji, wafugaji walikuwa wanaishi mikoani mwao bila ya kulanda landa ovyo nchi nzima wanajifanyia wapendalo, wakikemewa walalamishi kama nini na vitisho juu, ujeuri tu - wajifunze ufugaji wa kisasa kama ilivyo Botswana, Uholanzi, Uingereza na Marekani.
 
jiongeze kiakili...

soma maelezo yangu alafu toa na ww mapendekezo yako.

tatizo la watz tupo kukosoa hoja pasipo mapendekezo au mawazo mapya.
Unayetakiwa kujiongeza akili ni wewe unayeshindwa kujibu japo swali jepesi! Narudia; huko Bonde la Rufiji hakuna wakulima na mashamba?!
 
wafugaji ni watu wa kuhama hama... ilipaswa kuwepo maeneo rasmi ambayo wakulima watakuwa wanazunguka kama nyumbu wanavyoishi.

tatizo wafugaji wanajitafutia maeneo ya malisho badala ya serikali kuwatengea maeneo yao.
Kwa akili yako mtu ana ng'ombe 500 -1000 hata akiwa na eneo unatarajia ataendelea kubaki kwenye eneo husika hata kama hamna majani?!

Ni mjinga tu ambae hataki kukubali ukweli kwamba tatizo la msingi hapa ni mtu kuwa na mifugo mingi ambayo ni ngumu kui-manage! Ukishakuwa na mifugo mingi kuliko unavyoweza kui-manage hutaacha kuhama hama never and ever kwa sababu siku zote watataka kuwa pale ambapo kuna malisho!

Popote utakapowapeleka watatulia hapo endapo tu kuna malisho na malisho yakiisha LAZIMA watahamia sehemu nyingine kwa sababu there's no way mfugaji ataacha ng'ombe wake wafe wakati upande wa pili kuna malisho ambayo very unfortunately ni mali za wakulima!
 
Mgogoro kati ya wakulima na wafugaji hauwezi kwisha...
Utakuta mfugaji mmoja ana miliki ngombe zaidi ya 100 inapokuja suala la kuwalisha ni shida...
Serikali ilitakiwa iwatengee wafugaji maeneo yaooo...maalum,

Ova

Serikali inetoa mwongozo wa kutenga maeneo...tatizo ni njia inayotumiwa katika kutenga maeneo....Maeneo yanatengwa katika ngazi ya vijiji ambapo ardhi ni ndogo kutimiza mahitaji ya wafugaji....Ng'ombe kama nyati ana aina ya majani na mazingira ya kula hatulii eneo moja kwababu ua mabadiliko ya hali ya hewa kwa masaa husika...kwenye tabia za wanyama mimi siyo mbobezi bali nafahamu kwa kidogo saba tabia hizo...

Sasa kwakua ukitenga ardhi kwa mfugaji mijamoja ardhi itakatohitajika pengine ni sawa na eneo lote la Tanzania na bado lisitoshe. Wafugaji wanatupa jawabu ndiyo maana umiliki wao tofauti na sehemu zingine duniani ambapo wametenga maeneo kwa wafugaji ambao kwanza ni wachache na wenye ng'ombe wachacje bila kusahau huko ndiko kwenye uharibifu mkubwa wa mazingira; kinyume chake wafugaji wetu kiasi hawamiliki ardhi mojamoja bali ki jamii...huo ndiuo mufumo sahihi mpaka sasa wa umiliki wa ardhi ya ufugaji. Tatizo lilokuwepo ambalo na amini sheria italirekbisha ni ardhi hiyo kutokulindwa na sheria za ardhi ya mila ambapo ardhi inayotambulika umiliki ni ile ya moja moja ambapo mrithi anatambulika. Huko kwa wafugaji kama sheria hiyo ingetambua mapungufi hayo basi pengine ardhi ya NAFCO kwa mfano ingetakiwa kuwa mali halali ya wabarbaig wa Hanang'. Sasa pasipo kupoteza pointi ni muhimu ardhibya wafugaji ikatengwa kitaifa kama ilivyofanyika kwa ile ya uhifadhi na kutengenezewa sheria kuwa mpaka uibadili lazima kuwe na ugumu na itengwe ikiwa imeungana ungana ili kuruhusu wanyama mifugo kuhama hama lakini humo humo kwenye eneo lao huku eneo moja likiunganishwa kwa stock routes mithili ya corrido...owe marufuku eneo hilo shughuli za kilimo kufanyika....

Pengine utaniuliza ardhi hiyo itatoka wapi?

Tunayo maeneo mengi ambayo ki ecology yanaweza yakatumiea kwa dual purpose...moja ni misitu ya jamii community based forests ambapo takwimu zinatuambia about 90% ya misitu tuliyonayo ni ya aina hiyo....kuna sehemu ambapo ng'ombe wanaweza kufugika ila tu kuwe na management principles ambazo wafugaji wata ridhia...Mbali na hayo maeneo yapo maeneo ambayo siku hizi wanataka kuyafanya kuwa WMA yaani Waildlife Management Areas...kwa asili wafugaji hasa walr wa kimasai na wabarbaig wameweza kuishi na wanyama pasipo na shida yoyote ile ila tu kuwe na mikataba kati ya hizo communities na wizara ya mali asili na pengine tutaongeza sana katika sector zote mbili za utalii na ufugaji kwani makabila hayo poa yamelinda sana culture zao ambazo zitaweza kutumiwa kuvutia watalii katika namna mpya ya partcipatory conservation approach na kwa jinsi hiyo mapato yatokanayo yakasaidia ku cntrol illegal deals na kuongeza welfare ya jamii ya kifugaji...

