Anna Mghwira
R I P
- Mar 9, 2012
- 206
- 362
Migogoro ya ardhi imekuwa tatizo la muda mrefu nchini. Migogoro ya wakulima na wafugaji imevuka hali ya kawaida ya migogoro ya ardhi, sasa ni uhasama wa kundi moja dhidi ya kundi jingine. Migogoro imepata sura mpya na hadhi mpya kwa kila kundi. Kila wakati tumesikia hatua mbalimbali zikichukuliwa na serikali kutatua tatizo bila tatizo lenyewe kwisha: Kuna nini hasa?
Historia ya ardhi za nchi zilizokaliwa kikoloni ilihitaji kubadilishwa mara moja baada ya uhuru. Kwa sababu ardhi ndiyo ilikuwa mtaji mkuu wa uchumi wa kikoloni. Baada ya uhuru, ardhi inakuwa mtaji mkuu wa nchi huru, lakini afrika tumekataa uhuru wetu huo, wa ardhi na rasilimali zetu kwa ujumla. Tumewapa ama wakoloni wale wale ama wadau wa aina yao kumiliki rasilimali zetu. Hii ni moja ya changamoto za ardhi. Ardhi inakwa ndogo kwa matumizi yetu kwa sababu tumewapa waeni urithi huu. Tunakiri bila hofu kuwa utajiri wa asili umekwa laana ya asili badala ya kuwa Baraka ya asili.
Hapa Tanzania migogoro mingi iliyopo sasa inachangiwa na sera yetu ya siasa ni kilimo ambayo ilitoa kipaumbele cha maendeleo kwa wakulima na kuwanyima heshima hiyo hiyo wafugaji. Kwa muda mrefu tumewapuuza wafugaji. Tumeshindwa kuona thamani ya mchango wao mkubwa kwa pato la taifa. Kwa sababu hiyo kuna sera za kilmo zilizopitishwa ambazo zimekuwa kichocheo cha migogoro hii.
Mgogoro wa kwanza mkubwa kati ya wafugaji na wakulima ulianza pale wafugaji wa Ki-barbaig waliponyan’ganywa eneo la zaidi ya hekta elfu 70,000 miaka ya 60. Serikali ndiyo ilichukua eneo hili na kuanzisha mashamba ya ngano ya iliyokuwa NAFCO- Shirika la Umma la Kilimo cha ngano mkoani Manyara, wilaya ya Hanan’g. Tangu eneo hilo kubwa lichukuliwe awali na kampuni ya Ki-Kanada, baadae na serikali yetu, ardhi ya wafugaji imekuwa finyu na iliyojaa migogoro.
Serikali ikitaka kumaliza migogoro hii, ianzie pale. Iangalie hitilafu zilizojitokeza, dhuluma zilizofanyika kwa wananchi, na kuharibiwa kwa mfumo wa uzalishaji wa asili na wa kisasa wa ufugaji.
Kupitia sera ya Siasa ni Kilimo, serikali imefanikiwa kuwasaidia wakulima kwa kila hali, ifanye hivyo kwa wafugaji pia. Itajua kiini cha matatizo, na njia sahihi ya kuitatua. Kinachoonekana sasa ni kama kushughulikia matawi bila kugusa mizizi.
Sera yetu ya uwekezaji, sheria na taratibu zake na utekelezaji wake nazo ni changamoto nyingine. Hizi zinahitaji mabadiliko ya kikatiba kukidhi haja na hoja zote za umiliki na matumizi ya rasilimali zote za asili. Tunahitaji kuona mizizi ya matatizo haya ikishughulikiwa, si matawi yake.