Pengine utasema wasukuma ni tatizo, kwangu mimi, siyo! Sababu kubwa nibkwamba wasukuma wanaweza kuishi sehemu ya kijiji kinachoruhusu kilimo na wakati huo huo bomabla ng'ombe likawa kwenye hayo maeneo mengine mimi nitayaita ya hifadhi ya ufugaji endelevu..

Ipo namna nyingi sana ya ku manage hizo natural resources huku tukiongeza tija na kupunguza externality kitumia theories na practices ambazo ni sustainable.
 
Tatizo langu kubwa ambalo ni tatizo la average Tanzanians ni ego iliyokuwepo....Ukisena wafugaji wapunguze mifugo yao kwanini usiseme wakulima pia wapunguze ukubwa wa mashamba yao? Na wewe upunguze amount of money in your account?

Lakini sasa ebu tuende kitaalamu...kati ya kupunguza mifugo ambayo ina serve multipurpose na kupunguza ukubwa washamba huku ukitumia technology sahihi kuongeza mazao katika eneo dogo lipi ni pragmatic solutions?

Pengine hufahamu...basi acha nikueleze kidogo kwa uchache...kwenye tropical production systems ng'ombe ambao wako ecologically correct na well adapted kwenye ecosystem zetu ni hawa local breeds...tafiti zinaonyesha kuwa wafugaji waasili ndiyo ambao wameweza kuishi na mazingira kwa ubora zaidi kuliko wale ambao wanafuga diery(sp?) ukichukulia ng'ombe kama mlengwa mkubwa katika ufugaji. Hii ni kwa sababu diery farming imeiletea majanga makubwa dunia ambapo mpaka sasa mharibifu mkubwa wa mazingira hasa kwakukata misitu na kuzalisha hewa ya ukaa nyingi kupita inayozalishwa na magari ni huo ufugaji wa diary farming....uki google utapata machapisho lukuki kuhusu hili...Sasa huo ufugaji wa kisasa ni upi?

Hii inanipeleka level 2 ya discussion yangu...kwamba huo ufugaji wa asili japokuwa ni sahihi kwa mazingira changamoto yake kubwa ni kukosekana kwa ardhi ambayo inahitajiwabkwa mambo mengi ikichagizwa na ongezeko la idadi ya watu. Hii basi ni kusema huo ufugaji pia lazimankwa sasa kutokana na changamoto hizo siyo endelevu lakini unatupa majibu ya msingi kwamba siyo kweli kuwa wafugaji ni wajinga bali kuna mambo ya msingi ambayo kwa ujinga wa science ya wakati huo yalionekana kuwa ni ujinga. Wataalamu kwakutambua hilo wameona ipo haja sasa ya kuunganisha elimu zote mbili ile yaasili iliyodumazwa kwakua haikupewa kipaumbele na ile ambao imeratibishwa yaani formal kuja na suluhisho katika changamoto zinazoikabilia dunia hasa katika sector ya ufugaji.

Wakulima wao kinyume na wafugaji elimu yao ipo na dunia imesonga sana mbele katika technology ya kilimo kuliko ilivyo kwa ufugaji hata hivyo pia ipo na ile ya asili kama ambavyo mifumo yetu inajieleza na hiyo ikiwa ndiyo njia sahihi ya kuendeleza kilimo chetu huku kikifuata uasili wa maeneo ya ki geography...Mfano ukijua kwa asili mahindi, mtama na maharagwe yalitokea katika mifumo gani ya ki ecology basi ni sharti mazao hao yalimwe huko...Kamwe usiende kulima mahindi kwenye maeneo ambapo siyo asili yake ili tuweze kupata kilimo endelevu. Hii pia italinda soko la ndani kwani watu watakuwa wakilima vitu tofauti tofauti na hivyo kutengeneza soko pale ambapo zao moja halipatikani.
Hii yaelekea kuwa ni fani yako au inakuhusu moja kwa moja maana maelezo yako ni ya ufasaha. Swali la msingi, hii tropical ipo Tanzania tu. Au haya matatizo yapo kwetu tu, na ni kwa nini? Kuna jamii nyingi za ufugaji tunaambiwa walikuwa wakihamahama, mbona madhara yale hayaonekani kama kwetu?
Umezungumzia athari ya kimazingira, pamoja na huo ulioita ubora wa ufugaji wa asili, je ufugaji huo una tija katika kipato. Ungekuwa una tija, leo hii hawa wafugaji wasingekuwa wana tapatapa. Literary, ufinyu wa kipato chao ndio mateso kwao. Kwanini wasiondokane na dhana ya kutangatanga hata kwenye huo ufugaji asili? Hivi wakulima na wao wangekuwa wanatangatanga, nini kingetokea. Huwezi kuzalisha lita 2 za maziwa kwa siku, basi ikawa ni lazima asili idumishwe. Hivi tungetegemea mifugo hiyo ya asili tungejitosheleza kwa mahitaji ya maziwa?
 
Back
Top Bottom